Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, October 8, 2018

Basi la Arusha Express Lapinduka....Wanne Wapoteza Maisha

Takribani watu wanne wameripotiwa kufariki Dunia katika ajali iliyohusisha basi la abiria la 'Arusha Express' lililokuwa likisafiri kutoka jijini Arusha kueleka mkoani Dodoma kupinduka katika wilaya Babati mkoani Manyara.

Kwa mujibu Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga, ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi ambapo taarifa za awali licha ya vifo hivyo vinne mpaka sasa kuna majeruhi 11 na kati yao watano wako mahututi huku chanzo cha ajali kikiwa bado hakijajulikana.

"Nitatoa taarifa kamili nikiwa nimetulia, mpaka dakika hii vifo ni vinne watatu wamefariki eneo la tukio, na mmoja amefariki hospitali na majeruhi wapo 11 japo hatujajua chanzo cha ajali lakini ajali imetokea upande wenye kona kali na basi likalala upande wa kushoto''. Amesema Kamanda Agustino

Aidha Kamanda huyo amesema bado jeshi hilo linaendelea na shughuli za  kufuatilia majina ya wanaotajwa kupoteza maisha kwenye ajali hiyo ili waweze kutambuliwa na ndugu zao.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )