Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 4, 2018

Alikiba Kataja Sababu za Kufuta Wimbo Wake YouTube

adv1
Msanii wa muziki Bongo, Alikiba  ambaye siku ya jana alikumbana na lawama na kejeli za mashabiki wake mitandaoni baada ya kufuta wimbo wake mpya wa ‘HELA’ aliouachia usiku kupitia mtandao wa YouTube kisha kuufuta asubuhi, amefunguka sababu za kufuta wimbo huo.

Alikiba ametaja sababu kubwa ya kufuta wimbo huo ni siku ambayo aliachia, kwani haikuwa siku ambayo huitumia kuachia nyimbo mpya.

“Siku yenyewe haikuwa siku yangu ambayo napenda ku-release nyimbo, ilikuwa siku ya Jumanne, so tukamwambia jamaa autoe, inatakiwa siku kama ya leo Alhamisi, ndiyo maana ulikuta umetoka kwenye YouTube, ila sasa hivi ukiingia utaikuta”, amesema Alikiba.

Alikiba amelazimika kutoa maelezo hayo baada ya kushambuliwa na mashabiki kuwa ameutoa wimbo huo kwa kuwa ni mbaya huku wengine wakidai amerudia wimbo wake wa zamani.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )