Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, October 27, 2018

Kauli Ya Lady Jaydee Kama Yuko Tayari Kufanya Kolabo na Mtoto wa X Wake, Gardner Habash.

Msanii nguli kwenye game ya bongo fleva Judith Wambura marufu kama Comando Jide, ameweka wazi kuwa tayari kufanya collabo na msanii Karen, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mume wake mtangazaji Gardner Habash.

Jaydee amekiambia kituo cha EATV kwamba mikono yake iko wazi kumpokea binti huyo ambaye kwa sasa anakuja kwa kasi kwenye game ya bongo fleva, akiwa na kazi zake zinazoendelea kufanya vizuri.

Akimzungumzia Karen ambaye kwake alikuwa ni mama mlezi, amempongeza kwa kuwa binti mrembo na kuamua kuingia kwenye muziki rasmi, huku akimtaka kukaza buti.

“Kwanza nampongeza sana amekuwa binti mkubwa mrembo na anafanya mambo mazuri, kwa hiyo asikate tamaa kila kitu kinawezekana afuate ndoto zake ataweza kufanikiwa, kuhusu collabo anakaribishwa anytime mikono yangu iko wazi”, amesema Jaydee.

Hivi karibuni Karen alikuwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwamba kwenye game anamkubali Jaydee na ndiye mtu aliyegundua kipaji chake, wakati anaishi naye kama mama mlezi.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...