Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 25, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 122 na 123 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588  ILIPOISHIA 
 “Baby hii kazi tunayo kwenda kuifanya ni hatari, nikifa hakikisha kwamba kisasi unakilipiza kwa wale wote walio kutendea ubaya, hususani baba yangu”
Hawa alizungumza kwa sauti ya chini, taratibu akausogeza mdomo wake karibu na wangu, nikaupokea taratibu na tukaanza kunyonyana, nikamuona Mariam aliye simama nyuma ya Hawa, uso wake ukijikunja na moja kwa moja nikatambua kwamba wivu ndio unao mpelekea kuwa katika hali hiyo ya chuki na hasira.
   
ENDELEA   
Taratibu nikamuachia Hawa na kuyashika mashavu yake kwa viganja vyangu.
“Nitakulinda mke wangu, nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda katika usalama”
“Nashukuru mume wangu”   
“Mkuu tuna dakika moja kabla ya kuzama kwenye maji”
Lusi alizungumza huku akitutazama, Hawa akanipiga busu la mdomo kisha akavaa mrija wa kuhemea. Kila mtu akavaa mrija wa kuhemea huku kila mmoja akiwa ameshika tochi ambazo hutumika hata ndani ya maji. Lusi kwa ishara ya vidole akaanza kuhesabu kuanzia tano, kuja nne, tatu, mbili hadi inafika moja kila mtu akaanza kujitosa kwenye maji akiwa na mtungi wake mgongoni. Sote tukazama ndani ya maji ya na kuanza kumfwata Lusi ambaye ndio muongozaji wa hii oparesheni. Katika masiha yangu nimewahi kufanya mambo mengi ya hatari ila hili la uzamiaji ndani ya maji tena usiku ni hatari sana kuliko hata nilivyo kuwa ninafikiria. Tukazidi kusonga mbele huku mara kwa mara Hawa alinisogelea karibu yangu na tunazungumza kwa ishara ya vidole. Tukazidi kusonga mbele, baada ya dakika kumi na tano tukaifikia meli hii ambayo ipo katika mwendo wa kawaida.
 
Lusi akaendelea kutuonyesha njia ya kupita ili kuepuka mtu kukatwa na ma feni makubwa yaliyopo pembezoni mwa hii hii meli huku chini ya maji. Lusi akaanza kufungua moja ya sehemu kwa kumia kifaa malumu cha kukatia, haikuchukua mud asana akafanikiwa kuikata sehemu hii. Akaanza kuingia yeye, akafwatia Mariam, Hawa, mimi kisha akamalizia mume wa Mariam.
“Hapa maji si yanaweza kuingia ndani ya meli?”
Nilimuuliza Lusi huku nikitazama sehemu tuliyo tumia kuingilia.
“Hapana, nitaifunga”
Lusi akaanza kuifunga sehemu hii kwa kutumia gundi ambayo ndani ya muda mchache ikawa imeganda. Kila mmoja akaanza kuvua vifaa tulivyo vitumia katika kuogelea. Lusi  akafungua begi lake ambalo haliingii maji, akatoa laptop ndogo, akaiwasha na kuanza kuiminya minya batani.
“Unafanyaje?”    
 
“Hapa nina hack system yote ya humu ndani, kuanzia kamera hadi uendeshaji wa mitambo”
“Lusi yupo vizuri kwenye maswala haya”
Hawa alizungumza na kunifanya nibaki kimya tu nikimuangalia Lusi jinsi anavyo fanya utundu wake kwenye maswala ya mitandao.
“Itachukua muda gani?”
“Five minutes”
“Ok”   
Tukaendelea kusubiri katika chumba hichi kilicho jaa mitambo ya uendeshaji wa hii meli. Ndani ya dakika tano mashine kadhaa ambazo zinatembea ndani ya hii meli zikaanza kuzima moja baada ya nyingine, Lusi akajawa na tabasamu kubwa usoni mwake. 
 
“Nimekata mawasiliano yao yote, hakuna mtu anaye weza kuwasiliana na simu kwenda sehemu yoyote ndani na hata nje ya ya hii meli. Na kwa sasa meli nimeisimamisha, ni wakati wetu wakuweza kufanya mashambulizi”
Lusi alizungumza huku akitutazama kila mmoja kwenye uso wake, akatoa vinasa sauti vidogo vya kuvaa masikioni, akatukabidhi kila mmoja.
“Naamini tunasikiana?”
“Ndio Lusi, je kuna walinzi wangapi ndani ya hii meli?”
“Wapo walinzi thelathini, hao ni walinzi wa hii meli, ila kuna walinzi wa matajiri binafsi zaidi ya ishirini”
“Sawa”
“Je simu za mikononi haziwezi kutoka?”
“Yaa mawasiliano yote nimakata, na hata wakiitafuta hii meli kwa satelaiti hawato weza kuiona”
 
“Jamani natambua nyinyi nyote hapa mupo kwa ajili yangu, hii kazi sio yangu mimi peke yangu kama Hawa, hii kazi ni kwa ajili yetu sote. Itapo tubidi kuua, itabidi kuweza kufanya hivyo kwa ajili ya kujilinda sisi wenyewe. Lengo kubwa linalo tupeleka humu ndani, kwanza ni kujipatia nguvu ya pesa ambayo sehemu yoyote na muda wowote tunaweza hata kuinunua serikali na kumgeukia baba yangu, natambu kila mmoja ameweza kufanyiwa mauvu na baba yangu, ni wakati wa sisi kuhakikisha kwamba tunafanikiwa katika hili”
Hawa alizungumza kwa kujiamini sana huku akimtazama kila mmoja machoni mwake.
“Tuna lisaa moja kuhakikisha kwamba oparesheni hii inakwenda vizuri. Tutajigawa katika makundi mawili, Dany utaongozana na Mariam na mimi nitaongozana na kaka yangu, Lusi wewe utahakikisha kwamba hakuna mawasiliano yoyote yanayo tolewa nje na hawa watu, na utatuelekeza ni wapi walipo walinzi ili iwe rahisi kwa sisi kuweza kuwafanyia mashambulizi”
 
“Sawa mkuu”
“Timu yangu itakuwa timu A na Dany timu yako itakuwa ni timu B. Narudia tena, inapo tulazimu kuua itabidi tuue na itapo tulazimu kumsukuma mtu ili kuhakikisha kwamba tunapata kile kilicho tupeleka humu dani, cheni za dhahabu madini kila kitu chenye thamani na kina weza kubebeka itatubasa kukibeba sawa”
 
“Sawa”
Lusi  akatukabidhi kila mmoja kibegi chepesi cha kuvaa mgongoni chenye mikanda myembamba sana.
“Hawa”   
Nilimuita Hawa huku nikisogea pembeni, akanifwata na kusimama mbele yangu.
“Kwa nini umefanya maamuzi haya”
“Maamuzi gani Dany?”
“Nilikuambia kwamba nitakulinda, sasa inakuwaje ujiweke timu moja na kaka yako na mimi unipatie Mariam”
“Nina maana yangu ya kufanya hivyo Dany”
“Maana gani, ikiwa unatambua kabisa kwamba Mariam ni adui yangu na unatambua bado nina hasira naye”
“Dany hii ni kazi, kwenye kazi ninakuomba uadui uuweke pembeni na mapenzi pia uyaweke pembeni kwa muda, tukimaliza hii kazi ndani ya lisaa kila jambo litaendelea kama ilivyo kuwa”
“Hujanifanyia haki Hawa, hata kama wewe watu hawa wanaisikiliza amri yako, ila na mimi pia unatakiwa kunisikiliza maoni yangu na si kujiamulia”
“Dany nikiwa kwenye kazi huwa ni mtu mwengine, nimepanga na maamuzi yangu hayawezi kuvunjika. Tuingie kwenye kazi”
Hawa baada ya kumaliza kuzungumza, akaondoka na kuniacha nikiwa ninamshangaa kila mtu kwenye hichi chumba aliweza kuyasikia mazungumzo yetu kwa maana vinasa sauti tulivyo vivaa masikioni mwetu vinanasa mazungumzo yetu watu wote watano.
“Lusi tuambie tunze upande gani?”
“Hapa tulipo ni chini kabisa ya meli, hii meli ika gorofa nne kwenda juu. Kuna ngazi za kuapndika kutokea humu ndani ambazo ni zile pale. Timu A inaweza kuchukua uangalizi wa gorofa ya kwanza na timu B inaweza kuchukua uangalizi wa gorofa ya pili na baada ya hapo kila mmoja anaweza kwenda kuchukua ungalizi wa gorofa moja moja”
“Sawa, tutawanyike”
Nikamtazama Hawa jinsi anavyo jiweka vizuri jaketi lake la kuzuia risasi, nikamtazama na Mariam, nikatamani kubaki nyuma kwenye hii kazi ila nikajiona ninaweza kusababisha kila jambo kufeli katika hii kazi. Nikaanza kutembea kuelekea kwenye ngazi huku nikiwa na bastola yangu moja mkononi. Nikasimama kwenye mlango, nikashia kitasa taaribu, nikaufungua na kuchungulia nje nikawaona mafundi wawili wakija katika usawa wa huu mlango. Niaifunga bastola yangu kiwambo cha kuzuia sauti, kisha nikajitokeza na kuwapiga wote risasi.
 
“Clear”
Nilizungumza huku nikianza kusonga mbele, Marim akaanza kunifwata huku na yeye akiwa na bastola yake mkoni. Tukaanza kuua walinzi mmoja baada ya mwingine huku tukifwata maelekezo ya Lusi kupitia vinasa sati tulivyo vivaa masikioni, tukapandisha katika gorofa ya pili. Kusema kweli hii meli imebeba mtajiri watupu kwa maana ina kila aina ya starehe. Nikachomoa bastola yangu ambayo sijaifunga kiwambo cha kuzuia sauti, nikapiga risasi juu, milio ya risasi ikawafanya watu kuanza kuchanganyikiwa na kulala chini. Hapa ndipo tukapa nafasi ya kuwaona walinzi, ambao walijikuta wakianza kujibu mashambulizi. Kutokana na uwezo mkubwa wa matukio haikuwa ni jambo gumu sana kwetu kuwashambulia hawa walinzi.
“Dany”
Mariam aliniita, kwa ishara akanikonyeza niiname kidogo, akafyatua risasi na kunifanya niangalie nyumba yangu na kumkuta mwanamama amelala chini, damu zikimtoka kifuani na mkononi mwake ana kiji bastola kidogo ambacho huwa kinaingia risasi tano.
“Kaa hapa”
Nilimuambia Mariam huku nikianza kuondoka”
“Dany”
“Ndio”
Mariam akanitazama kwa matamshi ya ishara yam domo pasipo kutoka sauti akaniomba niweze kurudi salama kwa maana ninakwenda gorofa nyingine, nikatingisha kichwa huku nikimyooshea kidole gumba. Nikaondoka katika gorofa hii na kuanza kuwasiliana na Lusi.
 
“Hawa ameshikilia gorofa ya kwanza na gorofa ya tatu yupo kaka, wewe nenda gorofa ya nne”
“Sawa, kuna walinzi wangapi?”
“Ahahaaa, subiri subiri kidogoo…….Wapo walinzi kumi na wote wamevaa suti”
“Poa”
Nikachomoa magazine ya bastola yangu hii, nikaitazama na kukuta ikiwa na risasi mbili, nikaitoa na kuweka nyingine, nikapandisha kwenye ngazi za kwenda gorofa ya nne ambayo ndipo wanapo kaa matajiri wenye pesa nyingi. Nikaanza kunyanta kwenye kordo hii iliyo tulia na ina vyumba vicheche sana.
 
“Dany”
“Ndio Lusi”
“Kushoto kwako kuna mlango umeouona”
“Ndio”
“Ingia hapo, kuna ukumbi na matajiri wote wapo humo ndani wamejificha na walinzi wao”
“Poa nimekupata, je kuna kamera za ndani?”
“Yaaa, kamera ya ndani inaonyesha kuna walinzi wanne wapo mlangoni na bastola zao wamezinyooshea mlangoni”
“Poa poa”
“Dany”
Niliisikia sauti ya Hawa
“Ndio”
“Ninakuomba usiingie hapo peke yako, ngoja nikusaidie”
“Kaa katika nafasi yako, tupo kazini sihitaji msaada wako. Ninajua nini ninafanya”
 
“Please Dany”
“Hawa ninajua ninacho kifanya”
Nilizungumza kwa hasira, nikaangalia katika kuta za hii kordo, kwenye moja ya kordo nikaona mtungi wa gesi, kwa harkaa nikaukimbilia nikauchukua na uchomoa sehemu ulipo chomekwa, nikarudi nao hadi kwenye mlango, nikausimamisha vizuri kisha nikaifungua gesi ikaanza kutoka taratibu, nikarudi nyuma hadi kwenye moja ya kona, nikakaulenga mtungi huo, nilipo hakikisha umekaa kwenye tageti ya mikono yangu, nikafyatua risasi kadhaa, mlipuko mkubwa ukatokea katika eneo hili, malango ukavunjika, nikasikia mlio ya risasi inavyo toka kwa mfululizo ndani ya ukumbi walio jificha matajiri wakubwa. Kwa haraka nikaaza kurudi hadi mlangoni nilicho kifanya ni kulala chini kwa haraka na kunza kuwashambulia walinzi baadhi kwa kutokea chini nilipo lala. Moshi unao endelea kuzagaa katika hili eneo ukawa ndio nafasi yangu nzuri ya kuwashambulia walinzi hawa.
 
Nikafanikiwa kuingia ndani ya ukumbi huu, huku nikizidi kushambuliana na walinzi hawa hadi nikafanikiwa kuwaua wote.
“Kweli Dany unajua unacho kifanya”
Niliisikia sauti ya Lusi akizungumza, nikatabasamu huku nikitazama kamera moja iliyopo humu ndani.
“Ukinyanyuka itakuwa ndio kifo chako kama hawa walinzi ambao mumewaamini na kuwapa pesa za kuwalinda nyinyi na familia zenu. Ninacho kihitaji mimi, ni pesa, dhahabu zenu ukikiuka kufanya ninacho kueleza basi nitakuua”
 
Nilizungumza kwa kingereza huku nikiwatazama wazee hawa wa jinsia ya kiume na kike.
“Mtoto wa malaya, ni nani aliye kutuma kuvamia hii meli”
Mzee mmoja alizungumza huku akijaribu kunyanyuka, nikampiga risasi mbili za miguu yake, akaanguka chini, kifudifudi mke wake anayanyuka na kumgeuza mume wake anaye lia kw uchungu sana.
“Ninarudia tena, atakaye leta ujinga nitamuua. Wewe nyanyuka hapo”
Nilimuita muhudumu mmoja wa kike, akanyanyuka huku akitetemeka sana. Nikamkabidhi kibegi changu kidogo na kumumrisha kuanza kumpitia tajiri mmoja baada ya mwengine na ahakikishe kwamba kila kitu cha thamani kinawekwa ndani ya kibegi changu. Muhudumu huyu akanza kupitisha kwa kila tajari, ila alipo fika kwa mwanaume mmoja aliye valia suti ya garama, akasimama na kuzidi kutetemeka.
“Mr president ninakuomba uweke”
 
Msichana huyo alizungumza kwa sauti ya chini sana ila niliweza kusikia anacho kizungumza, taratibu nikaanza kutembea kwa tahadhari hadi kwa mwanaume huyu, nikamtazama kwenye koti lake upande wa kushoto nikaona nembo ya bendera ya Marekani, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio. Taratibu mzee huyu akaingiza mkono wake mfukoni, nikajikuta nikiishika bastola yangu kwa umakini huku nikiwa nimemnyooshea kichwani mwake ili hata akitaka kutoa silaha basi nitamuwahi kumuua. Sikuamini macho yangu nilipo muona anatoa kitambulisho chenye nembo ya raisi wa marekani.
 
Nikampokonya mzee huyu, nikaisoma kitambulisho hichi na ni kweli kinamuonyesha ni raisi wa Marekani jambo lililo zidi kunitisha kwa maana natambua wanajeshi wa Marekani walio sambaa dunia nzima lazima kwa muda huu watakuwa wanamtafuta raisi wao.
“Fuc**”
Nilizungumza huku nikisoma jina la raisi huyu anaye itwa Donald Bsh
“Vipi?”
Lusi aliniuliza
“Kuna tatizo”
“Tatizo gani?”
Niliisikia sauti ya Hawa akiniuliza kwa shauku kubwa ya kuhitaji kufahamu, nikajikuta nikimtazama raisi Donald Bsh, taartibu akatingisha kichwa huku machozi yakimwagika usoni mwake jambo lililo nifanya nishushe pumzi nyingi na kushindwa kumjibu Hawa swali alilo niuliza.
 
AISIIIII……….U KILL ME 123 

“Dany zungumza kuna tatizo gani?”   
Hawa aliniuliza, nikaka kimya kwa sekunde huku nikimtazama raisi Donald Bsh
“Hakuna tatizo nimesha lishuhulikia”
“Sawa, tunadakika chache zilizo salia, kila mtu anatakiwa kumaliza kazi yake”
“Sawa mkuu”
Nikamshi mkono raisi na kumnyanyua juu, nikamsogeza pembeni kwenye sehemu ya vinywaji. Nikamziba mdomo na kisha nikatazama eneo la juu hapa, hakuna kamera, nikakivua kinasa sauti kilichopo sikioni na kukikanyaga chini, ninatambua wezangu wote lazima watasikia kelele kali.
“Mimi sio mtu mbaya kwako na wala sio mtu ninaye hitaji kukuumiza wewe, ninaitwa Dany. Natambua kwamba ni raisi wa nchi kubwa Marekani, sihitaji kuliweka taifa lako katika hali ngumu. Unachotakiwa kufanya ni hichi nitakacho kuambi. Sawa”
Raisi akatingisha kichwa huku akiwa amenitolea macho.
“Tulio iteka hii meli tupo wanne, ninaamini kwa sasa wezangu watakuwa katika harakati za kuja kunichukua, hakikisha kwamba unatafuta sehemu ambayo unaweza kujificha na yenye usalama, ninacho kuomba ni wewe kuchukua hii bastola na unipige risasi ya bega sawa”
 
“Siwezi kufanya hivyo”
“Usipo fanya hivyo wapo watakao kuja kukuaa humu ndani, najua waafrika wengi na hususani watu nilio kuwa nao kwenye hii kazi hawaipendi Marekani, na wakijua kwamba raisi wa Marekani yupo humu ndani watakuua, fanya nilicho kuambia sawa”
Raisi mwili mzima ukazidi kumtetemeka, nikamkabidhi bastola yangu, watu wote humu ndani wakaonekena kunishangaa kwa maamuzi ninayo yafanya.
“Unajua ni wapi kwa kijificha?”   
“Ndio kuna mlago hapa ndani ya huu ukumbi ninaweza kujificha na kuna chumba….chumba salama”
“Ok fanya hivyo”
Raisi akakafumba macho yake huku akiwa amejawa na woga mwingi sana, nikamsogelea na kuigandamiza bastola yangu kwenye bega, akafnyatua risasi iliyo ingia kwenye bega langu na kuniangusha chini. Japo ni maumivu makubwa sana ambayo ninayapata, ila sina jinsi zaidi ya kuhakikisha kwamba ninayaokoa maisha ya raisi huyu raisi. Hazikupita hata dakika mbili akaingia Hawa akiwa na bastola yake mkononi, watu wote ambao walianza kunyanyuka walijikuta wakirudi chini na kulala kwenye sakafu.
“Dany Dany”       
Hawa aliniita kwa haraka huku akinisogelea, akanishika bega langu na kunitazama jeraha langu.
“Ilikuwaje mume wangu”
Nilimtazama Hawa huku jasho likinimwagika usoni mwangu kwa maana maumivu ninayo jisikia ni makali sana.
“Dany amejeruhiwa kwa risasi, ninarudia tena Dany amejeruhiwa na risasi”
Hawa alizungumza huku akishika sikio lake, taratibu akaninyanyua, akawatazama walinzi nilio wauoa humu ndani.
 
“Pole mume wangu”   
“Hei wewe lete hicho kibegi”
Hawa alizungumza, dada muhudumua ambaye alikuwa ndio mkusanyaji wa vitu vyote vya garama nilivyo chukua kwa watu wote humu ndani. Hawa akakivaa kibegi hichimgongoni na tukaanza kutoka ndani ya chumba chichi huku tukiwaacha watu wakiwa wamelala chini. Tukaanza kushuka kwenye ngazi kueleka chini, tukafanikiwa kufika katika chumba killichopo chini kabisa tulipo ingilia.
“Lusi una vifaa vya huduma ya kwanza?”
“Ndio mkuu”
“Nitolee haraka”
Hawa alizungumza huku akinikalisha chini, wakaanza kunihudumia kuhakikisha kwamba wanaitoa risasi pamoja na kuzuia damu kutoka. Zoezi hili halikuchukua muda mwingi wakawa wamefanikiwa kunitoa risasi na kunifunga jeraha langu.
“Ni wakati wa kuondoka sasa”
“Ila mume wangu ataogeleje?”
“Katika hii meli kuna boti ndogo za dharura kuna moja ambayo tayari nimesha iweka tayari”
 
“Ipo wapi?”
“Kuna mlango ule pale tutapandisha juu kidogo na ngazi kisha tutakuta mlango mwengine ambao tukitoka hapo tutakuta hiyo boti”
Mariam na mume wake wakingia wakiwa pamoja. Tukaanza kutoka katika chumba hichi huku Hawa akinisaidia kutembea, tuapita katika sehemu ambayo Lusi alituelekeza, tukakuta boti ndogo ambazo mara nyingi zinatumika kwa dharura pale meli inapo patwa na dhahama ya kuzama. Tukapande sote na kuondoka eneo hili kwa kasi sana. Hawa akatoa rimoti ndogo na kuishika mkononi mwake huku akitazama meli hii tunayo zidi kuiacha.
“Unataka kufanyaje?”
Nilimuuliza Hawa huku nikimtazama.
“Tumetegema mabomu mule nataka kulipua meli nzima”
“Usifanye hivyo?”
“Dany hatuwezi kuacha meli hivi ikiwa nyuso zetu zimeonekana na watu wengi, wewe unafikiriaje kwa mfano tukaacha watu hai”
“Kuna watoto wadogo mule, hawajui hata raha ya maisha na unataka kulipua hembu achana na huo mpango”
“Siwezi”
 
Hawa akaminya batani ya rimoti aliyo ishika, milipuko mingi ikaanza kulipuka katika meli, jambo lililo nikasirisha sana. Hawa akanitazama akataka kunishika mkono wangu ila nikakwepesha asinishike. Safari yetu ikachukua karibia masaa mawili na tukafanikiwa kufika pembezoni mwa bahari. Nikashuka mwenyewe kwenye boti hii na wala sikuhitaji msaada wa mtu yoyote kwa maana msaada wote nilio utoa kwa raisi wa Marekani ni bure kwani yeye na watu wote walio baki hai wamelipuka kwenye kwenye meli hiyo.
“Mkuu gari lipo tayari”
Lusi alizungumza huku akimtazama Hawa usoni, sikuzungumza chochote zaidi ya kusimama pembeni kidogo, Hawa taratibu akaanza kunifwata.
“Dany mume wangu, natambua kwamba nitakuwa nimekuudhi, ila ninakuomba unisamehe”
Nikamuangalia Hawa, kisha nikampita pembeni yake, tukaanza kuelekea huko Lusi anapo sema kwamba kuna gari linalo tusubiria. Tukafika barabarani na kuwakuta walinzi wawili wa Hawa, kila mmoja akiwa na gari lake. 
 
“Dany”
“Nini?”
“Tuingie gari hili”
“Nitapanda huku”
“Tafadhali Dany, ninahitaji kuzungumza na wewe”
“Tutazungumza huko tunapo kwenda sawa”
“Sawa”
Safari ikaanza ya kuondoka eneo hili ikaanza huku nikiwa nimejawa na huzuni kubwa sana moyoni mwangu kuona maelfu ya watu walikuwa ndani ya meli hii wamekufa. Japo nimeua baadhi ya walinzi ila nilifanya hivyo kuhakikisha kwmaba ninajilinda mimi mwenyewe. Tukafika katika moja ya nyumba iliyopo porini, na wala sikufahamu tupo nchi gani. Tukashuka wote kwenye magari, katika eneo hili nikawakuta baadhi ya walinzi wa Hawa ambao ninawafahamu kutokana na mafadha yao waliyo yavaa. Tukaingia ndani, nikaka kwenye sofa la kujitenda, Hawa akanitazama kwa macho yaliyo jaa simanzi kisha akaanza kuzungumza.
 
“Tunashukuru Mungu kazi yetu imekwenda vizuri japo mwenzetu pale amepigwa risasi, imekwenda vizuri sana. Kwa sasa ningeomba tupumzike asubuhi na mapema tutapanga mipango ya kuhakikisha kwamba tunawarudia vipi maadui zetu”
“Sawa mkuu”
Hawa baada ya kumaliza kuzungumza nikawa wa kwanza kunyanyuka kwenye sofa, nikatoka nje na kumfanya Hawa anifwate kwa nyuma.
“Dany”
“Ndio”
“Kwa nini huitaji kuzungumza na mimi, kwani kuna kosa gani kubwa ambalo nimelifanya na litapelekea wewe kuninunia na kunikasirikia”
“Hawa nisikilize, sinto weze kuaendelea kufwata amri yako, eti kisa wewe umenisaidia sawa. Ninapokuwa ninakushauri kitu na kujiona wewe ndio wewe katika hilo jambo ni vyema kwa sasa nijivue”
“Ujivue, una maana gani?”
“Ili kulinda penzi langu mimi na wewe, nitahitaji kila mtu sasa hivi atumie jinsi anavyo weza yeye mwenyewe kulipiza kisasi sawa”
 
“Hapana Dany usizungumze hivyo”
“Kulikuwa na haja gani ya kuwau watu wengine, ninakueleza bado ukafanya, maana yake wewe si una mamlaka yako peko yako na huitaji mtu yoyote aweze kukushauri si ndio?”
Nilizungumza kwa hasira huku nikimsogelea Hawa karibu kabisa na uso wake. Hawa akakaa kimya huku akiwa amenikodolea macho.
“Umepata ambacho ulihitaji kukipata, basi kazi zako utazifanya wewe mwenyewe na mimi ninaomba nijiweke kando katika kila kazi yako”
“Dany”
Hawa aliniita huku machozi yakimwagika usoni mwake. Taratibu akaanza kushuka chini, akapiga magoti na kuishika miguu yangu kwa mikono yake huku akiangua kilio kikubwa.
“Dany naomba unisamehe mume wangu, siwezi kukaa mbali na wewe mume wangu. Ninakupenda sana, nilicho kifanya natambua ni makosa tafadhali sana mume wangu”
 
Taratibu nikamnyanyua Hawa, nikamkumbatia taratibu, tukarudi ndani kwa pamoja. Moja kwa moja tukapitiliza hadi chumbani. Hawa akanivua nguo zangu, akanibadilisha bandeji kwenye jeraha langu na kunifunga jeraha langu. Tukaingia bafuni na kuoga kwa pamoja. Usiku huu ni usiku wa furaha kwetu kwa maana tulijikuta tukizama kwenye penzi zito na Hawa, katika kitanda cha sita kwa sita kilichopoa humu ndani.
    Asubuhi na mapema nikaamka, nikavaa suruali yangu pamoja na tisheti nyepesi, nikatoka chumbani na kuelekea nje, nikawakuta walinzi wachache wakiwa wanaimarisha ulinzi. Nikaanza kuzunguka katika maeneo ya karibu katika hili eneo. Kwa mbali nikaona maji mengi ambayo kwa haraka haraka niliweza kugundua kwamba maji haya ni maji ya bahari. Nikaanza kutembea kwa taratibu kuelekea katika eneo hilo. Sikuchukua muda mrefu sana kufika katika fukwe hii iliyo tulli.
 
Kwa mbali kidogo nikaona boti ndogo iliyo goma kwenye mchanga mwingi ulipo kwenye fukwe hii. Nikaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu huku nikiwa makini sana, nikiwa karibu katika boti hii nikasikia sauti ya mtoto mchanga akilia sana ndani ya boti hii. Nikazidi kuongeza umakini wangu kuanzia kutembea hadi kutazama eneo zima la hii fukwe. Nikafika katika eneo la hii boti, nikafanikiwa kumkuta mtoto mdogo akiwa amelala kifuani mwa raisi Donald Bsh anaonekana kujawa na majeraha kadhaa mwilini mwake.

“Muheshimiwa raisi, muheshimiwa raisi”
Nilimuita huku nikimchukua mtoto huyu mchanga aliye lala kifuani mwake. Nikavua tisheti yangu kwa haraka, nikaitandika chini kisha nikamlaza mtoto huyu. Nilipo hakikisha ametulia, nikamtoa raisi Donald Bsh kwenye hii boti. Nikafungua vifungo vya shati lake, kisha nikasikilizia mapigo ya moyo wake yanavyo dunda kwenye kifua chake, kwa mbali nikasikia mtingishiko wa kifua chake ukiashiria kwamba mapigo yake ya moyo yapo vizuri. Nikampanua mdomo wake kidogo kisha nikaanza kumpulizia pumzi mdomoni mwake, nilipo hakikisha kwamba nimepulizia pumzi ya maana, nikaanza kukiminya kifua chake kwa nguvu, nikarudia tena kumpulizia raisi pumzi mdomoni mwake, gafla raisi akafumbua macho yake na kuanza kuhema kwa kasi.
 
“Mr president”
Nilimuita huku nikimtazama usoni mwake.
“Dany”
Raisi aliniita huku akiwa amenikazia macho. Hata kabla sijazungumza kitu chochote helicopter sita za kijeshi zikaanza  kutua katika eneo hili, huku zikiwa zimetuweka kati mimi na raisi. Wanajeshi wengi wa kimarekani wakaanza kushuka mmoja baada ya mwingine, huku wakiwa na bunduki zao mikonini na wakaniamrisha kunyoosha mikono juu na kukaa mbali na raisi wao. 

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )