Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 4, 2018

Mabasi Yanayokalisha Abiria Kwenye Ndoo Yapewa Onyo

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa ameweka bayana, askari wa usalama barabarani hawataona muhali kuchukua hatua dhidi ya mabasi ya abiria yatakayojaza abiria pamoja na yanayokalisha abiria waliozidi kwenye ndoo za lita 20.
 
Aidha ameyaasa ,magari ya watoto wa shule mengi ni machakavu  hivyo ameelekeza wayapeleke yakaguliwe kabla ya kubeba wanafunzi .
 
Akitoa rai hiyo kwa waandishi wa habari, Nyigesa alisema ,haiwezekani madereva wakakiuka sheria za usalama barabarani kwa makusudi wakitegemea kutoa faini bali wanachotakiwa ni kufuata sheria zilizopo. 
 
Aliwataka ,abiria na jamii kutoa ushirikiano kwa askari hao kwa kutoa taarifa ama kuyafichua magari ya abiria yanayojaza abiria kupita kiasi ili wayachukulie hatua ikiwemo kupigwa faini. 
 
Nyigesa alieleza, magari ya watoto wa shule mengi ni machakavu  hivyo ameelekeza wayapeleke yakaguliwe kabla ya kubeba wanafunzi .
 
Aliwataka,  waendeshaji wa vyombo vya moto kutii sheria, na kwamba magari yao yatakaguliwa yawapo ndani ya mkoa huo.
 
“Magari ya watoto yaliyo mengi hayana mikanda sasa ni jukumu lao kujikaguwa kabla hawajakaguliwa na kukamatwa ,
“Hakuna polisi atakayemuonea aya dereva wala hatutaona muhali katika suala hili la kudhibiti ajali”alisisitiza Nyigesa.
Kamanda huyo alieleza, kila mmoja atii sheria bila kushurutishwa .
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )