Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, October 8, 2018

Jeshi La Polisi Jijini Mwanza Laua Majambazi Wawili

adv1
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewaua majambazi wawili katika mapambano ya majibizano ya kurushiana risasi na majambazi hao huko katika Lodge ya Vatican iliyopo Mtaa wa Calfonia –Nyegezi kata ya Nyagezi Wilaya ya Nyamagana Jiji na Mkoa wa Mwanza.

Tukio hilo limetokea tarehe 07/10/2018 majira ya saa 23:40hrs, hii ni baada ya kupatikana kwa taarifa toka kwa wasiri kwamba hapa Mkoani Mwanza wameingia majambazi wawili wakiwa na silaha za moto kwa ajali ya kufanya uhalifu na wamefikia Vatcan Lodge iliyopo mtaa Calfonia –Nyegezi.

Majambazi hao baada ya kufika kwenye Lodge hiyo walichukua chumba namba tano na kuweka mabegi yao kisha waliondoka kwenda maeneo ya katikati ya Jiji la Mwanza kwenye eneo ambalo walipanga kuja kufanya tukio la kiuhalifu. Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo Polisi tulikwenda mapema katika Lodge hiyo kisha tuliweka mtego.

Aidha ilipofika majira tajwa hapo juu, Polisi tulikwenda hadi kwenye chumba namba tano ambapo walifikia majambazi hao kisha tuligonga mlango mara kadhaa tukiwataka majambazi hao wafungue mlango ili tuwakamate wakiwa hai lakini waligoma. Ndipo baadae jambazi mmoja alifungua mlango ghafla kisha alifyatulia askari risasi, lakini kutokana na umahiri wa askari wetu waliweza kumpiga risasi jambazi huyo na kufariki dunia papo hapo.

Wakati jambazi huyo amepigwa risasi na askari, jambazi mwingine aliyekuwa ndani ya chumba alifunga mlango kisha alivunja dari ya lodge na kujificha kwenye dari hiyo. 

Polisi tulivunja mlango na kuingia ndani ya chumba hicho kisha alipelekewa moto mkali humohumo ndani ya dari ndipo baada ya kuona moto umekua mkali jambazi huyo alivunja paa la Lodge hiyo kisha alitoka na kuruka ukuta na kuanza kukimbia.

Polisi tulifyatua risasi kadhaa hewani na kumuamuru jambazi huyo asimame lakini alikaidi amri hiyo, ndipo baadae jambazi huyo alipigwa risasi wakati akiendelea kukimbia umbali wa mita mia moja toka ilipo lodge na kufariki dunia papo hapo.

Aidha katika tukio hilo, Polisi tumefanikiwa kukamata silaha moja iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za silaha aina ya short gun (Home made gun). Pia upekuzi ulifanyika katika chumba walichofikia majambazi hao na kupata risasi tano za silaha aina ya short gun ambazo hazijatumika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, linatoa wito kwa wananchi kuwa waendelee kutupatia taarifa, watu wote wanaongia hapa Mkoani kwetu lakini haijulikani shughuli wanayoifanya watupatie ili Polisi tuweze kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria. Pia tunatoa onyo kwa majambazi kwamba Mwanza wataingia lakini hawatatoka, hawa wameingia lakini hawajatoka.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )