Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, October 21, 2018

Lulu Michael Karudi UPYA Ndani ya Bongo Movie

Msanii wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ yupo locationi kwa ajili ya kuandaa movie mpya ambayo haijajulikana ni lini hasa itatoka.

Aliyefichua hilo ni mchumba wa Lulu, Majizzo ambaye amepostu picha ya Lulu kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusindikizia na caption iliyomeka;  Back to business Elizabeth Michael'

Novemba 13, 2017 muigizaji wa filamu Bongo, Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa muigizaji mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia.

Utakumbuka kifo cha Kanumba kilitokea April 04, 2012 na mwaka huo alifunguliwa mashkata na hukumu ikaja kutoka 2017.

Usiku wa May 13, 2018 ziliaza kusambaa taarifa mtandaoni kuwa Lulu yupo uraiani, siku iliyofuata mamlaka husika zilithibitisha kuwa Lulu ametoka kwa msamaha wa Rais Magufuli. Hivyo baada ya hayo yote Lulu anarejea tena kwenye filamu kwa kufungua ukurasa mpya.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )