Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, October 1, 2018

Bodi Ya Nafaka Na Mazao Mchanganyiko Kiungo Cha Wakulima Nchini

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ili kuhakikisha kuwa Kilimo kinakua kwa asilimia 6 kwa mwaka kuendana na malengo ya Programu Kabambe ya Maendeleo ya Kilimo Barani Afrika (CAADP).

ASDP Awamu ya pili inatekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2027/28 imekijikita katika kuleta mageuzi ya  mtazamo uliopo wa kilimo cha kujikimu kufikia uendeshaji wa kilimo kwa mfumo wa kibiashara.

Aidha ASDP awamu ya pili imeweka kipaumbele kuendeleza mazao ya kilimo yakiwemo mazao makuu matano ya biashara (pamba, tumbaku, korosho, kahawa na chai) kwa kushirikisha wadau mbalimbali, hatu inayolenga kutimiza malengo ya Tanzania kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

Wakulima nchini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa miundombinu mizuri na umbali wa masoko, hivyo hukwaza wakulima kusafirisha mazao yao hadi mahali pa kuyauzia na wengi wao kujikuta wakiuza mazao yao kwa walanguzi na wasafirishaji kwa bei ya chini.

Mara nyingi wakulima hupunjwa kwa sababu ya kukosa taarifa sahihi za soko, au kutoelewa vipimo halali vya uzito na ujazo na wafanyabiashara wasio waaminifu hunufaika isivyo halali kwa kufanya udanganyifu katika vipimo.

Kutokana na hali hiyo, Serikali ilianzisha Bodi ya Mazao Mchanganyiko ili kujikita katika biashara ya mazao ya nafaka na mengine yasiyo na chombo cha usimamizi ili kumpa unafuu wa maisha mkulima.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19, Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba anasema kutokana na usimamizi imara wa Serikali kupitia Bodi za mazao, uzalishaji wa mazao mbalimbali umeendelea kuimarika hususani mazao ya asili ya biashara.

Anasema kuwa katika mwaka 2017/18 Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko imenunua tani 2,504.09 za mahindi kutoka kwa wakulima wa mikoa ya Iringa na Ruvuma yenye thamani ya Tsh Bilioni 1.25.

Dkt. Tizeba anasema hadi kufikia mwezi Desemba mwaka hadi kufikia mwezi Desemba 2017 Bodi imesagisha tani 146.5 ambapo zimepatikana tani 112.7 za unga wa mahindi na tani 33.8 za pumba, ambapo usagishaji unaendelea na mauzo yanaendelea katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Dar es Salaam na Mwanza.

Anaongeza kuwa katika kuongeza uwezo, Bodi imepokea mkopo wa Tsh Bil 3.66 kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kununua mashine yenye uwezo wa kusagisha tani 60 za mahindi kwa siku na mashine yenye uwezo wa kukamua tani 20 za mbegu za alizeti kwa siku zitakazofungwa katika eneo la Kizota mjini Dodoma.

“Aidha, Mashine hizo zitakapoanza kufanya kazi Bodi itaweza kununua tani 17,000 za mahindi na tani 6,000 za mbegu za alizeti kutoka kwa wakulima kwa mwaka na mzabuni wa kufunga mashine hizo kampuni ya UGUR ya Uturuki inatarajia kukamilisha ufungaji wa mashine kabla mwezi Julai, 2018” anasema Waziri Tizeba.

Dkt. Tizeba anasema katika mwaka 2018/19 Serikali itaendelea na uhamasishaji wa uanzishwaji wa kilimo cha mkataba na kibishara kwa zao la muhogo katika kanda za Mashariki na Kusini kwa kushirikisha Halmashauri za Wilaya ya Mikoa ya Lindi, Mtwara, Manyara, Singida na Morogoro.

Kwa mujibu wa Dkt. Tizeba anasema kilimo cha mkataba, Serikali itahamasisha wakulima kulinda mazao ya mikunde, bustani na mafuta kibiashara kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Ununuzi wa mazao ya wakulima kupitia Bodi ya Mazao utasaidia kuokoa uharibifu wa mazao mengi ya nafaka yanayokaridiwa kabla ya kuvunwa yakiwa shamba kutokana na tekonojia duni ya utunzaji na uhifadhi.

Kuandaliwa kwa mfumo wa ukusanyaji wa takwimu za mazao ya chakula na mazao yanayosindikwa viwandani, utasaidia kubaini wa mazao hayo upotevu katika mnyororo wa thamani na kutengeneza mikakati ya kuboresha viwanda, na hatimaye kutengeneza ajira na kipato.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...