Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, October 25, 2018

Mahakama Yaamuru Pedeshee Ndama Mtoto Wa Ng'ombe Akamatwe

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kukamatwa kwa mfanyabiashara, Ndama Shabani Hussein maarufu ‘Pedeshee Ndama Mtoto ya Ng’ombe’ baada ya kukiuka taratibu za dhamanana.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde, ametoa hati hiyo jana, Jumatano Oktoba 24, 2018, baada ya mshtakiwa huyo kushindwa kufika mahakamani hapo bila kutoa taarifa, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa..

Aidha Hakimu Maira ametoa barua ya wito kwa wadhamini wa mshtakiwa huyo kufika mahakamani na kueleza alipo mshtakiwa.

Kabla ya kutolewa kwa amri hiyo ya kukamatwa kwa mshtakiwa, wakili wa Serikali, Mosia Kaima, alidai kuwa, kesi hiyo  ilikuja kwa kutajwa lakini mshtakiwa hayupo nahata mashaidi wake pia hawapo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12. 2018 kesi hiyo itakapokuja kwa kutajwa.

Ndama anakabiliwa na mashtaka matano yakiwemo ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu,
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )