Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 26, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 124 na 125 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA     

“Mr president”   
Nilimuita huku nikimtazama usoni mwake.
“Dany”           
Raisi aliniita huku akiwa amenikazia macho. Hata kabla sijazungumza kitu chochote helicopter sita za kijeshi zikaanza  kutua katika eneo hili, huku zikiwa zimetuweka kati mimi na raisi. Wanajeshi wengi wa kimarekani wakaanza kushuka mmoja baada ya mwingine, huku wakiwa na bunduki zao mikonini na wakaniamrisha kunyoosha mikono juu na kukaa mbali na raisi wao.
   
ENDELEA       
Gafla nikastukia kitu kizito kikinipiga kwa nyuma na kujikuta nikianguka chini na kupoteza fahamu.
                                                                                           ***
Taratibu nikayafungua macho yangu, nikaaza kutazama hili eneo nililopo. Ni ndani ya chumba kilicho pangiliwa vizuri, kitanda nilicho lalia kina ukubwa wa sita kwa sina na nikitanda cha kisasa kabisa. Taratibu nikakaa kitako huku nikijitama mwili wangu, jeraha lililopo begani mwangu, limefungwa vizuri tofauti na bandeji ambayo niliweza kufungwa mara ya kwanza na Hawa. 

Nikashuka kitandani huku nikiwa na boksa tu, nikapiga hatu hadi dirishani, nikafungua pazia na kuchungulia nje. Wingi wa magorofa makubwa kwenda juu, yakaniashiria kwabisa kwamba hapa nilipo ni nchini Marekani. Hata hapa nilipo nipo gorofani, mlango ukafunguliwa na kujikuta nikigeuka na kutazama ni nani anaye ingia.
 
“Habari yako bwana Daniel?”
Mzee mmoja mweusi kiasi alizungumza huku akitabamu sana usonimwake.
“Salama”
“Ninaitwa bwana Alexander Brown ni mshauri mkuu wa raisi wa Marekani”
“Nashukuru kukufahamu bwana Brown”
“Raisi anahitaji kuonana na wewe kuna mambo baadhi anahitaji kujadiliana nawe ikulu”
 
“Ikulu!!?”
Niliuliza huku macho yakinitoka kwa maana kusema kweli sikuwahi kufikiria hata siku moja kwamba ipo siku nitaingia kwenye ikulu tena ya Marekani.
“Ndio, na kwenye hilo kabati hapo kuna nguo unaweza kuzivaa, kisha nikakupeleka hoteli ukapata kifungua kinywa”
“Sawa bwana Brown”
Nilizungumza huku nikiwa na shauku kubwa sana ya kwenda kuingia ikulu ya Marekani, baada ya bwana Brown kutoka katika hichi chumba kwa haraka nikafungua kabati. Nikakuta suti mpya ikiwa kwenye makasha yake, imening’inizwa vizuri huku shati jeupe na tai nyeusi navyo zikiwa vimening’inizwa vizuri sana. 

Kwa furaha kubwa nikajikuta nikianza kuchaza stepu ambazo haya kwenye kwaya hazijawahi kutokea, nikajinyoosha viungo vyangu vya mwili, kisha nikaingia bafuni, nikaoga haraka pasipo kutotesha bandeji niliyo fungwakwenye bega langu. 

Nikajifuta mwili wangu kwa taulo kubwa linalo nukia vizuri, nililipo hakikisha kwamba nipo vizuri. Nikaanza kuvaa kitu kimoja baada ya kingine. Nilipo maliza nikasimama kwenye kioo hichi, huku nikijitazama juu hadi chini.
 
“Viatu”   
Nilizungumza huku nikifungua kabati hili tena, nikavuta droo moja iliyopo chini, nikakuta viatu pamoja na saa ambayo kwa muonekano wa haraka haraka inaonekana ina thamani kubwa sana.
“Asante Mungu”   
Nilijikuta nikitamka maeno hayo kwa furaha kubwa sana. Nilipo maliza kujiandaa, nikapiga hatua hadi mlangoni, nikafungua mlango na kuchungulia nje, nikakuta walinzi wanne pamoja na bwana Brown wakiwa wamesimama wakinisubiria mimi kutoka. 
 
“Twende huku Dany”   
“Sawa”
“Chukua kitambulisho hichi, uvae shingoni mwako kwani mtu haruhusiwi kuingi White House pasipo kuwa na kitambulisho husika”
“Sawa mkuu”
Nikatazama kitambulisho hichi nikakuta kikiwa na picha yangu pamoja na jina langu na la baba yangu, sikutaka kuhoji sana kwa maana nina tambua kwamba wamarekani wana njia nyingi za kuweza kumfahamu mtu kwa undani. Tukaingia kwenye gari moja refu ambalo kwa Tanzania tumezoea kuliita Six door(Milango sita). Mbele yetu zikatangulia pikipiki mbili za polisi huku nyuma yatu kukiwa na gari jeusi likituftwa.
 
“Dany hongera sana”
“Hongera ya nini muheshimiwa?”
“Umeweza kuyaokoa maisha ya raisi wetu””
“Ilikuwa ni jukumu langu kufanya hivyo kwa maana sina roho mbaya”
“Unaonekena”
“Ila ni kwa nini raisi amenileta hapa Marekani?”
“Kusema kweli kwangu mimi sifahamu, ila raisi yeye mwenyewe ndio anaye fahamu. Sisi huwa tunafwata amri yake tu”
“Sawa sawa”
Gari hizi zikasimama kwenye moja ya mgahawa, nikashuka na muheshimiwa Brown.
“Agizia chochote unacho kihitaji?”
“Kwa asubuhi hii sinto kula sana”
“Huwa waafrika sifa yao kubwa ni kwamba wanapenda kula, je ni kweli?”
 
“Hapana, ila wapo baadhi yao wanapenda kula sana, na wapo wanao penda kula kawaida”
Nikaagizia sambusa moja pamoja na chai ya maziwa. Muhudumu akanihudumia kwa haraka sana, nikanywa chai hii kwa haraka ili tu niwahi kwenda kuingia White House.
Tukatoka kwenye mgahawa huu na kuingia kwenye magari, safari ikazidi kusonga mbele huku polisi pikipiki zao zikipiga ving’ora na gari na kila sehemu tunapo pita magari yanatupisha. Kwa mbali nikaliona jengo la White House ambalo kwa mara nyingi huwa ninaliona kwenye baadhi ya filamu za Kimarekani.
 
Ndani ya muda mfupi gari zikaingia kwenye uzio wa ikulu na kusema kweli, nimeingia kwenye ikulu yetu Tanzania ila sijawahi kuona ulinzi mkali kama kwenye hii ikulu. Walinzi walio valia suti nyeusi wana randa randa kila eneo kuhakikisha tu kwamba usalama unakuwa madhubuti.
Moja kwa moja tukaingia ndani, kwenye kordo hizi zimejaa walinzi hadi sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi. Tukafika kwenye moja ya mlango, nikatazama juu kidogo nikaona maandishi yaliyo andikwa kwamba hii ndio ofisi ya raisi(President’s Office). Bwana Brown akagonga mlango, baada ya sekunde kadhaa ukafunguliwa kwa ndani na tukaruhusiwa kuingia. Raisi Donald Bush alipo nioana kwa haraka akanyanyuka kwenye kiti alicho kalia na kunifwata, akanipa mkono wa kulia na mimi nikampatia wangu.
“Karibu sana bwana Daniel”
“Shukrani muheshimiwa raisi”
“Karibu ukae”
Nikakaa kwenye sofa nzuri zilizopo ndani ya hii ofisi, bwana Brown naye akaka kwenye sofa jingine kwa ajili ya mazungumzo.
“Dany nashukuru kwa kuweza kuitikia muito wangu, natambua ni mambo mengi yalikuwa yakiendelea nyuma yako”
 
“Ni kweli muheshimiwa”
“Nimeweza kupitia faili lako, hususani maisha yako ya nyuma, ila sijaona kosa lolote ambalo ulilifanya tangu ulivyo kuwa katika kikosi cha NSS”
“Ni kweli”
“Sasa nimekuita hapa kwa ajili ya kazi moja kubwa sana, ninaamini kupitia wewe tunaweza kuifanya Afrika kuwa bara salama na bara lenye amani. Tunahitaji kufuta rushwa, ugaidi ambao unaendeshwa na baadhi ya viongozi walimo kwenye ngazi za juu katika serikali baadhi ya nchi za Afrika”
“Ni kweli muheshimiwa raisi”
“Kitu kimoja nilicho kigundua kutoka kwako, ni kwamba una kipaji kikubwa sana. Tena kipaji chako cha upambanaji ukikitumia vizuri unaweza kufuta giza linalo imulika nchi yako, japo wananchi bado hawaelewi ni kitu gani kinacho endelea katika serikali yao”
“Kweli muheshimiwa raisi”
“Brown naomba faili”
Bwana Brown akasimama na kuchukua faili lilipo juu ya meza ya raisi, akamkabidhi raisi aliye anza kulifunua tartaibu, akalitazama karatasi zake kwa sekunde kadhaa kisha akanikabidhi mimi.
 
“Humo kwenye hilo faili kuna malekezo na mipango yote ambayo tunahitaji wewe kuweza kuifanya. Nchi yangu hususani mimi nitakuwa nyuma yako kuhakikisha kwamba unharibu mifumo yote ya makundi ya kigaidi tukianzia na Al-Shabab, Boko Haramu na Al-Lady”
“Samahani muheshimiwa raisi ninaomba kuuliza”
“Uliza tu”
“Hili kundi la Al-Lady ndio mara yangu  ya kwanza kulisikia”
“Hilo kundi ukifungua nyuma huko utaona maelezo yake. Ila kwa kifupi ni kikundi ambacho kinamilikiwa na kiongozi wa nchi yako, na wafuasi wake ni wanajeshi wa kike ambao anawachukua kuanzi wakiwa watoto hadi kufika ukubwani. Kwa mtazamo unaweza kuona kwamba huyo Livna Livba ndio mkuu wao ila raisi wako ndio yupo nyuma ya hili”
“Kwa nini muheshimiwa raisi musiweze kulichukulia hatua hili jambo?”
“Hatuna ushaidi katika hili, ndio maana mataifa makubwa tunaendelea kuweza mashinikizo kwenye baadhi ya nchi za Afrika ili wamiliki wa hayo makundi waweze kushuka chini, ila kama unavyo jua, nchi kubwa hususani nchi yangu Marekani, hatupatani na nchi nyingi za kiarabu jambo linalo pelekea nchi hizo kuwapa misaada ya kipesa, silaha kwa viongozi hao wa nchi za kiafrika jambo linalo fanya kupata uzito wa kuweza kufwatilia maswala hayo”
Nikashusha pumzi huku nikitazama fiali hili, nikaipna picha ya Livna Livba ikiwa ni moja wapo ya viongozi wa vikundi vya magaidi. Picha nyingine nikamuona baba Hawa akiwa ni kiongozi wa Al-Shabab huku katika kundi la Boko Haramu nikimuona mkuu mmoja anaye itwa Generali Obote Mohamed.
“Hii kazi itaendesha na ofisi yangu ya raisi, ni kazi ya siri sana, utasimama kama mpelelezi wa kiserikali, tutakupa kila aina ya uwezo kuhakikisha kwamba hii kazi inakwenda vizuri”
“Sawa muheshimiwa raisi. Ninaweza kuuliza swali jingine?”
“Uliza tu?”
“Vipi watu kwenye meli waliweza kusalimika?”
Taratibu raisi nikaona furaha yake ikiisha usoni mwake, akamisha chini kichwa chake huku machozi yakimlenga lenga. Tukatazamana na bwana Brown kwa sekunde kadhaa, mguno wa raisi ukatufanya sote kumtazama.
“Mimi na yule kichanga ndio tulifanikiwa kutoka kwenye ile meli, ila wengine wote walifariki dunia katika mlipuko”
“Pole sana muheshimiwa”
 
“Asante , ila rafiki zako ambao walihusika kwenye huu mpango wa kuua maelfu ya watu ndani ya meli, tumeweza kuwakamata na wapo chini ya ulinzi wanaendelea kuhojiwa”
Nikajikuta nikibaki na kigugumizi kikali, nikatamani kuzungumza kitu ila mdomo wangu ukajikuta ukiwa mzito kiasi.
“Una kitu unahitaji kuzungumza juu ya hili?”
“Hapana muheshimiwa raisi, ila nitahitaji kuwaona nao”
“Unaweza kuwaona kwa hilo haina shida”
“Muheshimiwa raisi bila ya kuingilia maamuzi yako ila ninaona hilo jambo sio zuri sana kwa bwana Dany kuweza kulifanya”
“Kwa nini?”
“Tunahitaji kumtumia bwana Dany katika kuendesha hii oparesheni, kuonana na wezake na akiwa katika hali nzuri kama hiyo inaweza kuwafanya wezake kumuona kwamba yeye ni msaliti”
 
“Unashuuri nini bwana Browin”
“Ninacho kushauri muheshimiwa raisi kwa sasa tuhakikishe kwamba tunamuweka mbali bwana Daniel na wezake”
“Samahani kwa kuwaingilia, kwani hadi sasa hivi tangu wahojiwe je kuna jambo lolote ambalo wameweza kuzungumza”
“Hakuna walicho kizungumza”
“Kama hamuta jali ninaomba nionane nao, kwa maana wao watakuwa ni msaada mkubwa sana kwetu”
Muheshimiwa raisi Donald Bush akanitazama usoni mwangu kisha akamtazama bwana Brown, kisha akatingisha kichwa.
“Nimekubaliana na wewe”
Raisi alizungumza kisha akanyanyuka, akachukua mkonga wa simu ya mezani, akaminya moja ya batani na kuiweka sikioni mwake. 
 
“Andaeni magari mawili, bwana Daniel anapelekwa kwenye kikosi cha FBI, nitahitaji aonane na waalifu wote”
Raisi Donald Bush alizungumza na kukata simu.
“Muheshimiwa raisi bwana Daniel hawezi kwenda kuwaona wezake akiwa hivi amependeza, ni lazima watamuona yeye ni msaliti”
“Bwana Browin maamuzi yangu yamesha pita”
“Samahani, ninaweza kupatiwa nguo za wafungwa”
“Ndio”
“Ngingeziomba, nahitaji kufanana na wao”
“Sawa, Brown lishuhulikie hilo swala haraka iwezekanavyo”
“Sawa muheshimiwa raisi”
 
Nikaagana na muheshimiwa raisi, tukatoka ofisini hapa tukiwa tumeongozana na bwana Brown, akanikabidhi kwa mlinzi mmoja wa ikulu. Tukaingia kwenye gari za ikulu na safari ya kueleka kwenye makao makuu ya FBI ikaanza. Safari ikatuchukua muda mrefu kidogo na tukafika katika makao makuu ya FBI, moja kwa moja nikakabidhiwa kwa mkuu wa kikosi hichi cha FBI, nikaingizwa kwenye moja ya chumba, nikakabidhiwa nguo za wafungwa, nikavua nguo zangu na kuvaa vazi hili la kifungwa.
“Nifungeni pingu”
“Sawa”
Nikafungwa pingu za mikonini pamoja na nyororo ndefu miguuni mwangu. Askari wawili wakanipeleka kwenye chumba ambacho nikamkuta Hawa akiwa amechoka kwa kipigo kizito alicho patiwa. Hata kuingia kwangu ndani ya hichi chumba Hawa hajaweza kuniona kutokana na kichwa chake kukiinaminisha chini. Askari hawa wakatoka na kuniacha pake yangu na Hawa, taratibu nikaanza kutembea hadi kwenye kiti alicho kaa Hawa. Nikapiga magoti chini kwa mikono yangu yote miwili nikanyanyua kichwa chake.
 
“Hawa”
Nilimuita kwa sauti ya chini, taratibu Hawa akatafumbua macho yake. Tabasamu pana likaanza kumjaa usoni mwake.
“Dany mume wangu”
“Nipo hapa mke wangu”
Machozi yakaanza kumwagika Hawa taratibu, akusogeza mdomo wake karibu kabisa na mdomo wangu, akausitisha kwa muda kidogo kama mtu anaye tafakari kitu. Gafla nikastulia akinipiga kichwani mwangu kwa kwa nguvu kwa kutumia kichwa chake na kinifanya nianguke chini huku nikihisi kizungu zungu kikali sana.
“Wewe ni muongo msaliti mkubwa wewee”
Hawa alizungumza maneno hayo kwa hasira huku akilia kwa uchungua sana jambo lililo ufanya moyo wangu kuniuma sana.
                                                                           
AISIIIII……….U KILL ME 125

“Baby”       
Niliita taratibu huku nikinyanyuka chini nilipo anguka.
“Mimi sio baby wako, ninakuomba tena usinijue na usinifahamu. Dany nimefanya mambo yote kwa ajili yako leo hii umenifanya nishikiliwe na mikono ya hawa mashetani wa Marekani”
 
Hawa alizungumza huku machozi yakimwagika uso mzima.
“Hawa unazungumza nini mbona hata mimi mwenye nimeshikiliwa kama unavyo niona hapa”
Nilizungumza kwa msisitizo na kumfanya Hawa anitazama kuanzia juu hadi chini, kwa mavazi niliyo yavaa dhairi kwamba yanaonyesha kwamba na mimi ni mtuhumiwa katika hii kesi.
“Kwa nini hukuniambia kwamba kwenye ile meli kulikuwa na raisi tena wa Marekani?”
“Raisi?”
“Ndio kitabulisho cha raisi wa marekani nilikikuta chumbani kwetu kikiwa kimeanguka.  Na hicho ndicho kilicho tufanya sisi Wamarekani waweze kutukamata”
 Nikajifanya ninacheka kwa huzuni, huku machozi yakinimwagika usoni mwangu ili kuendelea kulinda uaminifu wangu kwa Hawa.
“Ina maana kwamba mimi ndio nimekileta kitambulisho hicho ndani kwetu?”
 
“Mimi na wewe ndio tulio ingia ndani ya chumba chetu inakuwaje kikwa humo?”
“Unaamini vipi kama mimi ndio niliye kileta wakati tumechukua vitu vingi kwa wale abiria ndani ya meli, iweje wewe uhisi mimi nimekileta na kama ningekuwa ninajua kwamba ndani ya meli kuna raisi basi tungekuwa tumepata mtu wa thamani kubwa kuliko vitu tulivyo vichukua. Kitu kingine kumbuka si kila mtu wako anakupenda lazima kutakuwa na msaliti, laiti na mimi ningekuwa ni msaliti basi nisinge shikiliwa na wala nisinge kuwepo kwenye hili jengo pamoja nanyi”
Maneno yangu yakamfanya Hawa kunitazama machoni mwangu kwa kunichunguza, uzuri ni kwamba ninaweza kuingiza kila hali ambayo ni ya uongo na kuifanya kuwa ya ukweli kwenye maisha yangu.
 
“Dany am sorry mume wangu”
Taratibu nikamkumbatia Hawa huku sote tukimwagikwa na machozi mengi kwenye nyuso zetu. Taratibu Hawa akanibusu mdomoni mwangu, tukajikuta tukinyonyana midomo yetu taratibu sana.
“Dany maisha yetu yote kwa sasa yataishia gerezani, samahani kwa kukuangusha katika harakati za kulipiza kisasi”
“Usiseme hivyo mke wangu, naamini kwamba tuna nafasi ya kuweza kutoka”
“Kivipi Dany, tazama ulinzi ulivyo mkali, hawa watu wana roho mbaya, hapa nilipo wamesha nichoma sindano zaidi tatu za maaumivu ili mradi niweze kuzungumza ukweli”
“Usijali mke wangu nitahakikisha kwamba tunatoka hapa”
“Dany ninakuomba usiyatoe maisha yako kwa ajili yangu, una sa…..”
 
Nikamuwekea Hawa kidole changu mdomoni, kumnyamazisha asizidi kuzungumza sana.
“Kama wewe ulivyo poteza kila kitu kwa ajili yangu, basi na mimi nitapoteza maisha kwa ajili yako sawa”
Hawa akanijibu kwa kutingisha kichwa kwa kunikubalia huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Taratibu tukakumbatiana tena na kuachiana, nikanyanyuka na kuanza kutembe kuelekea mlangoni.
“Dany?”   
“Ndio”
Niliitika huku nikigeuka na kumtazama Hawa usoni mwake.
“Vyovyote itakavyo kuwa hakikisha kwamba huzungumzi chochote kwao”
“Nimekuelewa mke wangu”
“Kuwa muangalifu”
“Asante”
Nikagonga mpango ukafunguliwa, nikatoka katika chumba chihi, nikafunguliwa pingu pamoja na minyororo iliyo fungwa miguuni mwangu, moja kwa moja nikaelekea katika chumba cha kubadilishina nguo, nikavaa nguo zangu kisha nikamfwata mkuu wa F.B.I.
“Ninahitaji kuzungumza na raisi”
“Twende huku”
 
Nikaingia naye kwenye moja ya ofisi ya vioo. Nikaka kwenye moja ya kiti ambacho mbele yake kuna Tv kubwa. Baada ya sekunde kadhaa nikamuona raisi kwenye Tv hii.
“Muheshimiwa raisi”   
“Ndio Dany”
“Nimemzungumza na Hawa, ila nimeshindwa kumuuliza maswali ambayo nyinyi mulihitaji kutafahamu”
“Kwa nini?”
“Hawa alisha anza kunihisi kwamba mimi ni msaliti kati yao. Ili kujiaminisha kwamba mimi si……”
“Samahani Dany kwa kukukatisha, ila si ulivaa nguo za kifungwa?”
“Ndio muheshimiwa raisi, ila nguo za kifungwa hazikuwa kielelezo kikubwa cha kumfanya Hawa kuweza kunielewa, ninacho kuomba muheshimiwa raisi, inabidi hapa tufanye mchazo ambao utawafunga akili wao”
 
“Mchezo gani Dany, kwa maana wenzako ni magaidi”
“Ndio muheshimiwa raisi, ila ni rahisi sana kumtumia gaidi kumpata gaidi na ni ngumu sana kumtumia mpelelezi kumpata gaidi huwa inahitajika akili ya ziada”
“Ni mchezo gani huo unahitaji mimi niufanye?”
“Ninaomba kwamba tuweze kupatiwa ndege ambayo itatupeleka moja kwa moja hadi Afrika hususani katika nchi ambayo muheshimiwa raisi utahitaji mimi niweze kuianza oparesheni yangu. Tukifika hapo mimi nitajua ni kitu gani cha kufanya kuhakikisha kwamba oparesheni yetu inakwenda vizuri. Cha pili muheshimiwa raisi, ningeomba waandaliwe watu watakao ingiza kujihusisha katika shambulizi la kutuokoa, mimi na wezangu tukiwa tunahamishwa, watu hao ndio watakao tupeleka hadi kwenye ndege itakayo tupeleka Afrika”
 
Nikamuona raisi Donald Bush akifumba macho yake kwa maana jambo nililo lizungumza, ni gumu sana kwenye maamuzi ya raisi kama raisi.
“Muheshimiwa raisi samahani kama nina yaingilia mazungumzo yenu”
Mkuu wa F.B.I alizungumza na kunifanya nimtazame.
“Zungumza Malki”
“Hii oparesheni anayo izungumza bwana Dany, ninaona ni oparesheni ya kijinga ama kipuuzi, itanipotezea watu wangu na pia itatia dosari kitengo changu, ikiwa ina fahamika magaidi walio waua maelfu ya Wamarekani kwenye meli leo hii wapo mikononi F.B.I na leo waambiwe kama wametoroka, hapo kusema kweli muheshimiwa raisi sikubaliani na mawazo ya Dany”
 
“Muheshimiwa raisi, hii ndio nafasi ya pekee kuhakikisha kwamba unaweza kututumia sisi na kuitekeleza kazi yako, kuliko kupelka mamia ya wanajeshi Somalia  wengi wao wanapoteza maisha bila sababu ya msingi. Tafadhali muheshimiwa raisi ninakuomba ulifikiria hili pia”
Ukimya wa raisi ukatufanya mimi na mkuu huyu wa F.B.I mbaye muonekano wake tu, hanipendi hata kuniona sehemu hii.
“Mushimiwa raisi na ukumbuke kwamba sera ya nchi yetu ya Marekani, ni kwamba hatufanyi makubaliano na magaidi na kazi yetu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunawaangusha magaidi chini”
 
“Muheshimiwa raisi, kumbuka kwamba nimeyaokoa maisha yako na nilijitahidi kuhakikisha kwamba ninajijeruhi mwenyewe kuyaokoa maisha yako, na laiti kama ningekuwa nina roho mbaya basi hata wewe ningekuua. Muheshimiwa raisi hii ndio nafasi ya pekee kutuaachia sisi Waafrika kujikomboa wenyewe”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga kwa mbali. Muheshimiwa raisi akakohoa kidogo kisha akatutazama.
“Malki hakikisha unafanya kile ambacho Dany anakihitaji”
“Muheshimiwa raisi….”
“Maamuzi yangu Malki hayapingwi, mimi ndio raisi wa nchi hii ya Marekani fanya kile nilicho kuagiza. Sawa?”
Raisi alizungumza kwa ukali na kumfanya mkuu wa F.B.I kuwa mpole.
 
“Sawa muheshimiwa raisi”   
“Dany nimekuamini na ninakuomba uweze kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba opareheni inakwenda vizuri”
“Sawa muheshimiwa raisi na asante kwa maamuzi yako, sinto kuangusha katika hili na kila gaidi uliye nipa kazi yake nitahakikisha unaishuhudia maiti yake”
“Sawa safari njema”
Mkuu wa F.B. akazima Tv hii huku usoni mwake akionekana kujawa na hasira kali, nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kaa na kumsogelea bwana Malki hadi karibu kabisa ya uso wake.
“Utafanya kile nitakacho kuambia ufanye na sinto hitaji kupingwa kwa chochote”
 
Nilizungumza huku nikiwa nimemkazia macho bwana Malik, na yeye akanikazia macho tena kwa msisitizo mkubwa sana.
“Usiombe mtu wangu hata mmoja akapotea ni lazima risasi yangu iingie kwenye kichwa chako, haiwezekani muafrika akanizidi akili”
“Tambua Muafrika ana akili kuliko Mmarekani, tulicho zidiana ni majengo tu basi”
“Ok, sihitaji mabishano na wewe, zungumza unahitaji nini?”
“Mahitaji yangu umeyasikia nilipo zungumza na muheshimiwa riasi, cha kufanya wewe, hakikisha kila kitu ninacho kuhitaji kinakamilika. Muda wa kusafirisha wafungwa ni saa mbili usiku na tukio litokee saa mbili na dakika thelathini usiku. Nimemaliza, fanya hivyo sawa”
“Sawa”
Bwana Malk akatoka kwenye ofisi hii kwa hasira kali sana na kuniacha mimi peke yangu, nikiwa ninatazama tazama wafanyakazi wengine wanao pita pita nje ya hii ofisi. Nikakaa ndani ya hii ofisi huku nikiwa ninafikiria hii kazi itakavyo kwenda, katika masiha yangu hii ndio nafasi yangu ya mwisho kutumia akili kubwa sana kuwaangusaha maadui zangu, huku nikiwa nina msaada wa muheshimiwa raisi wa Marekani bwana Donald Bush.
‘Mungu nisaidie’   
Nilizungumza huku nikimtazama Bwana Malki akija katika ofisi hii akiwa ameongozana na jamaa mmoja mwenye ndevu nyingi usoni mwake.  Wakaingia ndani ya hii ofisi ikabidi kunyanyuka na kusalimana na jamaa huyu.
 
“Asalam alaykum”
Mtu huyu alinisalimia huku akinipatia mkono wa kulia, nikaupokea taratibu huku nikiwa nimejawa na tabasamu pana usoni mwake.
“Walyakum mslam”
“Dewil huyu anaitwa Dany na Dany huyu anaitwa Dewil, ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano hapa F.B.I kwa upandw wa Pakistani”
“Ninashukuru kukufahamu bwana Dewil”
“Hata mimi ninashukuru kukufahamu bwana Dany. Nimesikia mpango wako nilio elezewa na mkuu hapa, tayari nimesha andaa vijana wa hiyo kazi na watajipanga pale muda utakapo jitokeza”
“Nashukuru kwa hilo bwana Dewil, vijana wako watakuwa ni wa aina gani?”
“Watakuwa ni Wapakistani, na watakupeleka moja kwa moja hadi kwenye ndege na humo utakuta kila kitu cha kazi yako kuelekea nchini Afrika”
 
“Nashukuru bwana Dewil”
“Unaweza kwenda bwana Dewil”
“Sawa mkuu”
Bwana Dewil akatoka, na kuniacha na bwana Malki.
“Ole wako opareheni hii ifeli au iwe ni njia moja wapo ya wewe kuwatorosha wezako. Nitahakikisha kwamba ninakusaka popote duniani, na nikikukamata nitakuua kwa mkono wangu, kama nyinyi mulivyo muua mke wangu kwenye mlipuko wa hiyo meli”
“Mbaya haito feli na ikufulu…….Mungu mwenyewe ndio atakaye fahamu nini nitakacho kufanya”
Tukatazama na bwana Malki kwa hasira sana, mlango wa hii ofisi ukafunguliwa na akaingia mwanaume msichana mmoja mrefu na mwenye asili ya kiafrika.
 
“Mkuu kuna simu yako kutoka ikulu unaweza kuipokea katika simu yako hiyo hapo mezani”
Bwana Malki akapiga hatua hadi mezani akaichukua simu hii na kuminya batani moja kisha akaiweka sikio la upande wa kushoto.
“Ndio”
“Nimekuelewa mkuu”
“Asante”
Bwana Malki akakata simu hiyo huku akinitazama usoni mwangu.
“Nifwate”
Bwana Malki alizungumza huku akinitazama kwa jazba. Tukatoka katika hii ofisi moja kwa moja tukaelekea hadi kwenye ukumbi ulio jaa viti. Taa za ukumbi huu zikazimwa, na projecta inayo piga mwanga wake ukutani ikawashwa, nikaanza kuona taratibu za oparesheni yangu nitakavyo kwenda barani Afrika ninavyo takiwa kuifanya.
 
“Tutaanzia nchini Somali, kisha Nigeria na kumalizia Tanza”
Mwanaume tuliye mkuta humu ndani alizungumza huku akinionyesha ramani za nchi hizi tatu alizo zitaja.
“Somalia, kundi la Al-Shabab ni kubwa sana, na lina watu wengi sana ambao sio rahisi sana kuweza kuwafahamu kiurahisi. Unacho takiwa kukifanya Dany na watu wako ni kujiweka katika mazingira ya kawaida.”
Mtu huyu akaendelea kunipa maelezo kwa nchi ya Nigeri na Tanza, tulipo maliza majadiliano haya ya nini ninacho takiwa kukifanya katika nchi hizi tatu, tukatoka katika chumba hichi.
“Ninahitaji kitu”
Nilimuambia bwana Malki na kumfanya asimame na kunitazama usoni mwangu.
 
“Nini?”
“Ninahitaji watu wangu wapatiwe chakula kwa maana wana njaa”
“Sawa, kuna kingine”
“Hakuna”
Bwana Malki akanirudisha kwenye ofisini niliyo kuwa. Masaa yakazidi kwenda, huku mara kwa mara nikiwa na kazi ya kuitazama saa yangu ya mkononi. Ilipo timu majira ya saa mbili kasoro robo nipelekwa katika chumba, nikabadilisha nguo zangu na kuvaa nguo za garezani, nikafungwa pingu pamoja nyororo miguuni mwangu, nikavaa raba nyeusi na nikaanza kupelekwa katika chumba amacho nikawakuta Hawa, Mariam, mume wa Mariam, Lusi pamoja na wasichana wengine wawili ambao nao ni walinzi wa Hawa.
Hawa akataka kunyanyuka ili anikumbatie ila akazuiwa na askari wa kike na kumfanya akae hapo hapo alipo kaa. Mariam akanitazama kwa macho makali, sikuzungumza kitu cha aina yoyote na nikajifanya kwamba nimenuna sana.
“Nyanyukeni”
Tuliamrishwa na sote tukanyanyuka, wakaingia wanaume kumi walio jazia miili yao, majaketi yao ya kuzuia risasi yameandikwa kwa maandishi meupe FBI. Wakatushika kwenye mikono yetu maeneo ya makwapa, wakatutoa katika chumba hichi. Tukaingizwa kwenye moja ya gari jeusi aina ya Van. Gari hili ikafungwa kwa nyuma, baada ya sekunde kadhaa. Tukaanza kusikia ving’ora vya magari haya ya wana FBI.
 
“Dany”
Hawa aliniita kwa upole.
“Mmmm”
“Upo salama?”
“Ndio, mke wangu. Jamani tunatakiwa kufanya jambo”
Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikitazama mbele ya gari hili. Tumetendanishwa na nondo ngumu kati yetu sisi na dereva. Kitu ambacho kusema kweli sio rahisi kwa sisi kuweza kumsumbua wala kumgusa dereva.
“Dany hatuna la kufanya na wewe”
Mariam alizungumza kwa sauti iliyo jaa hasira.
“Unazungumza nini Mariam”
“Hakuna mtu ambaye anaweza kushirikiana na wewe, unanuka usaliti”
 
“Hawa waeleze mimi ni msaliti kweli”
Hawa akakaa kimya huku kichwa chake akiwa amekiinamisha chini. Gafla tukastukia gari letu likinyanyuliwa juu, kisha likaangukia kiupande na kutufanya sote kujibamiza bamiza, gari likaanza kuserereka barabarani na kutufanya sote humu ndani kila mmoja kuomba sala yake. Gari likasimama, tukaanza kusikia mirindino ya milio ya risasi, kimoyo moyo nikaanza kujawa na furaha kwa maana mpango wetu unakwenda kama tulivyo pangwa. Mlango wa nyuma ya gari letu ukafunguliwa, wanaume wawili walio funika nyuso zao na kuacha macho yao tu huku mikononi mwao wakiwa na bunduki, wakaanza kuwatoa wezangu mmoja baada ya mwingine ndani ya gari hili na mimi nikawa wa mwisho kutolewa. 

Cha kusangaza Hawa na wezake wote wao wamesimama ila mimi ndio nimelazwa chini huku mitutu ya bundiki ya wanaume hawa wakiwa wamenielekezea mimi.
“Halooo Dany”
Sikuamini macho yangu nilipo muona baba Hawa akisimama pembeni yangu, huku mkononi mwake akiwa ameshika bastola tayari kwa kuniua.

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...