Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, October 6, 2018

IGP Sirro Kasema Hali ya Ulinzi na Usalama Nchini Imeimarika.....Kaongelea Pia Dhamana kwa Watuhumiwa

adv1
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro  amewashuru wananchi kwa ushirikiano uliopelekea matukio ya uhalifu nchini kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwemo matukio ya matumizi ya silaha.

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini hapa Siro amesema kuwa matukio mengi ya uhalifu hapa nchini yamepungua ambapo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano utakaosaidia kuondoa uhalifu nchini.

Amesema kuwa Dhamana ipo kisheria na kila mmoja na haki ya kuipata hivyo inategemea na kosa ulilofanya ndio linepelekea kupewa dhamana tena kwa siku yoyote na muda wowote.

“Swala la dhamana lipo kwa mujibu wa sheria na dhamana inatolewa wakati wowote ila inategemea na makosa ya mtuhumiwa”alisema siro

Amesema Hali ya ulinzi na usalama hapa nchi kwa sasa ni shwari kuanzia hapa Arusha na mikoa mengine isipokuwa kwa kigoma wameongeza askari kuendelea kudhibiti matukio kwa kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa ya mipakani ina muingiliano.

Aidha amesema kuwa matukio ya mauaji ya mapenzi yamekuwachangamoto kubwa na yanalisumbua jeshi hilo hususani masuala ya ubakaji lazima tuwe wastaarabu kuepuka matukio yatakayopelekea mauaji na familia kuteseka.

“Suala la mauaji ya wapenzi kwa wapenzi ikiwemo kufumaniana limekuwa changamoto kwetu tumejipanga kuyashughulikia na kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini kulishughulikia hilo lipo kwenye uwezo wao”alitanabisha Sirro

Amesema kuwa ushamba ndio unaopelekea mtu kumuua mpenzi wake hivyo kuifanya familia kuteseka na kuwasihi watanzania kuweza kuepuka matukio hayo kwa kuwa wastaarabu na kuvumiliana.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )