Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 4, 2018

CUF Lipumba Kumkamata Maalim Seif Akitua Liwale

adv1
Mbunge wa jimbo la Kaliua kupitia tiketi ya CUF, Magdalena Sakaya amesema kuwa endapo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi atajaribu kufika katika jimbo la Liwale kwa nia ya kumnadi mgombea bila kufuata utaratibu kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini kiongozi huyo atakamatwa na Jeshi la Polisi.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangu Maalim Seif atangaze mpango wa kwenda kumnadi Mgombea wa jimbo la Liwale, Mohamed Mtesa ambaye alipitishwa na upande wa Profesa Lipumba. Ambapo licha ya pande hizo zote  kuwa na migogoro zimenonesha kumuunga mkono mgombea huyo.

Sakaya amesema “Maalim Seif itakuwa ngumu kuingia Liwale, kwa sababu baada ya kukihujumu chama kwa muda mrefu tulitoa taarifa kwamba popote atakapofika akamatwe kwa sababu atahujumu tena, Makamanda wa mikoa na vituo vyote vya polisi Tanzania bara wanataarifa, akilazimisha kupanda jukwaa la kampeni atakumbana na nguvu ya Dola ".

“Sisi tulishawajua wao ni wahujumu siku zote, wamekuja kutuunga mkono kwa sababu CHADEMA wamejitoa kwenye uchaguzi, kwa hiyo tulikuwa tumeshawaandaa askari wetu ili wakionesha njama ya kutuhujumu wakamatwe, akitaka kuja kufunga kampeni lazima afuate taratibu, afike ofisini ili apangiwe na Mwenyekiti.” Ameongeza Sakaya

Kupitia Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF upande wa Maalim Seif, Mbarara Maharagande hivi karibuni alisema,

 “Sisi upande wetu hatuna tatizo, kwa sababu yule ni Mwenyekiti wetu wa Halmashauri na viongozi wetu wameshaelekea huko kumuunga mkono, Maalim Seif wiki hii anatarajia kwenda kufunga kampeni, Sisi ndio tulimwambia akachukue fomu na apitishe kwa upande wa Lipumba kwa sababu ndie anayetambuliwa na dola ".
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )