Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, October 6, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 91 na 92 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588   
ILIPOISHIA           
Nikatazama picha ya pili, nikaona askari mmoja akiwa amepigwa risasi ya kichwa, picha ya tatu ikanifanya ninyanyuke kwa haraka huku macho nimeyatoa.
Ili kuhakikisha ninacho kiona ni chenyewe na si utani, nikaikuza picha ya mama yangu anaye onekana kuchinjwa kikatilia sana jambo lililo nifanya nianze kutetemeka mwili mzima, huku nguvu za mwili nikihisi zinaanza kunishia. 

Nikajikaza hivyo hivyo kusogeza picha ya mbeleni, hapo napo nikamuona Diana mdogo wangu akiwa amachinjwa huku maziwa yake yakiwa yamekatwa jambo lililo nifanya nijikute nikiiachia simu ya mama Mariam ikaanguka chini, hata mimi mwenyewe siku sikumaliza hata sekunde tatu, nikajikuta nikianguka chini na kutulia tuli.

ENDELEA           
Kwa mbali nikamuona Mariam akimuachia mama yake na kuniwahi mimi hapa chini nilipo anguka.
“Mama umefanya nini, kumuonyesha Dany hizi picha lakini?”
Niliisikia sauti ya Mariam ikilalama kwa mbali sana.
“Mshike huko tumuweka hapa kwenye sofa amezimia”
Nikahisi nikinyanyuliwa, nikawekwa kwenye sofa.
“Mama kalete maji ya baridi”    
 
Vitendo vyote wanavyo vifanya Mariam na mama yake ninavisikia kwa mbali sana, japo mwili na viungo vyangu havina nguvu ya kuweza kukabiliana na hii hali. Maji ya baridi niliyo mwagiwa kichwani mwangu, yakanifanya nikurupuke katika hali ya kusizi. Nikasimama wima huku macho nikiwa nimeyatoa, mimi mwenyewe nikakiona kifua changu jinsi kinavyo panda na kushuka kutokana na mapigo yangu ya moyo kunienda kasi sana.
“Dany”
Mariam aliniita huku akiwa ameninyooshea mkono wa kulia, nikamtazama kwa umakini sana, akausogeza mkono wake na kunishika bega la upande wangu wa kulia.
“Dany tulia, tulia”
Mariam alizungumza huku akizidi kunisogelea. Nikajaribu kuzungumza kitu, ila kinywa changu hakikuweza kunyanyuka kabisa, taratibu Mariam akanirudisha na kunikalisha kwenye sofa walilo kuwa wamenilaza muda mchache ulio pita. Nikaendelea kufikiria nilicho kiona ni sahihi au nilikuwa ninaota. Nikamnyooshea mama Mariam mkono, jambo lililo mfanya kubaki amenitumbulia macho.
 
“Simu”
Nilizungumza kwa ufupi, mama Mariam akageuka nyuma na kuitazama simu  yake iliyo anguka katika sehemu ambayo nilianguka. Akapiga hatua taratibu na kuifwata hadi sehemu  nilipo aungukia, akaichukua na kurudi nayo, akanikabidhi pasipo Mariam kuzungumza chochote. Kwa bahati mbaya kioo cha simu hii kimepasuka na hakifanyi kazi ya aina yoyote.
 
Nakaanza kuikagua simu hii, nikaifungua nyuma na kutoa chipu ya kuhifadhia kumbukumbu(memory card). Nakaito chipu iliyopo kwenye simu yangu na kuiweka chipu hii ya mama Mariam, haikuchukua sekunde nyingi, ikawa imekubali kufanya kazi kwenye simu yangu, kwa haraka nikaingia kwenye upande wa picha, nikaanza kuziona picha za mwanzo nilizo ziona. Nikaiona picha ya mama yangu, machozi ya hasira taratibu yakaanza kunimwagika usoni mwangu, nikatazama picha ya Diana, nikapeleka mbele, hapo nikaona picha ya Asma, pamoja na mwanagu nao wakiwa wamechinjwa kikatili sana.
 
Nilihisi kama moyo unakwenda kupasuka kwa hasira na maumivu ninayo isikia, mwili mzima ukaanza kusisimka huku meno yakikaza, jasho jingi likaendelea kunimwagika.
“Dany”    
 
Mariam aliniita kwa sauti ya upole sana, ila jicho nililo mtazama nalo, hakuweza kuendelea kuzungumza tena akaka kimya, ukimya ukatawala ndani ya seble hii. Mlio wa simu yangu, ukanistua na kunifanya nitazame anaye nipigia. Jina la hawa lililo jitokeza juu ya simu yangu, likanifanya nibaki nikiwa nimelikodolea macho tuu, kwa hasira niliyo kuwa nayo sikuweza kuzungumza kitu cha ina yoyote.
Taratibu nikanyanyuka, kwenye sofa nililo kalia, nikaanza kutembea kueleka nje. Mariam kwa haraka akwahi mlangoni na kunizuia kwa kuichanua mikono yake, ili nisipite.
“Dany nakuomba unisikilize tafadhali”
“PISHA NJIA”
Hata sauti yangu imebadilika, inatoka ikiwa imekusanya besi kubwa, na mikwaruzo ambayo tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kuisikia.
 
“Dany siwezi kukupisha pasipo wewe kunisikiliza katika hili ninalo kwenda kulizungumza”
Mariam alizungumza kwa msisitizo sana, nikaendelea kumtazama kwa hasira, kwani anacho kifanya ninaona kama nikipingamizi kwangu.
“Dany natambua kwamba kifo cha familia yako ni lazima kinakuuma sana, ila tukae chini tuzungumze tufahamu kwamba tunaanzia wapi katika hili”
Nikaupeleka kwa nguvu mkono wangu wa kulia, ukaushika mkono wa Mariam, nikamvuta pembeni na akaanguka chini. Nikapiga hatua mbili mbele, Mariam akaniwahi kunidaka mguu  wa kulia akiendelea kunizuia kuondoka. 

Nikageuka nyuma na kumtazama kwa hasira sana, Mama Mariam aliye simama pembeni akishuhudia kinacho endelea, usoni mwake anamwagikwa na machozi mengi asijue anafanya kitu gani.
“Dany unajua ni jinsi gani ninayo kupenda, unajua ni jinsi gani ninavyo umia kukuona katika hiyo hali, tafadhali Dany, nakuomba usiondoke”
Mariam alizungumza huku machozi yakimwagika sana. Sikuhitaji kusikiliza porojo zake, nikauvuta mguu wangu kwa nguvu na ukaponyoka kwenye miguu yake. Kwa haraka nikatoka ndani kwao. 

Moja kwa moja nikaelekea nilipo lisimamisha gari langu, nikafungua na kuingia ndani, bastola yangu niloyo kuwa nimeiacha chini ya siti ta hili gari nikaiweka magazine na kuikoki vizuri, simu yangu nikaiweka kwenye siti ya pembeni, nikawasha gari kwa haraka na kuanza kulirudisha nyuma ili kuliweka sawa kueleka getini. Mariam akatoka ndani na kusimama mbele ya gari langu huku akinitazama machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. 
 
Mama yake naye akatoka akiwa analia, akasimama barazani, akitazama kinacho endelea. Nikamtazama Mariam machoni mwake, huruma ya kibinadamu tayari imesha niondoka moyoni mwangu, nikaichukua bastola yangu na kushuka kwenye gari, nikamnyooshea Marima, ambaye bado amesimama mbele ya gari langu.
“Dany niue tuu, naomba nafasi unisikilize”
Mariam alizungumza huku akinitazama, nikaendelea kumsogelea huku nikiwa nimemnyooshea bastola, moyoni mwangu nikaanza kusikia sauti mbili zikishindana, moja ikiniomba nimsikilize Mariam anacho hitaji kuzungumza huku nyingine ikiniomba nimpige risasi na nitaenda kujua mbele ya safari nani ni muhusika wa kifo cha familia yangu.
 
“Sihitaji kukuua Mariam, kwa mana sina chuki na wewe, japo nilishatumwa kukuua wewe na bosi wangu, ila sijafanya hivyo, tafadhali ninakuomba unipishe kabla sijafanya hivyo”
Niliendelea kuzungumza kwa sauti ya kukoroma, walinzi wa Mariam kwa haraka wakafika katika eneo tulilo simama huku wakiwa wameninyooshea bunduki.
“Dany ni vyema ukaniua, ni vyema nikafaa mimi. Kwa nini unashindwa kunisikiliza, kwa nini unashindwa kuheshimu ombi langu. Unajua nani ni muuaji wa familia yako”
Mariam alizungumza kwa sauti ya juu iliyo jaa ukali na uchungu ndani yake. 
 
“Nani ni muuaji? Livna, K2 au?”
Nilizidi kumuuliza Mariam kwa ukali zaidi, akaka kimya, baada ya kuona anaendelea kunipotezea muda, nikarudi kwenye gari langu, nikaingia ndani na kufunga. Nikakanyaga mafuta na breki, jambo lililofanya tairi za gari langu kuanza kuserereka kwa kasi sana. Mlizi mmoja alipo ona gari linaaza kusogea akamuwahi kumrukia bosi wake na kumsogeza pembeni nikapita kwa spidi sehemu alipo kuwa amesimama Mariam. 

Kasi yangu ikaishia getini baada ya kuoga geti limefungwa, kwa haraka nikashuka kwenye gari, nikalifungua geti nikarudi kwenye gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi.
Kutokana si mwenyeji katika nchi hii ya Somalia, akili yangu kwa haraka ikanituma kutafuta ramani kupitia hii simu, ambayo itanipa maelekezo ya kuweza kufika Tanzania kwa kutumia gari. 

Nikasimamisha gari pembeni ya barabara umbali mrefu sana kutoka sehemu ilipo nyuma ya Maria. Haikuchukua muda sana kuweza kuiunganisha huduma ya GPRS, iliyo anza kunielekeza kwa mshale maalumu, kuanzia sehemu nilipo na sehemu ninayo hitaji kuelekea. Masaa niliyo yayo hadi kufika Tanzania ni masaa thelathini na tano sawa na siku mbili na masaa kumi na moja kwa mwendo  wa gari. Kwani kuanzia hapa nilipo hadi kufika Tanzania, nikipitia nchi ya Kenya itachukua kilomita elfu mbili mianne na nane.
 
Cha kumshukuru Mungu pesa zote alizo nipa Hawa ninazo, na kiasi nilicho nacho kinaweza kunifikisha Tanzania, katika siku hizi mbili. Mafuta niliyo nayo ni nusu tenki, katika kuendesha kwangu muda mwingi nikawa nitazama tazama kama ninaweza kupata sheli ya kujaza mafuta. Kwa bahati nzuri nikafanikiwa kupata sheli, taratibu nikasimama kwenye moja ya mashine ya kujazia mafuta. Nikashuka, huku nikiwa na kiasi cha kutosha cha pesa kwa maana katika jengo la hii sheli kuna Supermakert ya kununulia vitu mbali mbali.
“Lita ngapi muheshimiwa?”  
  
Kijana wa kiume wa kisomali aliniuliza huku akiwa ameshika bomba la kujazia mafuta.
“Hadi tanki ijae”
“Sawa”
Akaanza kujaza mafuta, nikaelekea ndani ya suoer makert. Nikaanza kuchukua vitu vya kula njiani pamoja na maji mengi ya kutosha. Nilipo hakikisha kwamba vitu nilivyo vichukua vinanitosheleza, nikalipia, wakaniwekea vitu vyangu kwenye mifuko mkubwa na kurudi navyo kwenye gari. Nikamkuta kijana huyu ambaye ni miongoni wa wahudumu kwenye hii sheli, akiendelea kujaza mafuta kwenye gari langu.
“Dogo bado?”
“Bado kidogo mkuu”
“Muna uaza madungu”
“Yaliyo na mafuta au matupu?”
“Yaliyo na mafuta”
“Hayo yametuishia, kama vipi nikuuzie dumu tupu, kisha nikujazie mafuta”
 
“Sawa hakuna shida katika hilo”
Dogo akamaliza kuweka mafuta katika gari langu, akafungu vizuri mfuniko wa tanki la mafuta yangu, nikahakikisha amekkaza vizuri mfuniko huo, nilipo jiridhisha, nikasimama pembei ya gari langu nikimsubiria kijana huyu kurudi. Nikaisikia simu yangu ikiita ndani ya gari langu, jambo lililo nifanya nifungue mlango na kuichukua simu. Nikakuta ni Hawa anapiga, nikaipokea na  kuiweka simu sikioni.
“Dany ni kitu gani ambacho unakifanya?”
“Kivipi?”
“Umepoteza mawasiliano, huku sikuoni. Tafahadhali rudisha hiyo chipu kwenye simu”
Hawa alizungumza kwa ukali sana, nikakitazama kioo cha simu kisha nikairudisha sikioni mwangu.
“Nina kazi muhimu ambayo ninahitaji kuifanya ukiachilia mbali na kazi yako ambayo ulinipatia”
“WHAT………..!! Wewe ndio wa kunijibu mimi hivyo kumbuka mimi ni mkuu wako”
“Sijakuvunjia heshima, nawala sihitaji nikivunjie heshima, ila hutambui ni kitu gani kinacho endelea katika maisha yangu, hujui maisha yangu ya nyuma Hawa. Hii ni nafasi ya mimi kufanya kile ambacho kilikuwa nyuma ya maisha yangu”
“Bosi huruhusiwi kuzungumza na simu katika eneo hili la sheli”
 
Kijana anaye nihudumia aliniambia, jambo lililo nifanya nikate simu na kuitupia ndani ya gari, huku nikiwa nimejawa na hasira mara dufu.
“Bosi wewe ni Mtanzania nini?”
“Kwa nini unaniuliza hivyo?”
“Watanzani wanajulikana, hushangani kwa nini nilikuongelesha Kiswahili?”
“Ok kwa hiyo?”
“Ahaa hapana, ila mimi mwenyewe ninapafahamu Tanzania, kuna kaka zangu, wapo maeneo ya Dar es Salaam maeneo ya Kariakoo wana maduka yao huko”
“Dogo niwekee mafuta, sipendi blaaa blaaaa nyingi”
Nilizungumza kwa ukali, hadi kijana wa watu akapoteza tabasamu usoni mwake. Akanijazia dungu langu mafuta ya kutosha, kisha nikafungua buti ya gari, akaliweka dungu la mafuta na kulifunga buti la gari langu.
 
“Sina pesa ya kisomali, kama vipi ninakupatia Dola. Niambie itagarimu dola ngapi?”
“Ahaahaa…..ahaa dola kama mia nne”
Nikampatia noti za dola mia mia zikiwa nne, kisha nikaingia kwenye gari na kuufunga mlango kwa nguvu.
“Kaka uendeshe gari kwa umakini, hasira sio nzuri”
“Nenda kamuambie baba yako”
Nilimjibu kijana wa watu vibaya huku nikisindikiza na msunyo  mkali, kisha nikapandisha kioo cha gari langu na kuondoka katika eneo la sheli. Nikajifunga mkanda wa siti na kuendelea kuendesha gari langu kwa kasi huku nikifwatisha ramani ya simu inayo niongoza. Simu yangu ikaita tena, nikaichukua, sehemu nilipo iweka, nikaitazama kwa muda kisha nikapokea.
 
“Ndio”
“Dany hujui unajiingiza kwenye matatizo ya aina gani, hujui majibu yako ni jinsi gani yanavyo mkasirisha baba, tena anakusikia hapa ninavyo zungumza na wewe, kwa nini Dany unafanya hivyo lakini”
“Hawa, nimeishi katika mikono ya baba yako na wewe kwa kipindi kirefu sasa, ila hakuna hata mmoja wenu aliye weza kuniuliza maisha yangu ya kiundani sana, si wewe wala si baba. Nina wapenda tena sana, kazi ambayo baba na wewe mumenipatia imezalisha kazi nyingine. Kazi ambayo hata kama ungekuwa ni wewe usinge weza kuiacha kuifanya. Ni kazi ambayo imegarimu maisha yangu, ni kazi ambayo imeupasua moyo wangu, hakuna siku hata moja ambayo Hawa umenisikia mimi nikizungumza katika hali na sauti kama hii.”
 
Nikanyamaza kidogo huku nikijipangusa machozi, kwa maana maneno niliyo yazungumza yananitoa machozi ya uchungu.
“Sikuwahi kukuvunjia heshima, nimekuwa mtiifu  kwa kila mtu ndani ya hiyo ngome, nimekuwa nikijitahidi kwa kila jambo ambalo ninalifanya ninalifanya kwa juhudi na moyo  mmoja, kwa nini leo hii nimekuwa hivi. Kwa nini Hawa unashindwa kuniuliza kwa umakini zaidi eheee?”
Niliendelea kuzungumza huku nikilia, kasi ninayo liendesha gari langu, huku nimeshika mskani kwa mkono mmoja, inaweza kunihatarishia maisha yangu muda na wakati wowote, ila silijali hili.
 
“Dany mwanangu kuna kitu gani kimetokea”
Nilisikia sauti ya baba Hawa, hapa ndipo nikaamini kwamba kila ninacho kizungumza mzee ananisikia.
“Baba, mimi nilikuwa na familia. Ilikuwa nchinia Tanzania, mama, dada yangu, mke wangu pamoja na mwanagu mdogo wa kike. Ila hadi muda huu ninavyo zungumza, sipo nao tena. Wameuliwa kikatili, wamechijwa kikatili, sababu sijui ni nini. Ni vyema wangeniua mimi, ila si familia yangu, nimepoteza watu ambao ni muhimu sana kwenye maisha yangu”
Nikamsikia mzee akishusha pumzi, ukimya wa sekunde kadhaa ukatawala kati yetu.
“Wewe umejuaje Dany?”
“Ngoja nikutumie picha, nilifahamu hilo swala kutoka kwa mtu ambaye muliniagiza mimi kuweza kumuu.”
“Tutumie kwenye hii simu ya Hawa”
“Sawa mzee”
 
Nikakata simu, huku nikiwa ninaendesha gari, nikaanza kumtumia picha moja baada ya nyingine kupitia mtandao wa Whatsapp. Picha zote zikafunguliwa katika muda huo huo ambao nimezituma.
Nikaendelea kuendesha gari kwa mwendo wa kasi huku nikijitahidi kwenda na muda kwa mana ninahitaji usiku unikute nikiwa nipo kwenye mpaka kati ya Kenya na Somalia, naamini hapo nikifika usiku ninaweza kuhonga ma askari wa mipakani na itakuwa ni rahisi kwa mimi kuweza kupita hilo eneo kiurahisi sana. Simu ikaita tena, nikaipokea na kuiweka sikioni.
“Dany rudi kambini, kama ni kazi hii itafanywa na vijana maalumu”
Mzee alizungumza jambo lililo nishangaza sana akilini mwangu.
 
“Unasema?”
“Umenisikia, ninatoa amri kama mkuu wako wa kambi, na si baba tena. Rudi kambini kazi hii nitawakabdhi vijana”
“Kwa nini uwakabidhi vijana na si mimi, ninaiweza kuifanya kazi hii peke yangu. Na hakuna ambaye atanizuia, si wewe wala si mwanao. Ninakwenda kuifanya hii kazi mwenyewe”
“NITAHAKIKISHA HUTOKI NJE YA SOMALIA, NA NITAHAKIKISHA UNALETWA MBELE YANGU UKIWA HAI AU UMEKUFA, MWANA HARAMU MKUBWA WEWEEEE”
“Hahahaaa, mimi ni mwana haramu tena mkubwa sana, endapo nitajua umehusika na wewe katika hili. KICHWA CHAKO, nitakikata kwa mikono yangu mimi mwenyewe, na mbaya zaidi. Mimi ni mpelelezi niliye fuzu mafunzo mbali mbali tofauti na hayo unayo wapatia NGEDERE wako. Na ninakuhakikishia kwamba hiyo NGOME yako nitakuja kuifumua chini juu, juu chini. PUMBAVUUU”
Nikampiga mkwara mmoja ambao ninaamini ni mtakatifu kwa baba Hawa, kisha nikakata simu na kuongeza mwendo kasi wa gari langu, nilio kuwa nimeupunguza kidogo ili kuzungumza na huyu mzee mjinga.
                                                                           
AISIIIII……….U KILL ME 92                                                                                                 


Naamini kila ninapo katiza watu watakuwa wananishangaa kwa mwendo kasi wa gari langu ninalo liendesha. Nikaendelea kujitahidi kuhakikisha kwamba ninatoka ndani ya nchi hii ya Somalia haraka iwezekanavyo kwa maana hai ya hatari baba Hawa amesha itangaza kwangu mimi. Simu yangu ikaita, nikaitazama na kuona ni namba ngeni inaingia, kwa mara ya kwanza nikasita kuipokea, ikaita hadi ikakata. Simu ikaita tena, ikanibidi kuipokea ili kufahamu ni nani anaye nipigia.
 
“Dany, Dany please msikilize baba, usiende kinyume na sheria yake”
Niliisikia  sauti ya Hawa akizungumza kwa majonzi sana.
“Hawa naamini unafahamu uchungu wa familia, kwa mfano angeuwawa baba yako kipenzi wewe ungechukua maamuzi gani?”
Swali langu likamfanya Hawa kukaa kimya kwa takribani dakika moja.
“Dany upo  wapi?”   
“Sio jibu la swali nililo kuuliza?”
“Nimekuuliza kwa maana nahitaji kukusaidia, natambua ukiwa katika hali hiyo ya asira huto weza kufanya jambo lolote mwisho wa siku utaishia pabaya”
“Sijalishi hilo, nipo tayari kufa, na wala sihitaji msaafa wako Hawa. Umeyaokoa maisha yangu, asante sana kwa hilo”
“Dany tafadhali niambie ni wapi ulipo niweze kukusaidia?”
“Wewe na baba yako ni kitu kimoja, kama kweli unahitaji kunisaidia mimi subiri nikifika nchini Tanzania, ndio nitahitaji msaada wako”
 
“Sawa, ila kila mpango ambao  baba yangu ataupanga juu yako nitakueleza”
“Nitashukuru kama ni kweli”
“Nafanya haya yote kwa ajili ya upendo wangu kwako, tafadhali Dany sihitaji kukuona unapoteza maisha yako”
Nikashusha pumzi nzito huku nikiyafikiria maneno ya Hawa kichwani mwangu.
“Dany”
“Naam, ninakusikia”
“Fikiria hilo, nipo tayari kupoteza uaminifu wangu kwa baba yangu, kwa ajili yako. Tafadhali usife Dany wangu ninakupenda”
Niliendelea kumsikia Hawa anaye zungumza huku akilia kwa uchungu.
“Sawa nitaishi”
“Safari njema”
“Ok”
“Alafu Dany, unitafute kwenye hii namba, ile nyingine anayo baba. Pia usiiweke hiyo memory card uliyo itoa kwenye simu”
“Sawa
 
Nikakata simu, nikairudisha katika sehemu ambayo nimeitoa. Safari ikazidi kusonga mbele huku baadhi ya maeneo ambayo ninahisi kuna askari wa usalama wa barabarani, ninapunguza mwendo. Hadi inafika majira ya saa sita kasoro usiku nikawa nimefika eneo la Afmadow, mpakani mwa Kenya na Somalia. Bastola pamoja na magazine nikazivisha katika sehemu ambayo si rahisi kwa askri wakaguzi kuweza kuziona. Nikaandaa noti zangu mbili za dola mia mia. Taratibu nikaendesha gari langu hadi kwenye geti la kuingilia nchini Kenya.
 
“Habari yako mkuu”
Nilianza kujipendekeza kwa askari ambaye amefika karibu yangu, akiwa na bunduki mkononi mwake.
“Salama, washa taa ya gari lako”
Nikatii amri ya kuwasha taa ya ndani ya gari huku nikiwa na tabasamu pana usoni mwangu.
“Unaelekea wapi usiku huu?”
“Ahaa ninarudi nyumbani hapo Ijara, nimetoka Somalia mara moja”
Ilinibidi kudanganya kwani mji unao fwata kutoka nikisema ninakwenda mbali na hapo, wataanza kuniletea longolongo jambo ambalo sihitaji linitokee kwa muda huu.
“Naomba kipande chako”
 
“Ehee!!”
Niliuliza kwa mshangao kwa maana kingereza cha kikenya na kitanzania vina toafauti kubwa sana.
“Unashangaa ina maana hutambui kipande ni nini?”
“Ok ok muheshimiwa, kidogo nilipitiwa”
Nilizungumza huku nikianza kujipapasa mfukoni mwangu. Galfa askari huyu akaanguka chini, huku milio ya bunduki ikisikika ikitokea nyuma ya gari langu. Kwa kupitia kioo cha pembeni nikaona gari mbili zikija kwa mwendo  kasi sana. Kwa haraka sana nikafungu kioo cha  gari langu, huku nikianza kuliondoa eneo hili kwa kasi ya ajambu nilikilifwata geti lililopo barabarani. Askari waliopo kwenye hui mpaka wakaanza kushambulia watu ambao ninatambua fika wamegizwa na baba Hawa. 
 
Nikaligonnga getu na kuliangusha chini, nikaendelea kuongeza mwendo kasi wa gari langu, sikujali kama limebonyea seheu ya mbele.
Watu wa baba Hawa wakazidi kuniandama, kadri ninavyo watazama kupitia kioo changu cha pembeni, ndivyo jinsi ninavyo waona wanavyo zidi kuongezeka. Si magari mawili kama nilivyo yaona mwanzo, ila hadi sasa ninaona gari zisizo pungua saba, na zote zinakuja kwa mwendo wa kasi sana. Nikaichomoa bastola yangu, sehemu nilipo ificha, nikaweka magazine moja na kuanza kujibu mashabulizi ya wanajeshi wa Al-Shabab.
 
Hali haikuwa nzuri kabisa kwa upande wangu, kwani kadri ninavyo zidi kuongeza mwendo kasi wa gari langu, ndiovyo jinsi wana jeshi hawa wananikaribia, hadi ikafikia hatua nikaanza kukata tama. Nikaitazama simu yangu pembeni, mtando haupo kabisa jambo lililo ifanya hadi ramani ambayo nilikuwa ninaitegemea, kupotea kabisa. Gari sasa za wanajeshi wezangu, zikanisogelea pembeni hadi zikaanza kuwa karibu na mimi. Wakaanza kuligonga gari langu kwa kutumia ubavu wa gari zao. Sikuhitaji kuwa mnyonge, na mimi nikaanza kuendesha kwa kuyagonga magari yao kwa kutumia ubavu wa gari langu, japo yanabonyea ila dawa ya ubishi ni ubishi.

Kitu kilicho zidi kunishangaza kwa hawa wezangu, kitendo cha wao kunikaribia hakuna hata mmoja aliye thubutu kufyatua risasi kwangu, hapo ndipo nikagundua kwamba wameagizwa wanipeleke nikiwa hai. Nikatumia nafasi hii kwa kuwa jeuri zaidi, nilicho kifanya ni kuanza kupunguza mwendo kasi wa gari langu huku nikitazama gari hizi mbili zilizopo pembeni yangu kwa maana wameniweka kati kati na nyuma kuna magari mengie.
 
Nilipo waona nao wamepunguza mwendo kasi, nikaongeza mwendo kasi, nikawafanya nao kuongeza mwendo kasi, nilipo fika mbele kidogo nikafunga breki za gafla huku nikiwa nimekaza meno, mzinga ulio lia nyuma ya gari langu, ninaujua mimi na Mungu wangu, kwani gari mbili zilijikuta zikinivaa kwa nyuma na kulifanya gari langu kuhama kabisa kutoka barabarani, japo niinajitahidi kufunga mbreki, ila likaendelea kuserereka kwa maana limepoteza muelekeo katika barabara. Gari langu likaserereka hadi kwenye mti mkubwa ulipo karibu na barabara, likabamiza kwa nguvu na kutulia. Nikaanza kujitoa kwenye ftuza kubwa lililo tokeza kwenye mskani, kipindi nilipo funga breki za gafla. Japo nina maumivu sehemu mbali mbali katika mwili wangu, nikajitahidi kutola hivyo hivyo kwenye gari huku nikimwahikwa na damu za pua.
 
Nikajaribu kusimama, ila nikajikuta nikiyumba yumba kwa kizungu zungu kikali ambacho kimenitawala. Nikaanguka chini, huku nikiwaona wanajeshi  wengine wakinisogelea kwa haraka huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Nikajaribu kuinyanyua bastola yangu hata mikono haikuwa na nguvu kabisa. Kitu kizito kikatua kichwani kwangu, na kusababisha giza kali kutawala kwenye macho yangu.
                                                                                                                    ***
“Mfungeni vizuri”   
Niliisikia sauti ya baba Hawa kwa mbali sana, taratibu nikajitahidi kuyafumbua macho yangu, ila sikuona vizuri. Nikaanza kusikia maumivu ya mikono pamoja na miguu yangu katika sehemu ya viungio.
“Kaza na huko”
Niliendelea kuisikia sauti ya baba Hawa. Nikamwagiwa maji ya baridi usoni mwangu. Kidogo nikaanza kumuona baba Hawa pamoja na wanajeshi wengine wanne walio valia mabushori meusi yaliyo ficha sura zao. Nikaanza kujitazama, nikajikuta nikiwa sina nguo hata moja, huku mwili wangu unameremeta sana kwa mafuta ya kupikia niliyo mwagiwa mwilini mwangu.
 
“Mwanaharamu mkubwa wewe, uliye nipumbaza kutokana na meneno ya mwangu, nikakuamini. Nikakupenda na nikakujali kumbe ni mpelelezi, na siku zote huwa nachukia wapelekezi”
Baba Hawa alizungumza kwa hasira kali hadi mate kwenye mdogo wake yakawa yanamwagika mdomoni mwake. Woga wote ambao siku zote ninamuogopa huyu mzee, nikashangaa ukiwa unanitoweka moyoni mwangu. Nikajikuta nikicheka kwa dharau, baba Hawa akanitandika ngumi nzito ya tumoni iliyo nifanya nigugumie maumivu ya ndani kwa ndani.
 
“Ahaaaa haaaaa!!”
Niliendelea kucheka, huku nikijikaza tumbo langu.
“Nilikuambia huto toka ndani ya hii nchi, ukaniletea dharau si ndio?”
“Hivi wewe ni binadamu wa aina gani, wewe ni mtu wa aina gani usiye tambua uchungu wa familia. Eheheee……??”
“Ohooo siku zote ninapo agiza kazi yangu, sihitaji mtu kwenda kinyume na kile ninacho kipanga, ila wewe ukakiuka sheria zangu. Katika hilo sihitaji kukusamehe”
“Niueeeeeee, siogopi kufa, kwa maana mimi nimesha kufaa”
“Ohooo safi?”
Baba hawa akachukua fimbo aina ya mjeledi. Akasimama mita chache kutoka sehemu waliyo nifunga, pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote akaanza kunichapa kwa nguvu. Nikaendelea kugugumia kwa maumivu makali sana, ila baba Hawa akaendelea kupitandika kwa mjeledi huu ambao akivuta basi anaondoka na nyama za mwili wangu.
“Wewe ulikuja nikupeleleza au?”
Sikumjibu chochote baba Hawa zaidi ya kumtemea mate yaliyo tua kwenye sura yake. Akaendelea kunitandika mijeledi, hadi mwenyewe akachoka kabisa.
“Hakikisheni munaimarisha ulinzi hapa na asiingie mtu yoyote”
“Sawa mkuu”
“Na musimfungue na wala asipate chakula cha aina yoyote wala maji”
“Sawa mkuu”
Baba Hawa akatoka katika chumba hichi. Nikatamani malaika mtoa roho, ashuke na kuichukua roho yangu, kwa maana hadi hapa nilipo fikia nimepabaya sana, sidhani kama ninaweza kurudi katika mapambano dhihi ya maadui zangu. Mwili wangu umejaa majeraha ambayo, yatachukua muda mwingi sana kupona. Nikaendelea kukaa huku miguu na mikono ikiwa imechanuliwa na kamba zake zimefungwa kwenye engo tofuati tofauti katika hichi chumba.
Hapakuwa na mwajeshi hata mmoja ambaye alinigeuzia sura yake kwa kunitazama, kila mmoja alibaki akiwa amesimama upande wake.
 
“Heii”
Nilizungumza kwa sauti ya kukoroma, nikiwa na lengo la kuwaita wanajeshi hawa walio jikausha huku wakiwa wamesimama kama milingoti.
“Hei mimi si mwenzenu, mutaishi kwa kufwata amri hadi lini?”
Niliendelea kuzungumza kwa kujikaza sana, huku damu zikiwa zinanimwagika mdomoni mwangu.
“Ni umasikini au nini, kukubali kuona kijama mwenze….nu nikifa kwa mateso kisa amri ya huyu mzee. NI kipi anacho tupa zaidi ya chukula, maladhi na nguo. Tumekuwa watu wakujitolea muhanga kwa ajili ya huyu mseng** mmoja. Ni moja wa kubadilisha mifuno ya akili zetu”
Nilizungumza maneno ya kuwahamasisha hawa wezangu wanao nilinda, ila sikuona dalili yoyote ya hata mmoja wao kunielewa kwa kile ninacho kizungumza.
Mlango ukafunguliwa akaingia baba hawa akiwa amebadilisha mavazi yake. 
 
“Za asubuhi wewe bweha”
Baba hawa alizungumza huku akinisogelea sehemu nilipo. Nikamtazama kwa macho ya dharau huku nikimpandisha na kumshusha.
“Kanileteeni maji, pilipili ya unga na chumvi”
“Sawa mkuu”
Mwanajeshi mmoja akatoka, hakuchukua muda mwingi sana akarejea akiwa na ndoo pamoja na mfuko mweusi. Akakabidhi baba Hawa mfuko mweusi huku ndoo ya maji akiiweka mbele ya baba Hawa.
Mzee huyu akaanza kuchanganya pilipili pamoja na chumvi kisha akaviweka kwenye ndoo hii yenye maji yaliyo jaa. Alipo rishika akaanza kunimwagia maji hayo mwili mwangu.
Hata kama mtu ni jasiri kiasi gani ila kwa  maumivu ninayo yapata kwenye majeraha yangu, nikatamani ardhi ipasuke niingine na inimeze.
 
“Kidume huwa hapigi kelele iweje leo unapiga kelele”
“KU** WEWEEE”
Nilimtukana baba Hawa, akaiweka ndoo chini kwa hasika. Akatembea hadi kwenye meza iliyomo ndani ya hichi chumba huku imejaa makorokocho, akachukua mkasi mrefu na wenye makali, akanisogelea, kisha akamshika jogoo wangu kwa mkono wake wa kushoto, akaupitisha mkasi katikati ya jogoo wangu na kuanza kumkata taratibu, jambo lililo nifanya niangue kilio kikali sana ambacho tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kulia kilo cha aina hiyo.

ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )