Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 5, 2018

Basata yampongeza Diamond Kwa Kutoa Msaada Tandale

Baraza la Taifa la Sanaa (Basata) limempongeza msanii Diamond kwa kuwasaidia watu wa eneo lake la Tandale jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 5, 2018 na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza katika sherehe za kuzaliwa msanii huyo zinazofanyika viwanja vya Maguniani Tandale.

Amesema ni nadra kwa watu waliofanikiwa kukumbuka walikotoka kitendo cha kuwasaidia wana Tandale kimeonyesha utofauti wake.

Katibu Mtendaji huyo ametoa pongezi hizo za aina yake kwani alipopanda jukwaani alianza kwa kuchana mistari ya kumpongeza Diamond.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )