Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, September 22, 2018

Updates: Waliofariki Kivuko cha MV Nyerere Wafika 148

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kilichozama katika eneo la Bwisya, takribani mita 100 kabla ya kufika bandari ya Ukara imefikia 148, huku kazi ya ukoaji likiendelea.

Kivuko hicho kinachofanya safari kwa kusafirisha abiria na mizigo kati ya Ukara na Bugorora wilayani Ukerewe, kilizama juzi majira ya saa 8:10 mchana baada ya kutoka katika bandari ya Bugorora kwenda Ukara.

Kutokana na ajali hiyo, watu 40 pekee ndio waliookolewa wakiwa hai na 136 waliopolewa wakiwa wameshafariki dunia hadi jana jioni.

Leo Septemba 22, 2018 asubuhi Miili mingine 12 imeopolewa  na hivyo kufanya miili iliyopatikana hadi sasa kufikia 148.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )