Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, September 26, 2018

Walimu Hazina mbaroni kwa kuwapa wanafunzi darasa la saba mitihani

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kimataifa ya Hazina, Patrick Cheche na walimu wenzake wanne wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwapa maudhui ya mtihani wa taifa wa darasa la saba watahiniwa wa shule hiyo.

Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo Jumatano Septemba 26 na kusomewa  mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono.

Wakili Kombakono aliwaja washtakiwa hao kuwa ni,  Mwalimu Cheche, Laurence Ochieng, Justus James, Nasri Mohammed na Mambo Iddi.

Washtakiwa hao wanadaiwa Septemba 5, mwaka huu waliingilia mitihani ya taifa isivyo halali, walipata kwa makusudi wakawaonyesha watahiniwa maudhui ya mitihani hiyo ambapo walikana mashtaka hayo, kesi hiyo itatajwa Oktoba 10 mwaka huu.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )