Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, October 15, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 102 na 103 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

“GAIDI AMBAYE TUNAMTAFUTA ANAJULIKANA KWA JINA LA DANY, PICHA ZAKE TUTAANZA KUZISAMBAZA MUDA MFUPI KUANZIA HIVI SASA KWENYE VYOMBO VYA HABARI. ILA NINACHO TAKA KUMUELEZA DANY, POPOTE ULIPO NAJUA BADO UPO TANGA NITAHAJIKISHA SAA SITA USIKU HAIFIKI NITAKUWA NIMEKUKAMATA NA SHERIA ITACHUKUA SHERIA YAKE.”
Maeno ya Babyanka yakanifanya nichukue rimoti ya Tv na kuizima, Cajoli akabaki akiwa amenitumbulia macho na kukosa cha kuzungumza.
   
ENDELEA   
Nikazima tv na kuirudisha rimoti juu ya meza. Nikaka kwenye sofa huku kichwa changu kikiwa kimejawa na mawazo mengi sana.
“Dany si wanaweza kuja hadi hapa?”   
“Sidhani, ila ninahitaji kuondoka hapa”
“Uondoke hapa!!?”
“Natambua utapata sana shida wakifahamu kwamba mimi nipo hapa”
“Dany no, siwezi kuruhusu hilo swala kuweza kutokea kwako, ni bora hata ufikiria mbinu nyingine ya kufanya ila si kuondoka hapa Dany”
“Cajoli ila hii unaona hii ni hatari kwenye maisha yako”
“Vyovyote Dany ila sitaki uondoke kwanguu”
Cajoli alizungumza huku akimwagikwa na machozi mfululizo. Nikakaa kimya huku nikiendelea kufikiria ni mbinu gani nyingine ambayo ninaweza kuifanya”
“Ok nimefikiria mbinu nyingine”
“Mbinu gani?”
“Nahitaji kukua”
“Kukua?”
“Ndio”
 
Nikanyanyuka kwenye sofa na kueleka katika chumba ambacho kina silaha ambazo tulizihifadhi.
“Dany ila maneno yako kusema kweli sijayaelewa”
“Najua kwa sasa hivi huto weza kuielewa”
“Naomba unifafanulie kwa maana mimi ndio mtu wako wa karibu ambaye unaweza kunieleza kila kitu kinacho kusumbua”
“Cajoli nimeishia kwa miaka minne sasa, nikiwa ninaonekana kwamba mimi ni gaidi, ila kusema la ukweli mimi sio gaidi, nilikuwa ni mpelelezi katika kikosi cha NSS”
“Imekuwaje ukaonekana wewe ni gaidi?”
 
“Ni mambomengi ambao yametokea, kwenye maisha yangu, nikianza kukusimulia ninaamini leo hii itaishia nikiwa ninakusimulia”
“Niambie kwa kifupi tu Dany, au huniamini?”
Nikamtazama Cajoli usoni mwake, taratibu nikaanza kumsimulia historia ya maisha yangu kwa ufupi. Kitu nilicho kiepuka ni kumsimulia kuhusiana na maswala ya mahusiano ambayo niliyapitia hapo nyuma.
“Kwa sasa sihitaji kuwa mtu mwema”   
Nilizungumza huku nikiwa nimeyakaza meno yangu kwa hasira kwa maana maisha yangu yameharibika kutokana na mambo ya ajabu ajabu kwenye hii nchini. Watu wachache wananifanya nishindwe kuishi kwa amani, nishindwe kufanya mambo yangu kwa uhuru kama mwananchi wa kawaida ambaye ninahitaji kuyafurahia haya maisha kama wananchi wengine.
 
“Dany”
“Mmmmm”
“Nipo tayari kuhakikisha kwamba unakuwa mtu yoyote. Nimeumbwa kwa ajili yako, nipo kwa ajili ya kukusaidia, hukustahili kupitia magumu yote hayo ambayo umeyapitia. Bado kijana mdogo, laiti leo hii usinge kuwa umepitia matatizo hayo uliyo nieleza, ninaamini leo hii ungekuwa mbali sana”
“Yaa”
“Sasa unataka kuwa nani?”
“Gaidi, gaidi kama wanaye msema wao”
“Hata mimi nipo tayari kwa hilo”
“Real”
 
“Ndio Dany”
Tukajikuta tukikumbatiana kwa nguvu huku kila mmoja akilia kwa uchungu, ninamshukuru Mungu kwa kunipatia Cajoli, japo nimepitia mambo mengi, ila Cajoli amekuwa ni msichana anaye jitoa maisha yake kwangu mimi, japo wapo wengi ambao walijitoa maisha yao kwa ajili yangu ila kila mmoja alikuwa na malengo yake kwenye haya maisha.
“Nakupenda sana Dany”
“Ninakupenda pia honey”
Taratibu tukajiuta tukianza kunyonyana midomo yetu, hisia za mapenzi zikaitawala miili yetu. Tukaanza kupeana raha ambayo inastahili kwenye mahusiano yetu, baada ya kuhakikisha kwamba tumeridhika na kila mmoja amepata haki kwa mwenzake, tukaingia bafuni na kuoga.
“Nahitaji umpigie shem Cajoli”   
“Nimueleze nini?”
 
“Nahitaji kuitingisha serikali kwa huu mpango ninao uhitaji kuufanya. Nahitaji viongozi wote walio ingia madarakani kwa njia za short cut, nilazima watoke”
“Sawa”
Cajoli akachukua simu yake na  kumpigia Cajoli.
“Unaweza kuja kwangu”
“Nakuomba ufanye hivyo”
“Poa best”
Cajoli akakata simu na kurudi kitandani nilipo kaa.
“Anakuja ndani ya dakika kumi atakuwa hapa”
“Yupo hapa hapa town?”
“Sijamuuliza, ila huwa Cajol akisema dakika kumi, basi ni kumi kweli”
“Unaweza ukaniletea zile nguo nyeusi nilizo zichukua kwa Cajoli”
“Yaa zipo humu kabatini”
 
Cajol akanitolea nguo hizo ambazo zipo kwa ajili ya mapambano tu. Nikazivaa, na kujitazama kwenye kioo vizuri.
“Hapa kazi inakwenda kuanza leo hii”
Ndani ya dakika kumi, Cajoli akafika nyumbani kwetu.
“Shem wewe ndio umesababisha varangati lile?”
“Yaani wee acha tu”
“Mmmm ni shida aiseee kumbe una mtiti yaani huko njiani magari full kukaguliwa. Tanga sijawahi kuona foleni ila leo foleni ipo”
“Watanisaka sana, ila nahitaji kuwakomesha kwa aina nyingine”
“Kiaina gani”
“Nahitaji kutega bomu la nyuklia na ninahitaji raisi atoke madarakani”
Cajoli wote wakaka kimya huku kila mmoja akitafakari ni nini cha kunishauri kwa maana swala la bumu tena la nyuklia ni swala jengine sana kwenye maisha haya ya Watanzania.
“Dany”
 
“Ndio shem”
“Unajua uzito wa bomu la nyuklia?”
“Ndio ninafahamu”
“Unajua madhara yake yanakuwaje?”
“Cajoli hadi kuzungumza hivyo ujue ninatambua kila kitu. Mimi nilikuwa ni agent wa NSS, hao unao waona sasa hivi barabarani wakinitafuta, mimi nilikuwa ni miongoni mwao”
“Dany mume wangu, ila hili swala tulitazame kwa jicho jengine, kuna mamilioni ya watu ambao hawana hatia kwenye kisasi chako, sasa kwa nini unataka hao nao wahusike kwenye vifo vya bomu hilo”
“Hamjanielewa maana yangu. Nilikuwa nina maanisha kwamba kwa kutumia bomu hilo nitaji raisi kuweza kuachia madaraka”
 
“Asipo achia na bomu unalo inakuwaje hapo shem?”
“Nina lilipua”
Taratibu nikamuona Cajoli akikaa kwenye sofa huku akionekana kuchoka, ninahisi moyoni mwake anajutia sana kuwa katika mahusiano na mimi.
“Shem”
“Naam”
“Hili swala ni kubwa sana, ninakuomba tufikirie mbinu nyingine”
“Munahitaji kunisaidia au laa?”
Nilizungumza kwa ukali hadi wote wakastuka.
“Tupo tayari kukusaidia”
“Shukrani shem, kuanzia sasa sihitaji muwasiliane na watu wengine zaidi yangu mimi”
“Sawa”
“Natambua NSS akili zao, kwa sasa wananitafuta kwenye barabara, viwanja vya ndege, baharini. Huku kwenye majumba hawatoweza  kunitafuta. Kama itawezekana nalihitaji lile bomu”
 
“Dany kusema kweli bomu kulileta  mjini hapa kwa njia ya gari ni ngumu sana. Labda cha kukushauri hapa twende Kange kule tunaweza kupanga kila kitu”
“Wazo zuri, honey nikuombe kitu?”
“Ndio”
“Nakupenda sana mke wangu, ninakuomba hili swala niweze kulifanya mimi na shem”
“Cajoli ni mtu muhimu kwetu ana uwezo mkubwa sana katika maswala ya computer na ugunduzi. Best au bado hukumueleza mumeo juu ya kipaji chako”
“Nilihitaji kumfanyia suprize, ili nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda vizuri”
 
“Basi nyinyi mutakwenda pamoja mimi nitajua wapi kwa kupitia”
“Sawa, ila itahitajika pikipiki kuhakikisha kwamba unafika kwa wakati”
“Pikipiki itapatikana wapi?”
“Ngoja niwasiliane na Hassani”
Shem Cajoli alizungumza, sikutaka kumzuia kwa maana ili niweze kufika kange kwa nja rahisi ni kuhakikisha kwamba ninapata pikipiki.
“Niletee pikipiki hapa kwa wajina”   
“Nahitaji mpya yenye uwezo mkubwa. Iwe full tank”
“Acha kunihoji mswali mengi wakati maelekozo nimekupatia”
Cajoli akakata simu na kututazama.
“Pikipiki italetwa baada ya muda mchache kuanzia sasa”
“Sawa, jiandaeni kwenda Kange. Hivi sasa ni saa mbili kasoro usiku”
 
Cajoli na mwenzake hawakupinga chochote, wakaanza kujianda. Haukupita muda mwingi Hassani akaleta pikipiki aina ya boksa, akamkabidhi shem Cajoli, kisha jamaa akaondoka pasipo kielewa kitu kinacho endelea.
“Mlinzi weko hivi anatambua uwepo wangu?”
“Sidhani honey”
“Kwa shem, mlizi hakuwahi kukuona?”
“Nikirudi nipo ndani ya gari, nikishuka ninaingia ndani. Hajawahi kuniona kabisa”
“Ngoja nimpe likizo”   
Cajoli akatoka na kuniacha na shemeji. Kwa kupitia dirishani nikamuona akizungumza na mlinzi. Kisha akarudi ndani, akachukua kiasi cha pesa na kwenda kumkabidhi mlinzi huyu ambaye hakuonekana kurishishwa na maamuzi haya ya muda mfupi.
 
“Sisi utatukuta Kange”   
“Sawa kuweni makini”
“Poa”
Cajoli na rafiki yake wakaondoka hapa nyumbani huku kila mtu akitumia gari lake. Nikakaa kwenye sofa huku nikisubiria masaa yazidi kusonga mbele ili hata nikuondoka basi asinione mtu yoyote. Nikawasha tv na kukuta habari yangu ikiwa ndio inatawala kwa wakati huu. Picha zangu zinarushwa kwenye kila kituo cha televishion huku mtu ambaye atafanikisha kukamatwa kwangu atazawadia shilingi bilioni moja ya Kitanzania.
 
“Wenda wazimu nyinyi”
Nilijikuta nikizungumza huku nikielekea ndani ya chumba chenye begi lenye silaha. Nikachukua begi na kurudi nalo sebleni. Nikaanza kukiko bastola moja baada ya nyingine huku nikizichomeka sehemu mbali mbali katika mwili wangu, nikianzia kiunoni hadi miguuni, na uzuri wa suruali niliyo ivaa ina sehemu nyingi ya kufichia silaha.
 
Ilipo timu saa tano kamili usiku nikatoka nje na begi langu. Nikaliweka kwenye pikipiki vizuri. Nikaufunga mlango wa kuingilia ndani kwa Cajoli kisha funguo nikaificha kwenye kopo la maua lililopo karibu na mlango. Nikapanda pikipiki, taratibu nikatoka getini huku nikiwa nimevaa kofia maalumu la pikipiki, kwenye viganja nimevaa glovos ngumu na zenye rangi nyeusi kuhakikisha kwamba mikono haitelezi. Safari yangu nikainza huku nikiwa makini sana kila ninapo pita. Nikiwa katika maeno ya msikiti wa Madina, gari mbili za polisi nikaziona zikija nyuma yangu kwa kasi huku zikiwasha ving’ora, jambo lililo nifanya nizidi kuongenza mwendo kasi wa piki piki yangu aina ya Boxer, ambazo husifika kwa mwendo kasi barabarani.
                                                                           
AISIIIII……….U KILL ME 103                                                                                               

Kadri nilivyo zidi kwenda kasi ndivyo jinsi nilivyozidi kuwaacha askari hawa umbali mkubwa na wala sifahamu kama wananifwata mimi au laa. Nikapita barabara za mkato hadi nikafanikiwa kufika nyumbani kwa Cajoli.
“Vipi hawajakustukia?”
“Hapana, japo kuna gari mbili za polisi zilikuwa zikinifukuzia, ila sijajua kama ni mimi ndio waliokuwa wakinifukuzia au mtu mwengine”
“Karibu tena nyumbani kwangu”
“Usijali”
Shem Cajoli akachukua pikipiki yangu na kuiweka kwenye moja ya chumba, cha nje kisha tukaingia ndani pamoja.
“Wife yupo wapi?”
“Yupo huku chini”
 
Tukashuka kwenye ngazi za kuelekea katika chumba ambacho kipo chini ya ardhi. Nikamkuta Cajoli akimunya minya batani ya computer iliyomo humu chumbani.
“Karibu honey”
“Asante”
Nilimjibu huku nikimbusu shavuni mwake.
“Ndio tunaanza kazi hapa na nimepata wazo jipya ambalo tulilizungumza na wajina hapa, tukaona ni vyema kukushirikisha”
“Ehee ninawasikiliza makamanda wangu”
Nilizungumza huku nivuta kiti kilichopo pembeni na mpenzi wangu Cajoli.
“Dany hii tunayo kwenda kuifanya ni biashara, ambayo kwanza italitingisha taifa, pili tutahakikisha kwamba tunaingiza pesa nyingi sana. Unatambua kwamba ukiwa na pesa unaweza kufanya kila kitu hata kumtoa raisi madarakani inawezekana kwa kutumia pesa”
“Eheee niambie mama maana ninaona hilo unalo kwenda kulizungumza lina udabwidambwi ndani yake”
“Hahaa shem kumbe una maneno ya Kiswahili namna hiyo”
“Kawaida tu shemeji yangu. Baby endelea”
 
“Hapa nipo katika hatua ya kutengeneza virus, ambavyo tutaviweka kwenye maji ambayo watu wakinywa. Hawato kufa ila wataugua ugonjwa wa kutoka mapunye mwili mzima”
“Mapunye!!?”
“Yaa mapunye haya yatawatoka mwili mzima. Na yatapelekea mtu kuoza mwili wake. Ila sisi tunaweza kutengeneza dawa, itakayo waponya mapunye hayo. Kwa njia hiyo tutaingiza bilioni of shillings”
Cajoli alizungumza kwa kujiamini sana.
“Shem hilo wazo ni zuri sana. Kutokana wewe unapambana na watu ambao wapo serikalini na unataka kuwaangusha kirahisi, hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi sana. Hapa cha kutumia ni akili, maarifa na utalipiza kisasi chako taratibu na ninakuhakikishia kwamba utajikuta ukifika mbali sana”
Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari mpango mpya ambao wasichana hawa wameuweka mezani.
“Hao virus watakuwa kwa njia ya maji maji au?”
 
“Yaa watakuwepo kwenye maji machache tu. Na kwadakika moja virus hao ninao watengeneza watakuwa wakiongezeka kwa zaidi ya virusi milioni mia moja. Sasa piga picha lisaa moja lina lina dakika ngapi, siku moja nayo ina dakika ngapi. Ni watanzania wangapi kwa siku wanakunywa maji?”
“Ni wengi, sasa kwa mfano wale wanao chemsha maji inakuwaje kwao?”
“Honey hawa virusi ninao watengeneza hata akichemshwa, awekewe sijui water gurd hafi yaani hii ni taaluma ambayo ninayo mimi mwenyewe duniani kwa kutengeneza hawa virusi, mtu mwengine ni mama yangu ambaye kwa sasa ni marehemu”
 
“Hao virusi katika maji wanaweza kuishi kwa kipindi gani?”
“Zaidi ya mwaka mmoja na nusu”
“Waoooo”
Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria wazo kama hili. Japo ni watanza wengi ndio wanakwenda kuathirika na huu ugonjwa, ambao hakuna mtu atakaye kufa, basi kwangu ni furaha kwani kisasi changu kinakwenda kukamilika taratibu taratibu
“Na mtu atakapo kunywa maji ni baada ya muda gani anaweza kuathirika”
“Lisaa, ninataka wachukue lisaa kuutawala mwili wa binadamu, ili isije kugundulika mapema kwamba tatizo kubwa lipo kwenye maji”
“Hapo safi, na utachukua muda gani hadi kukamilisha kuwatengeneza”
“Nina dakika kumi na tano mbele, nikisha watengeneza kuna kemikali nitazichanya baada ya hapo virusi watakuwa tayari kuanza kazi”
 
“Shemeji mke wako yupo vizuri, nikuibie siri?”
“Niibie tu”
“Yeye ndio aliye tengeneza hili bomu la nyuklia”
“Weeee!!”
“Ohoo nakuambia hapo mukipata mtoto basi atakuwa genius”
Kwa furaha nikajikuta nikimkumbatia Cajoli wangu.
“Hii kazi ikikamilika, ninawahakikishia mutaishi maisha ya furaha na yakijiri”
“Mungu abariki katika hili”
“Samahani injinia, sasa hivi mke wangu nitakuwa ninakuita injinia”
“Bila sahamani mume wangu”
“Hao virusi tukiwaweka kwenye maji, watasambaa kwenye maji Tanzanzima kwa kasi ya kiasi gani?”
“Yaani hawa virusi tukiwamwaga, kwa mfano kwenye chanzo cha maji ya dawasko hapa Tanga watasambaa kwa kasi ya yaa naweza kufananisha na kasi ya nini?”
“Ferrari?”
 
“Aghaa hilo ni gari mume wangu, ninaweza kuchukulia kasi ya sauti au hewa”
“Duu ni kasi kibwa sana”
“Yaa nahitaji hadi asubuhi kuna pambazuka tuna amka na habari hii”
“Kazi nzuri mke wangu, ngoja tusikuchanganye tukuachie nafasi ya kufanya kazi”
“Ahaa munaweza kubaki humu humu tu, mukaangalia jinsi ninavyo waunda”
Ikatubidi mimi na shem Cajoli tubaki kuwa watazamaji wa kitu anacho kifanya Cajoli kwenye hii computer, jambo ambalo kusema kweli hadi sasa hivi sielewi kitu ambacho anakifanya kwa maana sisi wawili hatuna utaalamu wa mambohayo. Baada ya dakika kumi na tano, akatugeukia na kututazama.
 
“Virusi wetu wapo tayari, hapa kazi iliyo baki ni kuanza kuinda hiyo fumula niliyo iweka kwenye computer”
“Hapo kumbe ulikuwa una unda fumula?”
“Yaa, baada ya hapo ninachukua kemikali ambazo zinahitaji, kirusi chetu tunamuunda ndani ya dakika mbili atakuwa hai”
“Sawa”
“Wajina naomba zile kemikali nilizo undia bomu la nyuklia”
“Poa”
Shem Cajoli akatembea hadi kwenye moja ya ukuta katika hichi chumba. Kuna kijimlango cha chumba, akaingiza namba za siri kisha akakifungua. Akatoa chupa kadhaa alizo zishika kwa umakini, Cajoli akachukua glove pamoja na miwani kubwa, akazivaa na kuisogelea meza ambayo shem Cajoli ameweka chupa hizi za kemikali. Cajoli akawasha taa kubwa iliyopo kwenye meza yenye kemikali
 
“Nawaomba mukae mbali kidogo, kwa maana hizi kemikali sio nzuri pake zitakapo mdondokea mtu”
“Sawa injinia”
Tukasimama umbali kidogo kutoka katika sehemu alipo Camila, akaanza kuchanganya changanya kemikali zake haraka haraka. Alipo hakikisha zimekamilika akachukua kibakuli alicho changanyia kemikali hizo na kukiweka kwenye darubini(Microscope) na kuanza kupima.
“Njooni muone”       
Cajoli alizungumza huku akitabasamu sana. Tukakimbilia hadi sehemu alipo, akaanza kuchungulia shem Cajoli, kisha akanipisha mimi kuchungulia kitu anacho kiona kwenye hii darubini ya kidaktari.
 
Kitu ninacho kiona ni vijidudu dudu, vidogo sana na kila baada ya dakika moja vinaongezeka.
“Hivi ndio virusi?”
“Yaa hivyo ndio virusi ambavyo nilikuwa nikiviunda, hapo ni lazima watu wataisoma namba”
“Kazi nzuri mke wangu, sasa si tuanze na majaribio kwanza?”
“Hakuna haja ya majaribio shem, hapa tunalibwaga bomu, alafu tukaa pembeni kusikilizia majibu”
“Ila watu si hawato  kufa mke wangu?”
“Nakuhakikishia mume wangu hakuna mtu ambaye  atakufa kwa maana hichi tunacho kifanya, ni kuiforce serikali hii ambayo leo hii wewe inakuita gaidi ila kesho au kesho kutwa watakuita daktari”
“Kama ni hivyo ninakuomba virusi hawa tuanze kuwaachia kuanzi sasa”
“Itabidi hapa tugawane kazi, vyanzo vyote vya maji yanayo tumiwa kwa watanzania tumwage hawa virusi”
“Ila nimepata wazo jengine?”
“Wazo gani?”
 
“Tukisema tutumie njia ya kupeleka kwenye vyanzo vya maji, inaweza kuwa ngumu sana. Nilicho fikiria kwamba hao virusi niwabadilishe kuwa katika hali ya hewa, nikiwaachia hewani. Wakimbilie sehemu yoyote ya maji ambayo hayajafunikwa”
“Inawezekana kubadilishwa?”
“Ndio inawezekana”
“Basi tufaje hivyo”
“Ila itachukua lisaa kufanya hivyo”
“Hakuna tabu mke wangu”
Cajoli kwa haraka akavuta kiti alicho kuwa amekalia. Akaanza kuminya minya batani za computer akatengeneza alicho kitengeneza kisha akarudi kwenye meza ya kemikali. Tukaa umbali kidogo, alipo hakikisha amemaliza kutengenza virusi hawa wawe kwenye njia ya hewa, akachukua kichupa kidogo na kuweka maji maji hayo kisha akakifunga.
“Hichi kichupa, wajina nitahitaji ukiweke juu ya nyumba yako ukifungue, maji maji hayo yatapungua kadri jinsi virusi watakavyokuwa akisafiri kwa hewa”
“Sawa, sasa na sisi maji ya humu ndani?”
“Tuanzeni kufunika, tuhakikishe kwamba maji tunayo kunywa yawe katika usalama”
“Unaonaje ukatengeneza kinga yake”
“Ni rahisi kuitengeneza na tutakuwa tunaitumia sisi wenyewe.”
“Sawa, shem twende ukanisaidie”
“Twendeni wote”
Tukatoka katika chumba hichi kilichopo chini ya ardhi. Tukaanza kazi ya kufunika vyombo vyote vyenye maji. Tulipo hakikisha kwamba tumemaliza. Tukatoka nje, Cajol akanipa kichupa hicho, tukaweka ngazi sehemu ambayo ninaweza kupanda kwenda juu kirahisi. Kazi ya kupanda juu haikuniwia ugumu kabisa. 
 
‘Mungu tusamehe katika hili’
Nilizungumza huku taratibu nikifungua kichupa hichi. Nikaanza kushuhudi jinsi kinavyo pungua maji yake taratibu. Nikashuka na kuwakuta Cajoli wakinisubiri,
“Kinapungua kweli aisee”       
“Yaa hiyo itakuwa ni kazi, hapa virusi hao wanakimbilia sehemu yenye maji. Na hewa hii itasambaa  nzima”
“Vipi kwa wale wa Kenya, kwa maana hii hewa haina mipaka?”
Ukimya ukatawala kati yetu huku kila mmoja akifikiria jambo hilo.
“Ngoja tuangalie itakuwaje, ikionekana vipi nao wacha waje tu. Ni moja ya biashara, unacho kihitaji wewe Dany ni pesa na nguvu”
Cajoli alizungumza kwa kujiamini na kuzidi kunifanya nijione mshindi katika kisasi changu ambacho kwa sasa sihitaji kutumia nguvu sana kulipiza, ila ninatumia akili kuhakikisha maadui zangu wanaisoma namba.

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )