Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, October 13, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 101 na 102 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 

Nikamvuta taratibu K2 kwa kutumia darubini ya hii bunduki. Nilipo hakikisha msalaba mwekundu ninao uona kwenye hii darubini umekaa vizuri kichwani mwake, taratibu nikaikoki bunduki, huku nikishusha pumzi nyingi. Nikamuangalia K2 jinsi anavyo furahi na wananchi huku akiwapa mikono ya hongera. Gafla mwili mzima ukaanza kunitetemeka huku jasho jingi likinimwahika mwili mzima. Nikajaribu kuhakikisha kwamba ninajikaza kumuweka K2 katika tageti yangu, ila ninashindwa kabisa. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi, taratibu nikajaribu kunyanyuka ila nikashindwa kabisa na kujikuta nikiiangusha bunduki pembeni na kulala chali, huku nikitazama juu na kuona jinsi dunia inavyo zunguka kwa kasi jambo ambalo kwenye maisha yangu sikuwahi kuliona hata siku moja.
       
 ENDELEA   
Nikaendelea kulala chini huku nikijishangaa sana kwa kitu hichi ambacho kimetokea kwenye maisha yangu. Taratibu nikajikaza kunyanyuka ila kwa kizunguzungu hichi nilicho nacho, nikajikuta nikishindwa kabisa na kurudi kulala chini tena. Zikapita zaidi ya dakika ishirini, nikajikuta nikipata nguvu na kunyanyuka tena. Nikachungulia eneo la uwanjani ila sikumuoa raisi katika eneo ambalo alikushudiwa kukaa.
“Sniper namba moja uanipata?”
Nilisikia sauti ya Babyanka kwenye masikio yangu, nikamtazama askari wa NSS, niliye mpiga kwa kitako cha bastola yangu akiwa amelala chini bado hajapata fahamu yoyote.
“Yaaa”    
 
Nilijibu kwa kifupi ili sauti yangu kuto kujulikana kwa maana imeniwia urahisi kufahamu kwamba huyu ni mdunguaji namba moja kutokana na ukaaji wake na sehemu aliyopo, kwa maana sio jambo geni kwangu  kwa maana mimi mwenyewe nilisha wahi kuwa katika kiosi cha NSS na ninawajua A hadi Z.
“Raisi yupo katika kugagua mabanda ya biashara”
“Nimekupata”
Nikaichukua bunduki na kuishika vizuri, nikaiweka sawa shemu ilipo kuwa kwa maana ina viguu vyake viwili  vya kusimamia hii ni kutokana na uzito wake. Nikaanza kupitosha pitisha macho yangu kwenye mabanda ya biashara ambapo raisi anakagua miradi ya biashara.
 
Nikaona kundi la walinzi kwenye moja ya jengo la biashara, nikatambua kwenye hilo banda ndani ni lazima K2 atakuwemo. Nikaikoki bunduki vizuri nikakadiria ni mita ngapi kutoka hapa nilipo hadi kwenye banda hilo, nikaiweka bunduki sawa, huku nikishusha pumzi yangu.
‘Toka toka’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikitazama kutitia darubini, sikumuona raisi. Nikaona baadhi ya wafanyakazi wa hilo banda wakitoka mmoja baada ya mwingine, nikagundua ni lazima raisi atakuwa anatoka, nikabana pumzi yangu vizuri kuhakikisha kwamba riasi nitakayo ipiga inafika kwa mtu sahihi na muda sahihi ambao nimepanga mimi uweze kufika kwake.
 
“Nikamuona K2 akitoka, ila kuna mzee mnene akiwa amemziba na hakuna sehemu ambayo ninaweza kumpiga risasi na akafaa kwa maana ninaiona mikono na muguu yake, kichwa wala kiwili wili chake sikioni.
‘Comoonnnnn mzee ondoka hapo’
Nilizungumza huku nikiwa ninahasira sana.
“Freeziiiii”
Nilisikia sauti kali ya kike nyuma yangu, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi kwa maana ninesha kamatwa.
“Ukifanya ujinga wowote nitakuua”
Sauti hii ninaitambua kabisa ni sauti ya Babyanka.
“Kuna muuaji nimempata gorofani, timu nzima mlindeni rai……”
 
Sikutaka Babyanka amalizie sentensi yake, kwa haraka nikajigeuza na kumpiga mtama mkali Babyanka na kumfanya anguke chini. Kofia la sweta nililo vaa kichwani mwangu likafunuka na kumfanya Babyanka kunitolea macho.
“Dany!!”
Sikutaka kumjibu kitu chochote kwa maana ninatambua Babyanka ananifahamu vizuri na hana uwezo wa kunipiga riasi kwa maana anatembua na kuelewa kila kitu kilicho tokea kwenye maisha yangu. Nikaanza kutembea kuelekea sehemu ulipo mlango.
 
“Simama nitakupiga risasi”   
Babyanka alizungumza kwa ukali sana, nikasimama na kugeuka nyuma huku nikimtazama kwa macho makali sana usoni mwake.
“Timu mzima, kuna muuaji, narudia tena kuna muuaji kwenye gorofa namba moja. Sniper namba moja yupo chini”
Babyanka aliendelea kuwasiliana na wezake huku akiwa ameninyooshea bastola yake, nikatambua kabisa upendo wa Babyanka umetoweka juu yangu. Taratibu nikaanza kutafuta njia ya kuvuta bastola yangu niliyo ichomeka kwenye soski mguuni.
“Dany kwa nini unahitaji kumuua raisi. Huyui kwamba amechaguliwa na mamilioni ya Watanza”
 
Babyanka alizungumza kwa sauti ya upole, nikatambua lengo lake la kuzungumza hivyo. Antaka kunizubaisha ili mradi wezake waweze kufika katika eneo hili na kunikamta kirahisi. Askari niliye mpiga kwa kitako cha bunduki akanza kunyanyuka huku akijivuta vuta chini jambo lililo toa mlio na kumfanya Babyanka kutazama nyuma.

 Kwa kasi ya ajabu nikachomo bastoka yangu mguuni. Nikampiga risasi Babyanka ya kifuani mwake na akaanguka chini. Ninatambua kabisa kwamba sehemu hiyo niliyo mpiga si rahisi kwa yeye kuweza kufa hii ni kutokana na jaketi la kuzuia risasi alilo livaa. Kwa kasi ya ajabu nikaufungua mlango wa kuingilia kwenye za kushuka kwenye hili gorofa. Nikaanza kushuka kwa haraka, ila ikafikia sehemu ikanibidi kusita kidogo, nikachungulia chini, nikawaona wana askari wa kikosi cha NSS, wakipanda kwa kasi huku wakiwa na bunduki zao.
 
Sehemu niliyopo haina mlango kabisa ambao ninaweza kusema kwamba ninaweza kuingia. Ikanilazimu kuanza kupandisha juu kwa kasi. Juu napo nikamuona Babyanka na yule askari ambaye nilikuwa nimepiga kwa kitako cha bastola wakishuka kwenye ngazi kwa kasi huku kila mmoja akiwa ameshika bastola yake. 
 
Nikafyatua risasi sehemu wanapo shuka Babyanka na askari wake. Ikawawafanya askari wanao pandisha ngazi kujiahami kwa kufyatua risasi pasipo kutambua ni sehemu gani ambayo mimi nipo.
Nikaanza kujibu mashambulizi ya askari wote, wanao panda na wanao shuka, kwa bahati nzuri sehemu niliyo kuna mlango wa kuingilia kwenye chumba ambacho wala sitambui kina kitu gani ndani.
 
Nikaupiga kikumbo mlango huu, ila haukufunguka kwa kutumia bastola nipiga risasi kadhaa kwenye kitasha cha mlango, kisha nikaupiga kikumbo na ukafunguka. Chumba hichi kinacho tumika kama stoo, kina dirisha mmoja la vioo. Kwa haraka nikalisogelea dirisha hili, nikachungulia chini, nikaona kuna uwazi mdogo sana ambao ninaweza kupita kwa maana mbele kuna ukuta mwengine wa gorofa. Pembeni ya hili dirisha kuna bomba la maji ambalo ninaweza kulitumia kushuka chini kwa haraka. Akili yangu inayo fanya kazi kama compyuta, ikanituma kufanya hivyo. Kwa kasi ya ajabu nikaanza kushuka kuelekea chini. Nikafanikiwa kufika chini, sikuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kuanza kukimbia kwenye kijiuchochoro hichi ambacho ni chembamba sana.
 
Nikafanikiwa kuingia kwenye moja ya nyumba eneo la uwani. Kwenye nguo ya hii nyumba kuna kamba iliyo anikwa nguo za kiume. Nikazichukua kwa haraka nguo hizi ambazo sikuli kama ni mbichi au zimekauka. Nikaona mlango wa chumba uliopo wazi, Kwa haraka nikabadilisha nguo zangu na kuvaa nguo hizi huku jaketi langu la kuzuia risasi nikiwa nimelivaa juu ya hii tisheti.
 
Nikachungulia nje, sikuona watu nikatoka kama mtu wa kaiwada na kuanza kutembea kwenye kordo ya hii nyumba. Nikafika mlango wa mbele, nikachungulia nje, nikaona gari za askari zikikatiza kila sehemu huku askari wa kikosi cha NSS wakikimbia wakihisi nimelekea huko wanapo eleka.
 
Raia ambao nao wamesikia milio ya risasi kila mmoja alihitaji kuokoa maisha yake. Nikatazama mazingira jinsi yalivyo kaa. Nikajitama na jaketi langu hili la kuzuia risasi, lipo tofauti na askari wa vikosi vyote waliopo katika hili eneo. Sikuwa na jinsi zaidi ya kulivua. Nijajichanganya kwenye kundi la wananchi wanao jaribu kuyaokoa maisha yao. Kitu kikubwa ambacho kinanisaidia ni hichi kifaa cha mawasiliano kilichopo masikioni mwangu, ninaweza kunasa mawasiliano ya wana NSS ambayo yaliweza kuniongoza na kupita sehemu ambazo wao hawapo. Kwa kutembea kwa kujihami na kujificha ficha nikafanikiwa kufika eneo la Makorora. Nikakivua kifaa hichi cha mawasiliano kwa maana nikizungumza na mtu basi sauti yangu itasikika. Nikakiangusha chini na kukikanyaga kwa kiatu na kukiponda ponda. Nikatembea hasi sehemu walipo waendesha pikipiki
“Inakuwaje wana”
 
“Poa vipi chief”
“Poa, oya mwana nirushe hapo Sahare”
“Buku nne mwana”
“Hakuna tabu”
“Oya wana ngona nimpeleke mchizi”
Dereva bodaboda, akawasha pikipiki yake, na mimi nikapanda tukaondoka eneo hili.
“Nasikia Tangamano kimenuka?”
“Kimetokea kitu gani?”
“Nasikia kuna milio ya risasi, wananchi wametawanyika kila mmoja ameokoa roho yake”
“Ahaaa, mimi sijaisikia hiyo ishu”
“Ahaa mwana kimenuka kishenzi aisee, yaani raisi timu, sijui hata raisi kama amesalimika”
Dereva huyu wa pikipiki aliendelea kunipa taarifa na mimi nikajifanya mgeni sana katika taarifa hii.
 
“Duu ila si anawalinzi raisi”
“Yaaa alafu raisi mwenyewe demu yaani tabu tupu”
“Ila si tulimchagua kwa kura zetu”
“Ahaa mimi sikumpa kura, nilikuwa ninamkubali yule raisi aliye pita ila sijui kwa nini aliumwa”
“Ahaa hayo ni mambo yao wenyewe.”
“Kweli kaka”
Nikamuelekeza hadi mtaa ambao ninaishi. Kitu kikubwa kilicho niumiza kichwa ni pesa, kwa maana nimeacha pesa zangu kwenye suruali niliyo ivaa, na nilijisahau kabisa kukagua mifuko ya suruali ambayo nimeivua. Nikaanza kuigiza kujipapasa mifukoni mwangu nikiwa kama sielewi hali halisi niliyo nayo.
“Vipi?”
Dereva boda boda aliniuliza huku akiwa amenitumbulia macho ya mshangao.
 
“Natafuta waleti yangu siioni mwana”
“Ahaa itakuwaje sasa?”
Dereva bodaboda sauti yake nikaona ikibadilika na kueleka katika hali ya hasira. Gari ya Cajoli ikasimama pembeni yetu.
“D”
Cajo aliniita baada ya kufungua kioo cha gari nikasogelea kwenye gari.
“Nipatie elfu tano”
Cajoli akanipatia shilingi elfu tano, nikampatia dereva bodaboda ambaye muda wote alikuwa akinitumbulia macho tu.
“Kaka pesa yako, shukrani”
Nikaingia kwenye gari na kuondoka na Cajoli.
“Nimesikia kuna tatizo limetokea Tangamano, wewe ndio umesababisha?”
“Ndio”
“Dany huoni kwamba hii hali itakuwa ni hatari kwako?”
“Natambua, ila nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda kutulia, ulikuwa unatoka wapi?”
 
“Nilikuwa ninakwenda huko Tangamano kushuhudia kwa maana niliona kwenye tv cha kumshukuru Mungu nimewexa kukukuta hapa”
Tukafika nyumbani n amoja kwa moja tukaelekea chumbani baada ya kushuka kwenye gari.
“Siamini kama nimeshindwa kumuua raisi”
“Dany ni kitu gani ambacho uliniahidi?”
“Yaa nilikuahidi, ila nikipata nafasi ni lazima nimuue”
“Dany”
“Cajoli hili swala ninakuomba usiliingilie kabisa natambua ni nini ninacho kifanya”
Nilizungumza kwa kufoka hadi Cajoli akaka kimya huku mwili ukimtetemeka kwa maana Cajoli kwa siku hizi mbili tangu tuanzishe uhusiano watu hakuwahi kuniona nikiwa nimekasirika kwa kiasi hichi.
 
“Am sorry mume wangu”
Cajoli alizungumza kwa sauti ya upole huku machozi yakianza kimwagika usoni mwake. Taratibu nikamshogelea na kumkumbatia.
“Usijali mke wangu nimekusamehe”
“Nimezungumza hayo yote kwa ajili ya upendo wangu tu kwako, sihitaji uondoke mikononi mwangu nimesha kuzoea.”
“Nimekuzoea pia mke wangu”
Nikamuachia Cajoli na kuwasha Tv, taarifa ambayo inaonyeshwa kwa wakati huu ni kusiana na tukio zima mashambulizi yaliyo tokea katika uwanja wa Tangamano. Muandishi akamuhoji mkuu wa ulinzi ambaye ni Babyanka kuhusiana tukio lililo tokea.
“GAIDI AMBAYE TUNAMTAFUTA ANAJULIKANA KWA JINA LA DANY, PICHA ZAKE TUTAANZA KUZISAMBAZA MUDA MFUPI KUANZIA HIVI SASA KWENYE VYOMBO VYA HABARI. ILA NINACHO TAKA KUMUELEZA DANY, POPOTE ULIPO NAJUA BADO UPO TANGA NITAHAJIKISHA SAA SITA USIKU HAIFIKI NITAKUWA NIMEKUKAMATA NA SHERIA ITACHUKUA SHERIA YAKE.”
Maeno ya Babyanka yakanifanya nichukue rimoti ya Tv na kuizima, Cajoli akabaki akiwa amenitumbulia macho na kukosa cha kuzungumza.

AISIIIII……….U KILL ME 102                                                                                                


Nikazima tv na kuirudisha rimoti juu ya meza. Nikaka kwenye sofa huku kichwa changu kikiwa kimejawa na mawazo mengi sana.
“Dany si wanaweza kuja hadi hapa?”   
“Sidhani, ila ninahitaji kuondoka hapa”
“Uondoke hapa!!?”
“Natambua utapata sana shida wakifahamu kwamba mimi nipo hapa”
“Dany no, siwezi kuruhusu hilo swala kuweza kutokea kwako, ni bora hata ufikiria mbinu nyingine ya kufanya ila si kuondoka hapa Dany”
“Cajoli ila hii unaona hii ni hatari kwenye maisha yako”
“Vyovyote Dany ila sitaki uondoke kwanguu”
Cajoli alizungumza huku akimwagikwa na machozi mfululizo. Nikakaa kimya huku nikiendelea kufikiria ni mbinu gani nyingine ambayo ninaweza kuifanya”
 
“Ok nimefikiria mbinu nyingine”
“Mbinu gani?”
“Nahitaji kukua”
“Kukua?”
“Ndio”
Nikanyanyuka kwenye sofa na kueleka katika chumba ambacho kina silaha ambazo tulizihifadhi.
“Dany ila maneno yako kusema kweli sijayaelewa”
“Najua kwa sasa hivi huto weza kuielewa”
“Naomba unifafanulie kwa maana mimi ndio mtu wako wa karibu ambaye unaweza kunieleza kila kitu kinacho kusumbua”
“Cajoli nimeishia kwa miaka minne sasa, nikiwa ninaonekana kwamba mimi ni gaidi, ila kusema la ukweli mimi sio gaidi, nilikuwa ni mpelelezi katika kikosi cha NSS”
“Imekuwaje ukaonekana wewe ni gaidi?”
“Ni mambomengi ambao yametokea, kwenye maisha yangu, nikianza kukusimulia ninaamini leo hii itaishia nikiwa ninakusimulia”
 
“Niambie kwa kifupi tu Dany, au huniamini?”
Nikamtazama Cajoli usoni mwake, taratibu nikaanza kumsimulia historia ya maisha yangu kwa ufupi. Kitu nilicho kiepuka ni kumsimulia kuhusiana na maswala ya mahusiano ambayo niliyapitia hapo nyuma.
“Kwa sasa sihitaji kuwa mtu mwema”   
Nilizungumza huku nikiwa nimeyakaza meno yangu kwa hasira kwa maana maisha yangu yameharibika kutokana na mambo ya ajabu ajabu kwenye hii nchini. Watu wachache wananifanya nishindwe kuishi kwa amani, nishindwe kufanya mambo yangu kwa uhuru kama mwananchi wa kawaida ambaye ninahitaji kuyafurahia haya maisha kama wananchi wengine.
 
“Dany”
“Mmmmm”
“Nipo tayari kuhakikisha kwamba unakuwa mtu yoyote. Nimeumbwa kwa ajili yako, nipo kwa ajili ya kukusaidia, hukustahili kupitia magumu yote hayo ambayo umeyapitia. Bado kijana mdogo, laiti leo hii usinge kuwa umepitia matatizo hayo uliyo nieleza, ninaamini leo hii ungekuwa mbali sana”
“Yaa”
“Sasa unataka kuwa nani?”
“Gaidi, gaidi kama wanaye msema wao”
“Hata mimi nipo tayari kwa hilo”
“Real”
“Ndio Dany”
Tukajikuta tukikumbatiana kwa nguvu huku kila mmoja akilia kwa uchungu, ninamshukuru Mungu kwa kunipatia Cajoli, japo nimepitia mambo mengi, ila Cajoli amekuwa ni msichana anaye jitoa maisha yake kwangu mimi, japo wapo wengi ambao walijitoa maisha yao kwa ajili yangu ila kila mmoja alikuwa na malengo yake kwenye haya maisha.
 
“Nakupenda sana Dany”
“Ninakupenda pia honey”
Taratibu tukajiuta tukianza kunyonyana midomo yetu, hisia za mapenzi zikaitawala miili yetu. Tukaanza kupeana raha ambayo inastahili kwenye mahusiano yetu, baada ya kuhakikisha kwamba tumeridhika na kila mmoja amepata haki kwa mwenzake, tukaingia bafuni na kuoga.
“Nahitaji umpigie shem Cajoli”   
“Nimueleze nini?”
“Nahitaji kuitingisha serikali kwa huu mpango ninao uhitaji kuufanya. Nahitaji viongozi wote walio ingia madarakani kwa njia za short cut, nilazima watoke”
“Sawa”
Cajoli akachukua simu yake na  kumpigia Cajoli.
“Unaweza kuja kwangu”
“Nakuomba ufanye hivyo”
“Poa best”
Cajoli akakata simu na kurudi kitandani nilipo kaa.
“Anakuja ndani ya dakika kumi atakuwa hapa”
 
“Yupo hapa hapa town?”
“Sijamuuliza, ila huwa Cajol akisema dakika kumi, basi ni kumi kweli”
“Unaweza ukaniletea zile nguo nyeusi nilizo zichukua kwa Cajoli”
“Yaa zipo humu kabatini”
Cajol akanitolea nguo hizo ambazo zipo kwa ajili ya mapambano tu. Nikazivaa, na kujitazama kwenye kioo vizuri.
“Hapa kazi inakwenda kuanza leo hii”
Ndani ya dakika kumi, Cajoli akafika nyumbani kwetu.
“Shem wewe ndio umesababisha varangati lile?”
“Yaani wee acha tu”
“Mmmm ni shida aiseee kumbe una mtiti yaani huko njiani magari full kukaguliwa. Tanga sijawahi kuona foleni ila leo foleni ipo”
“Watanisaka sana, ila nahitaji kuwakomesha kwa aina nyingine”
“Kiaina gani”
 
“Nahitaji kutega bomu la nyuklia na ninahitaji raisi atoke madarakani”
Cajoli wote wakaka kimya huku kila mmoja akitafakari ni nini cha kunishauri kwa maana swala la bumu tena la nyuklia ni swala jengine sana kwenye maisha haya ya Waanzania.
“Dany”
“Ndio shem”
“Unajua uzito wa bomu la nyuklia?”
“Ndio ninafahamu”
“Unajua madhara yake yanakuwaje?”
“Cajoli hadi kuzungumza hivyo ujue ninatambua kila kitu. Mimi nilikuwa ni agent wa NSS, hao unao waona sasa hivi barabarani wakinitafuta, mimi nilikuwa ni miongoni mwao”
“Dany mume wangu, ila hili swala tulitazame kwa jicho jengine, kuna mamilioni ya watu ambao hawana hatia kwenye kisasi chako, sasa kwa nini unataka hao nao wahusike kwenye vifo vya bomu hilo”
 
“Hamjanielewa maana yangu. Nilikuwa nina maanisha kwamba kwa kutumia bomu hilo nitaji raisi kuweza kuachia madaraka”
“Asipo achia na bomu unalo inakuwaje hapo shem?”
“Nina lilipua”
Taratibu nikamuona Cajoli akikaa kwenye sofa huku akionekana kuchoka, ninahisi moyoni mwake anajutia sana kuwa katika mahusiano na mimi.
“Shem”
“Naam”
“Hili swala ni kubwa sana, ninakuomba tufikirie mbinu nyingine”
“Munahitaji kunisaidia au laa?”
Nilizungumza kwa ukali hadi wote wakastuka.
“Tupo tayari kukusaidia”
“Shukrani shem, kuanzia sasa sihitaji muwasiliane na watu wengine zaidi yangu mimi”
“Sawa”
 
“Natambua NSS akili zao, kwa sasa wananitafuta kwenye barabara, viwanja vya ndege, baharini. Huku kwenye majumba hawatoweza  kunitafuta. Kama itawezekana nalihitaji lile bomu”
“Dany kusema kweli bomu kulileta  mjini hapa kwa njia ya gari ni ngumu sana. Labda cha kukushauri hapa twende Kange kule tunaweza kupanga kila kitu”
“Wazo zuri, honey nikuombe kitu?”
“Ndio”
“Nakupenda sana mke wangu, ninakuomba hili swala niweze kulifanya mimi na shem”
“Cajoli ni mtu muhimu kwetu ana uwezo mkubwa sana katika maswala ya computer na ugunduzi. Best au bado hukumueleza mumeo juu ya kipaji chako”
“Nilihitaji kumfanyia suprize, ili nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda vizuri”
“Basi nyinyi mutakwenda pamoja mimi nitajua wapi kwa kupitia”
“Sawa, ila itahitajika pikipiki kuhakikisha kwamba unafika kwa wakati”
 
“Pikipiki itapatikana wapi?”
“Ngoja niwasiliane na Hassani”
Shem Cajoli alizungumza, sikutaka kumzuia kwa maana ili niweze kufika kange kwa nja rahisi ni kuhakikisha kwamba ninapata pikipiki.
“Niletee pikipiki hapa kwa wajina”   
“Nahitaji mpya yenye uwezo mkubwa. Iwe full tank”
“Acha kunihoji mswali mengi wakati maelekozo nimekupatia”
Cajoli akakata simu na kututazama.
“Pikipiki italetwa baada ya muda mchache kuanzia sasa”
“Sawa, jiandaeni kwenda Kange. Hivi sasa ni saa mbili kasoro usiku”
 
Cajoli na mwenzake hawakupinga chochote, wakaanza kujianda. Haukupita muda mwingi Hassani akaleta pikipiki aina ya boksa, akamkabidhi shem Cajoli, kisha jamaa akaondoka pasipo kielewa kitu kinacho endelea.
“Mlinzi weko hivi anatambua uwepo wangu?”
“Sidhani honey”
“Kwa shem, mlizi hakuwahi kukuona?”
“Nikirudi nipo ndani ya gari, nikishuka ninaingia ndani. Hajawahi kuniona kabisa”
“Ngoja nimpe likizo”   
Cajoli akatoka na kuniacha na shemeji. Kwa kupitia dirishani nikamuona akizungumza na mlinzi. Kisha akarudi ndani, akachukua kiasi cha pesa na kwenda kumkabidhi mlinzi huyu ambaye hakuonekana kurishishwa na maamuzi haya ya muda mfupi.
 
“Sisi utatukuta Kange”   
“Sawa kuweni makini”
“Poa”
Cajoli na rafiki yake wakaondoka hapa nyumbani huku kila mtu akitumia gari lake. Nikakaa kwenye sofa huku nikisubiria masaa yazidi kusonga mbele ili hata nikuondoka basi asinione mtu yoyote. Nikawasha tv na kukuta habari yangu ikiwa ndio inatawala kwa wakati huu. Picha zangu zinarushwa kwenye kila kituo cha televishion huku mtu ambaye atafanikisha kukamatwa kwangu atazawadia shilingi bilioni moja ya Kitanzania.
 
“Wenda wazimu nyinyi”
Nilijikuta nikizungumza huku nikielekea ndani ya chumba chenye begi lenye silaha. Nikachukua begi na kurudi nalo sebleni. Nikaanza kukiko bastola moja baada ya nyingine huku nikizichomeka sehemu mbali mbali katika mwili wangu, nikianzia kiunoni hadi miguuni, na uzuri wa suruali niliyo ivaa ina sehemu nyingi ya kufichia silaha.
 
Ilipo timu saa tano kamili usiku nikatoka nje na begi langu. Nikaliweka kwenye pikipiki vizuri. Nikaufunga mlango wa kuingilia ndani kwa Cajoli kisha funguo nikaificha kwenye kopo la maua lililopo karibu na mlango. 

Nikapanda pikipiki, taratibu nikatoka getini huku nikiwa nimevaa kofia maalumu la pikipiki, kwenye viganja nimevaa glovos ngumu na zenye rangi nyeusi kuhakikisha kwamba mikono haitelezi. Safari yangu nikainza huku nikiwa makini sana kila ninapo pita. 

Nikiwa katika maeno ya msikiti wa Madina, gari mbili za polisi nikaziona zikija nyuma yangu kwa kasi huku zikiwasha ving’ora, jambo lililo nifanya nizidi kuongenza mwendo kasi wa piki piki yangu aina ya Boxer, ambazo husifika kwa mwendo kasi barabarani.

==>>ITAENDELEA KESHO
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )