Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 16, 2018

Alichokisema Haji Manara Baada Ya Kuachiwa Kwa Dhamana Leo

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ametoa ujumbe wake wa kwanza tangu aachiwe huru na polisi baada ya kuwa chini ya ulinzi kwa muda akihojiwa kuhusu kutekwa kwa mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'Mo'.
 
Manara ambaye alikuwa miongoni mwa watu 26 wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwaajili ya mahojiano, ameachiwa leo Oktoba 16, 2018. 

Baada ya kuachiwa Manara amesema watu waendelee kumuombea Mo Dewji aweze kupatikana.

''Kila jambo huja na sababu yake, na mitihani ya kilimwengu tumeumbiwa sisi binaadamu, naendelea kuwasihi tuviache vyombo vinavyohusika vitimize wajibu wao, kubwa tuendeleze dua na sala kwaajili ya kiongozi wetu InshaAllah'', ameandika Manara katika ukurasa wake wa Instagram.

Mohammed Dewji ambaye ni mwanahisa mkuu wa klabu ya Simba akimiliki asilimia 49 ya hisa, alitekwa alfajiri ya Oktoba 11, 2018 maeneo ya Masaki jijini Dar es salaam.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )