Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, September 9, 2018

Wizara Ya Mambo Ya Ndani Yatuma Rambirambi Kwa Wafiwa Wa Ajali Iliyotokea Jijini Mbeya

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inatoa pole kwa familia zote ambazo zimepoteza ndugu na jamaa zao na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matano, iliyotokea katika eneo la Igawilo Mjini Mbeya siku ya tarehe 7 Septemba, 2018 na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi wengine.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Kangi Alphaxard Lugola, (MB), kwa masikitiko makubwa anatoa pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao na kuwatakia majeruhi wote ahueni ya haraka ili warejee katika hali zao za kawaida na kuendelea na shughuli zao za kujenga nchi.

“Natoa pole nyingi kwa Watanzania wenzangu waliowapoteza wapendwa wao katika ajali hii na nawatakia majeruhi wote afya njema na wapate ahueni haraka ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida”.

“Ni wakati muafaka kwa Watanzania wenzangu, Wasimamizi wa Sheria za Usalama Barabarani na Madereva kutokatishwa tamaa na ajali hii na badala yake changamoto hii iwafanye waongeze umakini barabarani, kuongeza umadhubuti katika usimamizi wa Sheria ya Usalama barabarani kwa kuchukua hatua kali zaidi kwa madereva wazembe na askari wasiotimiza wajibu wako wa kuhakikisha magari mabovu hayaruhusiwi kutembea barabarani”.

Mwenyezi Mungu azipe roho za ndugu zetu pumziko la amani. Amina

Imetolewa na:
Meja Jenerali Jacob G. Kingu, ndc
KATIBU MKUU
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )