Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, October 17, 2018

Hatima ya Kubenea na Komu Baada ya Kikao Cha Kamati Kuu CHADEMA Kumalizika

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kesho Alhamisi kinatarajia kutoa hatma ya wabunge wake wawili Saed Kubenea wa jimbo la Ubungo pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini, Antony Komu kufuatia wabunge hao kudaiwa kupanga njama za kumdhuru moja ya mwanachama mwenzao.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya nje wa CHADEMA, John Mrema hatma ya wabunge hao inatarajia kujulikana kesho kufuatia kikao cha dharura cha wajumbe wa kamati kuu wa chama hicho walioketi hii leo wakiongozwa na Mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Mbowe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, John Mrema amesema ;“kamati kuu imeitishwa na tukawaita wabunge hao wawili, tumeshamaliza kumhoji mheshimiwa, Antony Komu na sasa tunaendelea na mahojiano na mheshimiwa Kubenea”

 “Kwa kuzingatia  mamlaka ya nidhamu ya kamati kuu kwenye chama chetu, tutapata wasaa wa kuwaita waandishi wa habari ili kuzungumza na kwa mwenendo unavyokwenda maamuzi hayo yatatolewa kesho kwa maana kikao kinaweza kumalizika usiku”, ameongeza John Mrema

 Hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, ilisambaa sauti fupi ikimuhusisha mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea pamoja na Mbunge wa Moshi Vijijini Antony Komu  wakipanga njama ya kumzuru Meya wa Manispaa ya Ubungo, Borniface Jakob.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )