Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 19, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 110 na 111 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

Kwa haraka nikaufungua mlango na kukuta Beatrice akiwa amesimama na watu wake
“Haraka anda timu itakayo kwenda post, kuangalia ni gorofa gani lililo tegwa bomu”
“Sawa dokta”
Nikarufi katika chumba alipo Hassan Abdlah, nikamkazia macho kwa haraka nikamfwata hadi sehemu alipo kaa, nikamnyanyua na kumuangusha chini kwa nguvu.
“Ni wapi alipo Cajoli mke wangu la sivyo risasi zote hizi zitaishia kichwani mwako”
“Ca…..ca….caj…oli ni master plan”
“Master Plan una maana gani?”
“Cajoli mke wako ndio aliye panga haya yote”
Masikio yangu nikahisi yananiwasha kwa hichi nilicho kisikia kwa maana Cajoli ninaye mfahamu mimi sioamini kama ni mwanamke mwengine msaliti kwenye maisha yangu.
           
ENDELEA       
Sikutaka kumuamini Hassani moja kwa moja katika mambo aliyo yaseme, pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote. Nikamminya kidonda chake nilicho mpiga risasi na kumfanya atoe ukelele.
“Cajoli katika hili anausika vipi?”   
Nilimuuliza kwa hali ya ukali sana huku nikiendelea kukiminya kidonda chake kwa nguvu sana.
“Sifahamu ila mi nilisikia tu wezangu wakizungumza”
“Kwa sasa amefichwa wapi?”
“Eheee”
 
Nikaona hanielewi, nikamtandika risasi nyingine ya paja na kumfanya azidi kulia kwa maumivu makali sana.
“Nimekuuliza ni wapi alipo Cajoli”   
“Yu…yupo kwenye mapango ya Amboni Tanga”
“Ndipo sehemu alipo shikiliwa?”
“Ndipo kundi zima lilipo jificha na hata bomu la nyuklia linaogozewa huko”
Nikamuacha Hassan na kutoka nje ya chumba hichi.
“Hassan amesemaje?”   
Beatrice aliniuliza huku akinitazama machoni.
“Sehemu walipo jificha magaidi ni katika Mapango ya ambani. Na sehemu hiyo ndipo wanapo ogoza mpango mzima wa kulipua bomu lilipo hapa Dar es Salaam”
“Inabidi kuandaa timu kwenda huko?””
 
“Niandalie helcopter, pamoja na vijana wawili unao waamini kama wanaweza kuifanya hii kazi vizuri”
“Kabla ya kufanya hivyo nilazima uzungumze na raisi”
“Sawa”
Nikaingia kwenye moja ya ofisi ambayo kuna tv kubwa inayo tumika kuwasiliana na raisi. Beatrice akaka kiti cha pembeni yangu huku sote tukiitazama Tv hii yenye nembo ya raisi. Baada ya sekunde kadhaa tukaunganishwa na raisi aliyopo katika chumba kingine na wakuu wa jeshi.
“Muheshimiwa raisi, dokta Lameck ameweza kutusaidia kuweza kufahamu ni wapi magaidi ni wapi walipo jificha kwa kumuhoji gaidi tuliye mkamata”
 
“Kazi nzuri sana dokta Lameck, ni sehemu gani ambayo wamejicha hao magaidi”
“Muheshima raisi, magaidi hao wamejificha katika mapango ya Amboni, na hapo ndipo wanapo fanya shuhuli zao za kuongoza bomu hili la nyuklia ambalo wamesema kwamba ifikapo saa kumi na mbili asubuhi linalipuka na sio saa sita mchana”
Nilizungumza na raisi huku nikimtazama kwenye Tv hii.
“Mungu wangu, na sasa hivi ni saa hivi umebaki muda mchache sana”
“Ndio muheshimiwa kikubwa ni kwenda kuhakikisha kwamba tunazuia ulipukaji wa bomu hili.”
“Na lipo sehemu gani?”
“Lipo katika gorofa refu maeneo ya Posta, sasa kazi ni kuhakikisha kwamba bomu hilo linaweza kuteguliwa mapema iwezekanavyo. Tuna dakika arobaini hadi sasa muheshimiwa raisi”
 
“Dokta Lameck unahitaji nini?”
“Ninahitaji  helcopter, pamoja na vijana wawili kwenda kuianza hii oparesheni, pili nitahitaji timu  nyingie kuja nyuma yangu. Hawa ni magaidi kwa hiyo siweze kujua wana mbinu gani nyingine ambazo wanaweza kuzifanya”
“Umepata”
“Beatrice andaa vijana wako, na kila hitaji analo litaka dokta Lameck, na kuwa karibu yake kwa kuwasiliana naye”
“Sawa muheshimiwa raisi”
“Dokta Lameck, nimekuamini na Mungu akubariki kwa kule unapo elekea kuifanya kazi hii”
“Asante muheshimiwa raisi”
Tukatoka katika chumba hichi na Beatrice, akanikabidhi simu pamoja na miwani maalumu ambayo inasaidia mtu kuweza kuona kwenye giza kali.
 
“Naamini unaweza kutumia hiyo miwani?”   
“Nafahamu, ninahitaji magazine nyingine za kutosha. Hakikisha timu yako itakayo kuja nyuma yangu, inawasiliana nami kwa ukaribu zaidi”
“Sawa dokta Lameck. Vijana ni hawa hapa. Agent Moris na Agent Emily”
“Habari zetu”
“Salama dokta”
“Naamini mumeshapewa maelezo ya awali kuhusiana na tukio zima jinsi linavyo endelea?”
“Ndio dokta na helcopter ipo tayari”
“Dokta Lameck magazine za bastola zako hizi hapa”
Agent Beatrice akanikabidhi kijibegi kidogo nikafungua ndani nikakuta magazine za kutosha pamoja na saa ya mkononi.
“Safari njema dokta”  
  
“Shukrani”
Tukatoka nje ya jengo hili na kuingia ndani ya helcopter. Taratibu helcopter ikaanza kuacha ardhi na kueleea hewani. Yote haya ninayafanya kwa ajili ya mke wangu na si kwajili ya nchi yangu.
“Dokta Lameck hii hiki ni kifaa maalumu chenye ramani ya pango zima la Amboni, tunaweza kufahamu ni wapi magaidi  walipo jificha”
Agent Moris akanikabidhi kifaa kidogo kilicho kaa kama simu aina za smartphone ila si simu. Nikaanza kuipitia ramani ya pango zima la Amboni.
“Shukrani”   
Nilimjibu Agent Morsi huku nikiweka kifaa hichi mfukoni mwa suruali yangu.
“Inatubidi kushuka umbali kidogo kutokea sehemu yalipo mapango”
 
“Ndio dokta hilo linaelekeweka”
“Sawa”
Hatukuchukua dakika nyingi, tukawa tumekaribia kwenye eneo la karibu kabisa na mapango ya Amboni, helicopter taratibu ikashuka chini, mimi na wezangu wawili tukashuka na helicopter ikaondoka eneo hili.
“Tuna dakika kumi za kuhakikisha kwamba oparesheni hii inakwisha”
“Dokta dakika kumi ni chache”
“Hata dakika moja pia ni nyingi, mimi ndio kiongozi wa hii oparesheni munatakiwa kufwata amri yangu”
Nilizungumza kwa kujiamini sana huku nkiwatazama vijana hawa machoni mwao. Wakakubaliana nami japo wanaonekena wana maswali mengi sana vichwani mwao kuhusiana na mimi kwa maana dokta na kazi ya kutafuta magaidi ni vitu viwili tofauti.
 
“Kutoka hapa hadi kwenye mapango ni mwendo wa dakika mbili kwa hatua za haraka”
“Sawa doka”
Nikachomoa bastola yangu moja kwenye kiuno changu sehemu nilipo kuwa nimeichomeka. Kwa haraka nikaanza kutembea kuelekea yalipo mapango. Vijana hawa wawili wa NSS, wakaanza kunifwata kwa nyuma, sikutaka kuonyesha udhaifu kwamba mimi ni daktari ila kitu ninacho kifanya hapa ni ukomandoo ambao nimejifunza shemeu mbali mbali kutokana na maisha yangu kubadilika kwa asilimia kubwa sana.
 
Tukafika kwenye mapango ya amboni, kila mmoja akavaa miwani yake inayo msaidia kuona kwenye giza totoro. Taratibu tukaanza kuingia ndani huku kila mmoja silaha yake akiwa ameishika mkononi mwake. Kuseme kweli haya ni mapango ambayo yanatisha sana, mapango ambayo yana historia kubwa sana kwenye nchi ya Tanzania. Takribani dakika tano zikakatika tukiwa tunatazama ni sehemu gani ambayo tunaweza kuwaona magaidi.
“Dokta au jamaa ametudanganya?”
“Hapana tuzidi kusonga mbele”
“Ila dokta kardi jinsi tunavyo zidi kwenda ndivyo jinsi tunavyo zidi kupotea sisi wenyewe”
 
“Nimewaambia kwamba ninahitaji tusonge mbele, kama mtu huitaji kuwa pomoja nami unaweza kurudi nyuma”
Agent Emily akatulia kwa muda huku akitafakari nini cha kuzungumza, akatingisha kichwa na kukubaliana kuendelea na mimi, ila Agent Moris anaonekana kuwa wasiwasi mwingi.
“Nisikilize agent Moris, hii ni oparesheni ya kwenda kuokoa maisha ya mamilioni ya Watanzania watakao kufa pasipo hatia ya aina yoyote. Huko tulipo toka kuna watoto, wake, wajane na watu wa kila aina. Ukishindwa kuyaokoa maisha yao leo basi wewe hii kazi huiwezi”
Nilizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa ushawishi mkubwa sana kwa agent Moris. Akanitazama kisha akatingisha kichwa cha kukataa kuendelea na safari hii ya kutafuta magaidi. Taratibu akaanza kurudi nyuma na kuanza kuondoka katika eneo hili la mapango.
“Agent Emily tunaweza kuendelea na safari?”
“Ndio dokta”
 
Tukaendelea na utafutaji wetu wa kukatiza kila eneo la haya mapango huku tukiongozwa na ramani iliyopo kwenye hichi kifaa maalumu. Tukaanza kusikia milio ya vyuma kama vinavyo gongwa gongwa.
“Dokta umesikia hivyo?”   
“Yeaa”
“Sauti zinasikika kutoka upande huu wa mashariki”
“Twende”
Taratibu tukaanza kutembea kwa taadhari, kadri jinsi tunavyo zidi kwenda mbele ndivyo jisni tulivyo zidi kusikia milio  ya vyuma hivyo jinsi vinavyo gongwa. Sasa tukaanza kuuona mwanga ukitokea kwenye moja ya njia. Tukazidi kusonga mbele kuufwata mwanga huu, hadi tukafanikiwa kufika katika njia hii nyembamba sana, ambayo inaruhusu mtu mmoja mmoja kupita.
 
“Upo tayari?”
“Ndio dokta”
“Twende”
Tukaanza kujipenyeza katika hii njia, na tukatokea katika sehemu ambayo sote mimi na agent Emily tukabaki tunashangaa. Sehemu hii imekaa kama ukumbi, na imefungwa taa kubwa katika kila ukuta ambazo zinamulika na eneo zima linaonekana vizuri. Kwenye kumbi huu kuna magaidi si chini ya hamsini, huku mabomu mawili makubwa ya nyuklia yakiwa yemeandaliwa vizuri sana.
“Naomba darubini”  
  
Agent Emily akanipatia darubini, uzuri wa sehemu tuliyopo ni juu kabisa na watu wote tunawaona kwa chini. Taratibu nikaanza kutazama mtu mmoja baada ya mwengine, nikamuona mke wangu Cajoli akiwa amesimamiwa na vijana wawili walio mshikia bunduki huku akiamrishwa kutengeneza bomu la nyuklia.
“Ohoo Mungu wangu”
“Nini dokta?”
“Yule pale ni mke wangu”
“Hembu”
Agent Emily akachukua darubini na kuangalia eneo alipo Cajoli, akatazama na maeneo mengi.
“Tunafanyaje hapa dokta?”
“Tutanakiwa kuvamia hili eneo kwa umakini sana, ila tukikosea tu basi mke wangu tutampoteza”
“Sawa dokta, inabidi tutafute njia ambayo tunaweza kupita”
“Hakuna tabu”
 
Hata kabla hatujatoka katika hili eneo tukastukia tukimulikwa na taa kubwa, tukataka kukimbia ila watu zaidi ya nane wakawa wametuzunguka wakiwa na bunduki zao.
“Wekeni silaha zenu chini”   
Mtu mmoja alizungumza huku akwia amejifunga kilemba kichwani mwake. Hatukuwa na ubishi wowote zaidi ya kuweka silaha zetu chini. Magaidi wawili wakatufwata na kutufunga mbingu huku mikono ikiwa nyuma. Wakaanza kutuongoza kushuka chini kwenye ukumbi huu, Cajoli alipo niona akataka kunikimbilia ila akauziwa kwa kunyooshewa bunduki, machozi mengi yakanedeleka kumwagika Cajoli. Kwa nguvu tukapigiswa magoti chini huku tukizungukwa na magaidi hawa ambao sasa nimewatambua kwamba wanatokea katika kundi la Al-Shabab.
 
“Mkuu tumempata dokta Lameck”   
Gaidi mmoja alizungumza kiarabu, kwa simu yake ya upepo. Haukupita muda sana nikamuona Yudia akiwa ameongozana na Dany feki wakitufwata sehemu tulipo. Hasira ikaanza kunipanda kwa maana Yudia ni adui yangu wa muda mrefu  sana.
“Ohoo Dany, ni muda mrefu sana sijakuona”
Yudia alizungumza huku akinishika kidevu changu, akanigeuza kichwa changu kushota na kulia, akamtazama Cajoli kwa jicho la dharau kisha akanipiga busu la mdomoni, japo nimejitahidi kulikwepa ila akanilazimisha, jambo lililo mfanya Cajoli kuzidi kulia kwa hasira.
 
“Dany pole kwa msiba wa mama yako, mkeo, mdogo wako na mwanao. Iliwabidi wafe kutokana na kiherehere chao.”
Tukiwa katika eneo hili, nikamuona Agent Moris akija katika eneo hili akiwa ameshika begi kubwa mkononi mwake.
“Moris asante sana kwa kutuletea hawa watu, sasa munaweza kumsindikiza”
“Wewe malaya wa kiume kumbe msaliti”
Agent Emily alizungumza huku akihitaji kunyanyuka, ila kwa haraka Yudia akachomoa bastola yake kiunoni na kumpiga risasi mbili za kichwa agent Emily na huo ukawa mwisho wake jambo lililo nifanya nizidi kupandwa na hasira hadi machozi yakaanza kunilenga lenga.
 
AISIIIII……….U KILL ME 111

“Na wewe ukileta ujinga basi nitahakikisha kwamba unakufa”   
Yudia alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, akairudisha bastola yake sehemu alipo itoa, akawaamrisha watu wake kuninyanyua. Wakanipapasa na kuchukua silaha zangu, simu, miwani pamoja na jaketi la kuzuia risasi. Walicho nibakisha ni nguo zangu tu.
“Mpelekeni mukamfunge”       
“Sawa mkuu”
 
Jamaa hawa wakanikokota kokota huku nikimtazama Yudia pamoja na Dany huyu feki, ambaye moja kwa moja ninaamini kwamba ametengenezewa sura hii ya bandia ambayo inafanana na mimi. Nikaingizwa kwenye moja ya chumba chenye geti la chuma. Wasiwasi mkubwa kuhusiana na nchi yangu kuingia katika hali nguvu ya kivita ikaanza kunitawala moyoni mwangu.
‘Ni nini nitafanya?’   
Nilijiuliza huku nikitazama kila sehemu ya chumba hichi kilichomo ndani ya haya mapango. Kila kitu nilicho kuja nacho magaidi hawa wamekichukua na kuniacha nikiwa na nguo zangu nilizo zivaa tu. Nikajaribu kutingisha geti hili halitingishiki kabisa na nje limefungwa kwa kufuli kubwa. Nikaendelea kukaa katika chumba hichi kwa zadi ya nusu saa, geti likafunguliwa na wakaingia wawili wakaniamrisha kunyoosha mikono yangu mbele ili wanifunge pingu ili wanitoe katika hichi chumba. Sikuhitaji kukubaliana nao kabisa katika kusubiri nipate mateso ambayo kusema kweli sifahamu yanaweza kuwa ni mateso ya namna gani.
“Nyoosha mikono yako”   
     
Gaidi mmoja alizungumza kwa hasira huku akininyooshe bunduki yake aina ya Ak47. Taratibu nikanyoosha mikono yangu mbele, kitendo cha mwenzake kuishika mkono wangu wa kushoto ili aufunge pingu, ikawa ni kosa kubwa sana kwake, kwa maana hiyo ndio ikawa nafasi yangu ya pekee kummvuta kwa harake, nikampiga kigoti cha kifua, hata kabla mwenzek hajafyatua risasi, tayari nilisha jirusha hewani na kumtumia teke moja la mikono yake, lililo pelekea kushindwa kuihimili kuishia bunduki hiyo na kujikut ikianguka chini.
 
Sikutaka magaidi hawa wafanye lolote, sikuwa na huruma na gaidi hata mmoja, kazi yangu ni kuhakikisha kwamba ninazisitisha pumzi zao zote na kuwaangamiza kimya kimya pasipo mtu yoyo kuweza kusikia na ndivyo nilivyo hakikisha kwamba ninawaangamiza kwa kuwavunja shingo zao. Nikaokota bunduki ya mmoja wao, nikachomoa magazine na kukuta risasi za kutosha, nikairudisha nilipo ichomoa na kuikoki bunduki tayari kwa kushambulia. 
 
Nikachukua kisu cha gaidi mmoja na kuichomeka kwenye soksi, kisha taratbu nikaanza kutoka humu ndani huku nikiwa nimeishika bunduki hii ya aina ya MK47 yenye sifa nzuri katika maswala ya utoaji wa risasi.
Nikaanzisha oparesheni ya kuua gaidi mmoja baada ya mwengine kwa kuwavunja shingo zao pasipo wao kugundua ni jambao gani linalo endelea ndani ya mapango haya yakutisha, cha kushukuru Mungu kuna taa hizi zinamulika katika kila eneo hili walilo jificha magaidi.
“Hei”   
Gaidi mmoja alizunumza baada ya kuniona nikinyata karibu ya mwenzake, kwa haraka akafanyatua risasi ambayo kwa uharaka wangu, nililimvuta mwenzake na kumuweka kama ngao mbele yangu na kumfanya riasasi hiyo kumpiga yeye. Mlio huu wa risasi ya huyu gaidi ikawa imeharibi kula kitu kwa manaa tangu nianze kuwaua hadi sasa hakuna ambaye aliweza kustukia hali halisi inavyo endelea ndani ya mapango haya. Nikachomoa kisu nilicho kichomeka kwenye soksi, nikakirusha kwa kasi na kutua kifuani mwagaidi huuyu ananye nishambulia.
 
Mashambulizi yakaanza kutawala ndani ya haya mapango kati yangu mimi na hawa magaidi, sikuwa na mbinu nyingine yoyote zaidi ya kujitahidi na mimi kulinda mwili wangu. Ubaya ambao magaidi hawa wamekutana nao kutoka kwangu ni kwamba ninawajua hadi katika kambi yao na nimesha kuwa miongoni mwao na nimeshirikiana nao kwenye baadhi ya kazi ambazo bila wao kunijua waliweza kuniamini. 

Hata mbinu zao na ubora wao katika kutumia silaha huwa ninaujua, hawana muda wa kusubiri, kumuona adui ili wamvamie, wao wakijua tu kwamba mbele yao kuna adui basi wanajifyatulia risasi kama wenda wazimu, kitu ambacho katika mashambulizi ni kibaya sana.
 
Ili kuto kuharibu risasi zangu, sihitaji kushambulia pasipo kumuona adui, nikaanza kufwata mfumo ambao nilisha fundishwa na mwalimu wangu katika chuo cha NSS, alikuwa anatueleza kila siku kwamba ‘save your bullet, one bullet one person’
“Zima taa zima taa”   
Magaidi nilianza kusikia kelel hizo za magaidi, wakaanza kushambulia taa zinazo mulika katika eneo hili na kupeleka giza kali ndani ya mapango haya na hapa ndipo walipo niweza kwa maana sina uwezo wowote wa kuona katika giza totoro kutokana sina miwani maamulu ambazo zinatumiwa kauona kwenye giza.
 
“Narudia nahitaji nimpate akiwa hai, narudia tena ninahitaji nimpate akiwa hai”
Nilisikia sauti ya Yudia ikitoea katika kipaza sauti cha gaidi niliye muaa mita chache kutoka sehemu nilipo. Kwa hisia za kuifwata sehemu ilipo tokea, nikaanza kutembea huku nikimtafuta gadidi huyo, kwa bahati nzuri nikamgonga kwa mguu wa kushoto, kwa haraka nikachuchumaa na kuanza kumpapasa kuanzia chini kuelekea juu, kwa bahati nzuri nikafanikiwa kukipata kichwa chake, nikampapasa machoni mwake kwa maana ninakumbuka nilimuona akiwa amevaa miwani kabla ya kumuaa, nikaishika miwani yake na kumvua. Nikaivaa machoni mwangu, ika badala ya kuona mbele nikajikuta nikiona giza totoro.
“Fuc***”   
Nikaivua miwani hiyo na kuitupa chini kwa maana sio miwani za ‘night vision’. Ukimya ndani ya pango hili ukaendelea kutawala na fika ninafahamu kwamba wananiwinda mimi, kwa maana nimesha sikia ninahitajika niwe mzima. Gafla nikastukia kitu kizito kikitua kichwani mwangu na kujikuta nikianguka
chini na kupoteza fahamu.   
                                                                                                    ***
Kitu chenye arufu kali na ya kustua, kikapita kwenye pua zangu na kujikuta nikikurupuka huku nikiweweseka. Mwanga mkali wa taa unao nimulika usoni mwangu, ukanifanya nizidi kuweweseka.
“Sogeza taa pembeni”
Sauti ya Yudia kusema kweli ninaifahamu vizuri sana, ni sauti ambayo hata nikiwa usinigizi nikiisikia basi nilazima nitambue kwamba mzungumzaji ni Yudia.
 
“Dany nakujua vizuri, sana na nilitambua kwamba ni lazima utaniletea fujo kwenye ngome yangu, pasipo kujua kwamba kwa sasa Yudia yule si yule mfanyakazi wa ndani kwenu na wala si mfanyakazi chini ya mwanaharamu K2”
Yudia alizungumza huku akiwa amesimama mbele yangu. Kiti nilicho kalia nimefungwa kisawa sawa na wala sina uwezo kabisa wa kusimama wala kufanya kitu chochote na pembeni yangu wamesimama wanaume wanne wenye bunduki huku nyuso zao zikiwa zimefunikwa na mabushori yalio waacha macho tu.
“Nilipo pata habari kwamba umempata daktari ambaye alikuwa ni target yangu ili aniwezeshe kunipa nguvu, basi nikaseme hiyo ndio nafasi yangu kuweza kukukamata wewe.”
“Sielewei unazungumza nini?”
“Mleteni ndani”
 
Mke wangu Cajoli akaingizwa ndani ya chumba hichi akiwa ameshikwa na wanaume wawili, uso wake umajaa michirizi ya damu na inavyo onekana amepigwa sana. Wakampigisha magoti kwa nguvu hadi nikajikuta niking’ata meno yangu kwa hasira nikitamani utokee muujiza kamba za manila walizo nifunga zifunguke, nimkamate Yudia, nimkamue kama miwa inavyo kamuliwa kwenye mashine na kutoa juisi, ila ndio hivyo sina uwezo.   
 
“Huyu unaye muita mke wako ni daktari wa uvumbuzi wa mambo, hata hilo jina la dokta Lameck ulilo pewa halikustahili wewe kupewa yeye ndio dokta na yeye ndio niliye kuwa ninamuhitaji kabla ya kufahamu kwamba wewe una mahusiano naye.”
“Leo ndio siku ya ukweli wako wote kutoka nje, la sivyo nitakuua wewe. Washa kamera”
Yudia akaendelea kuwaamuru watu wake, tukatazamana na Cajoli, nikamuona jinsi machozi yake yanavyo endelea kumchuruzika kwenye mashavu yake. Kimoyo moyo nikajikuta nikijutia na kujiuliza ni kwa nini niliamua kuingia kwenye mapenzi na Cajoli na kumsababishia matatizo haya yote mtoto wa watu asiye na hatia.
 
    Yudia akaamuru kiti kilichopo nyuma yangu kusogezwa mbele yangu, kisha Cajoli akakalishwa kwa nguvu huku akiendelea kumwagikwa na machozi. Kamera ikageuzwa kwake, kisha Yudia akanisogelea huku akiwa ameshika bastola yake. Akaniwekea bastola ya kichwa huku akimtazama Cajoli usoni mwake.
“Yudia ni kitu gani unacho hitaji kukifanya?”
“Hayakuhusu”
“Nahitaji kufanya ni nani aliye nyuma ya ugonjwa wa mapunye ulio enea Tanzan kuanzia siku ya jana?”
Yudia alizungumza huku akiwa amemkazia macho Cajoli na bastola yake akiwa ameiweka karibu kabisa na kichwa changu.
 
“Cajoli usizungumze chochote please baby”
Gaidi moja likanipiga ngumi nzito ya kifua hadi nikajihisi kutapika damu jambo lililo mfanya Cajoli kuzidisha kilio.
“Nasema nasema”       
“Zungumza sasa la sivyo mpenzi wako atakufa”
“Mimi, mume wangu Dany ndio tulikuwa na wazo la kuhakikisha kwamba tunatengeneza virusi ambao watakwenda kuwashambulia watanza, ikiwa ni njia moja wapo ya sisi kulipiza kisasi kwa raisi K2”
‘Ohoo Mungu wangu Cajoli kwa nini umezungumza?’
Nilijikuta nikijilaumu moyoni mwangu huku nikimtazama Cajoli jinsi anavyo zugumza huku machozi yakimwahiga.
“Na baada ya hapo ikawaje?”
 
“Tulitengeneza ant biotic ya kua virusi hao kwa makubaliano ya kuingia mkataba na serikali  ili tuweze kujipatia kiwango kikubwa cha pesa”
“Na zoezi lenu lilikwenda salama?”
“Ndio”
“Pesa zipo wapi?”
Taratibu Cajoli akanitazama mimi huku akiwa amejawa huzuni nyingi usoni mwake. Gaidi akanipiga kofi zito la uso lililo nifanya nijisikie maruwe ruwe, Cajoli akazidi kulia jambo lililo zidi kuniumiza moyo wangu.
“Usipo zungumza mumeo ataendelea kuteseka hadi atakufa mbele ya macho yangu”
‘Noo Cajoli nooo’
 
Nilizungumza kwa kunyanyua lipsi zangu tu pasipo kutoa sauti huku nikimtazama Cajoli aliye kaa kimya akiendelea kulia. Gaidi akatoa kisu chenye ncha kali na kukisogeza karibu na jicho langu kwa ajili ya kulitoa jicho langu la upande wa kulia.
“Moja, mbili, t……”
Ikambidi Cajoli kukatisha hesabu ya Yudia kuokoa kiungo changu muhimu kwenye maisha yangu.
“Nazungumza nazungumza”
“Zungumz”
“Pesa ipo kwenye akaunti yangu”
“Ni kiasi gani?”
“Dola bilioni moja”
“Muongo”
 
Taratibu gaidi huyu wa kiume akaanza kunichana kwenye shavu langu la kulia, kitendo cha Cajoli kuona damu zikinichuruzika kwenye shavu langu akaropoka.
“Dola bilioni kumi”
“Waoo vizuri sana. Rudisha Camera huku”
Yudia alizungumza na kusogea pembeni akachukua busholi na kulivaa kichwani mwake kuificha sura yake. Akasimama nyuma yangu huku sote tukitazama kamera hii inayo endelea kurekodi kila kitu kinacho endelea katika eneo hili.
“Raisi K2, si kila kitu kwamba serikali yako inaweza kufanya. Huyu ni gaidi uliye kuwa unamtafuta tangu kipindi ambacho haujawa raisi hadi leo umeshikilia nchi.”
Gaidi mmoa akanisogelea akiwa ameshika kitambaa chenye harufu mulani ambayo sijaielewa ni harufu ya maji maji gani, akaanza kunisugua usoni mwangu na kutoa make up yote ambayo nilifanyiwa kitaalamu na shem Cajoli na nikabaki katika sura yangu halisi.
 
“Huyu ni Daniel, siku zote ulikuwa ukimtafuta kwa udi na uvumba. Wananchi, huyu ndio aliye wafanya muteseke kwa kutokwa mapunye miilini mwenu. Ni mtu hatari sana kwa amani ya nchi yenu, gaidi huyu aliweza kuingia hadi ndani ya ikulu ya raisi wenu kwa ujanja wa kujiita daktari, ila si daktari na nilimtengeneza gaidi anaye fanania na yeye ili kuzidi kumpa nafasi ya kuaminika ndani ya ofisi ya raisi. Na tumekipata kile ambacho tulikuwa tunakihitaji kukipata.”
Yudia alizungumza maneno ambayo tayari yamesha nipandikizia chuki kwa kila mwananchi ambaye anaitazama video hii ambayo nina amini kwamba inaruka moja kwa moja kwenye vituo vya televishion kwa maana magaidi hawa wa Al-Shabab wana ujuzi mkubwa sana wa kuingiza video zao kwenye vituo vya televishion pasipo wahusika wa vituo hivyo kukubaliana na hilo.
 
“Kabla sijasahau, muheshimiwa raisi maovu yako nayo yanakuja muda mchache kuanzia hivi sasa, na ninatambua kwamba bomu la nyuklia lililo kuwa limetegwa katika eneo la Posta wamefanikiwa kulitegua, ila waambie wananchi wajiandae kuomboleza vilio vya kusaga meno kwa maana hamto jua muda wala saa ambayo nitaachia bomu jingine”
Yudia akatoka nyuma yangu na kamera ikazimwa, akavua bushori alilo vaa na kusimama mbele yangu kuku akinitazama.
“Nchi nzima sasa watakuwa wamesha tambua mbaya wao ni nani”
“Yudia umekwenda mbali sana katika hili”
“Hahaa Dany, nimekusaidia. Nimekufanya uwe maarufu kuliko mtu yoyote ”
“Sawa ninakuomba umuachie mke wangu aondoke zake”
“Hahaa Dany unahisi ninaweza kufanya ujinga wa namna hiyo. Narudi kama nilivyo kuambia, mke ndio alikuwa chaguo langu, ila ulivyo dandia basi kwa mbele sikuwa na budi ya kufanya hichi nilicho kifanya leo. Naamini kwamba utakuwa unafahamu ni nani aliye iangamiza familia yako?”
“Ndio”
 
“Kwa nini ulipata nafasi na ukashindwa kumuua?”
“Muda ukifika nitahakikisha nitamua?”
“Dany huna muda tena, kweli umekaa meza moja na K2 ukashindwa kumuua. Natambua kwa sasa hato kuwa rafiki yako tena atakusaka kama anavyo nisaka mimi”
“Imekuwaje hadi leo mnatafutana?”
“Maslai madogo, ubabe wake isitoshe nilikuwa nina familia yangu tayari”
“Familia kivipi?”
“Meya wa jiji la Tanga ambaye ulimuua, alikuwa ni baba yangu, yeye na baba Hawa ni mtu na mdogo wake. Tulimchukulia K2 kama mtu wa karibu sana, akatushirikisha katika kikosi chake na kunifanya niwe mtu  niliye muamini kwa asilimia kubwa sana, ila alinisaliti”
“Alikusaliti kivipi?”
“Alinichukulia mwanaume wa maisha yangu, alinichukulia mwanaume niliye mpenda. Isitoshe akamuaa mwanaume huyo mbele ya macho yangu”
“Mwanaume huyo ni nani?”
“Ni raisi aliye pita”
“Ina maana K2 alimuua kaka yake?”
“Ndio”
Moyo wangu ukajikuta ukipatwa na ubaridi mkali sana, japo nipo kwenye mateso ila maneno ya Yudia yamezidi kunifanya kumchukia K2 na kuapia nikipata nafasi nyingine nitahakikisha kwamba nitakikata kichwa chake kwa mikono yangu mimi mwenyewe.

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...