Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, October 1, 2018

Lugola Awataka Wakuu Wa Idara Kushirikiana Na Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wakuu wa idara kushirikiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Katavi.

Amesema hayo leo Oktoba mosi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakuu wa idara wa mkoa wa Katavi, alipowasili mjini Mpanda akitokea Kigoma.

Waziri huyo amefanya ziara ofisi za mkoa huo kwa ajili ya kujua ushirikiano wa watendaji wakuu wa mkoa huo pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo.

Waziri Lugola amepolekewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Katavi, Lilian Matinga na baadhi ya maofisa mbalimbali wa polisi mkoani humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, ACP Damas Nyanda alipokua anafafanua jambo katika Kikao cha Wakuu wa Idara wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoani humo. Watatu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Abdallah Malela. 

Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...