Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 16, 2018

Hanspope afikishwa Mahakamani Leo

adv1
Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe  amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Oktoba 16, 2018 ambapo ataunganishwa katika kesi inayowakabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange.

Mwenyekiti huyo wa usajili wa Simba amefikishwa mahakamani hapo ikiwa ni siku moja baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kukiri kumkamata  baada ya kumtangaza katika vyombo vya habari na kumtaka aripoti katika ofisi zake ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Alikamatwa juzi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Dubai.adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )