Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, October 5, 2018

Birthday ya DIAMOND: Nasaha Nzito ya Jacqueline Mengi Tandale

adv1
Aliyewahi kuwa Miss Tanzania Jacqueline Mengi ametoa somo kwa kinamama wanaohitaji mitaji kibiashara  kuthamini mitaji midogo ili kufikia mafanikio kibiashara.

Akizungumza leo Oktoba 5,2018 katika viwanja vya Maguniani Tandale jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kuzaliwa Diamond, Jacqueline amesema wanawake wanapaswa kuwa na malengo ili kufanikisha ndoto zao kibiashara.

“Hakuna kitu muhimu kama kuwa na malengo, mkipewa mtaji msije kufika nyumbani na kwenda kupika uji, hizo fedha za mtaji hamtakiwi kuzila msisahau kina baba watawaambia zileteni msitoe.”

“Nawategemea mtakaopata mitaji leo mwakani tukirudi mtakuwa watu wakubwa, vijana cha kwanza ni kujiamini kwamba mnaweza kama Diamond japokuwa anawazidi lakini kijana ukijitambua unaweza kufanya jambo jiamini kwani ndiyo njia ya mafanikio,” amesema Jacqueline ambaye ni mke wa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )