Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, October 20, 2018

BREAKING: IGP Sirro Anaongea na Waandishi wa Habari Muda Kuhusiana na Tukio la Mo Dewji


18."Watekaji wale walikuwa wanataka fedha,  kutokana na hitaji lao hilo Mo Dewji alipowapa simu aongee na wazazi wake watekaji wale kwa kuogopa na kujua uimara wa Jeshi la Polisi wakaogopa na kuona njia pekee ya salama kwao ni kulitelekeza gari lao na kumwachia MO"IGP Simon Sirro


17."Niwashukuru polisi na vyombo vya usalama kwa kufanikisha hili, wakati mwingine haya matukio yatusaidie kutuunganisha, matukio haya yasitugawe, tuwe wamoja" IGP Simon Sirro.
 

16."Watu wetu wako kwenye hizo nchi, tunataka kuwaonyesha ukizoea Tanzania siyo mahali salama, kama walizoea kwenye nchi zao siyo hapa kwetu. Kuacha gari hii na silaha siyo mwisho wa upelelezi. Najua kuna Mtanzania mmoja, tuwapate tuzungumze nao lugha nzuri" IGP Sirro.

15."Baada ya MO Kupatikana Kwenye biashara hii lazima tuwaonyeshe kuwa hii ni Tanzania, lazima tuwapate, na tukiwapata watueleze walikuwa wanataka kufanya nuini. - IGP Sirro.


14."Tulipofika hapa Gymkana tukalikuta gari lilimteka Mohammed Dewji limetelekezwa tukaona tulizuie mtu asiingie kwanza tufanye upekuzi, tumekuta silaha ya kivita AK 47 moja na bastola tatu"IGP Sirro

13."Mtandao wote tulikuwa tunaujua, namba ya gari na nchi waliyotokea na kimsingi tulikuwa tunakwenda kuwakamata na kuwakamata kwangu kungekuwa kwa aina yake.Nitoe rai kwa wageni wanaodhani Tanzania ni sehemu ya kufanya uhalifu na wakabaki salama wajue wanajidanganya"IGP Simon Sirro

12."Fikiria Mohammed Dewji amekuja  kutekwa kwa silaha nne, bastola zilikuwa na risasi 16, na hii AK 47 ilikuwa na risasi 19, ni silaha nzito ya kivita, inaweza kupiga risasi 19 mfululizo"-IGP Sirro

11.''Kwa mujibu wa ripoti niliyopewa, watekaji walikuwa wanaongea Kiingereza na Kiswahili cha hovyo hovyo na mimi baada ya hapa nitaenda kumjulia hali Mo na kumuuliza zaidi'' - IGP Sirro

10.''Hili gari walitaka kujaribu kutaka kulichoma ili wapoteze ushahidi lakini nadhani walikuwa na hofu juu ya hilo hawakufanikiwa'' IGP Sirro 

9."Nyinyi ni mashahidi jana nimezungumzia hii press nikiwa na uhakika lakini kuna watu wachache ambao sijui nia yao ni nini?, tukijaribu kufanya wao wanatufundisha" IGP Sirro

8.''Sikutaka kusema, lakini watu wetu wapo kwenye nchi zao wanafanya uchunguzi kwa kushirikiana na wenzetu wa Interpol na tunataka kuwaonyesha kuwa ukijaribu Tanzania sio sehemu sahihi labda wamezoea kwao huko'' - IGP Sirro

7.''Kumrudisha Mo na kutelekeza gari hili sio mwisho, Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi, ninafahamu kati yao kuna mtanzania na tunataka tukiwapata tuongee lugha nzuri kuwa walikuwa wanataka nini''  IGP Sirro

6."Kuna kikundi cha watu wachache ambao ndio wamejenga imani ya kutoliamini jeshi la polisi, wao ndio wanajifanya wanajua upelelezi na wanajua zaidi ya jeshi la polisi hata kufikia hatua ya kutufundisha sisi jeshi la polisi namna ya kufanya kazi gani?" IGP Simon Sirro

5.''Kwenye gari tumekuta silaha za kivita kama AK47, 'Sub-machine gun' na Bastola 3. AK47 ikiwa na risasi 19 na risasi 16 za Bastola''  IGP Sirro

4."Mohammed Dewji amesema watekaji hao walikuwa na wasiwasi sana, baada ya kuona hawawezi kutoka, njia pekee  ni kuliacha hili gari hapa majira ya saa saba usiku, MO aliwapa taarifa wazazi wake wakaja kumchukua" - IGP Sirro.

3."Nimepata taarifa kwamba waliomteka Mohammed Dewji amesema walimwambia wanataka pesa, alipowauliza shilingi ngapi hawakusema. Aliwapa simu waongee na baba yake lakini waliogopa kwa sababu wanafahamu ulinzi wetu ni imara tungewakamata." - IGP Sirro

2.''Kuna watu tu wachache wanajaribu kuvuruga kazi za jeshi la  polisi na hatutawapa nafasi ya kufanya hivyo na sijui nia yao ni nini na wanatumwa nani kwa faida ya nani'' - IGP Sirro

1.''Wangechelewa tungewakamata na kuwakamata kwangu kungekuwa kwa tofauti, matukio haya yanapotokea yasitugawanye'' - IGP Sirro
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...