Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 5, 2018

Manara Aibuka Sherehe ya Kuzaliwa Diamond na Kuahidi Kusomesha Walemavu Tandale, Kuanzisha Ligi ya Diamond

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara leo aliamua kuingiza siasa baada ya kuibuka  kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa mwanamuziki Diamond.

Haji Manara aliufananisha umati uliofika kumuona nyota huyo na wapiga kura kwa kusema Diamond angepita bila kupingwa iwapo angegombea nafasi yoyote ya ubunge.

“Kama Diamond angetaka kufanya siasa hizi zote kura zake nawaambia, nimejaribu kumuuliza kuhusu hilo lakini mwenyewe amesema hataki kufanya siasa hivyo wanasiasa mtulize roho zenu,” amesema Manara.

Mara baada ya kusema hayo shangwe ziliibuka uwanjani hapo na baadaye Manara alizungumza tena na baadaye alitoa mipira kwa shule za Tandale.

Amesema ili watoto wakue vizuri ni muhimu wapate muda wa kucheza hivyo anatoa mipira hiyo ili kuhakikisha wanashiriki michezo.

Amesema katika kumuunga mkono Diamond amezungumza na wadau ambao wamekubali kuweka ligi Tandale itakayofahamika kwa jina la ‘Diamond Tandale Super Cup.’

Manara ametangaza kugharamia ada za wanafunzi wote walemavu watakaoanza shule Januari mwakani.

“Wanafunzi walemavu wote watakaoanza mwakani nitalipa ada kuanzia msingi hadi sekondari ili mradi iwe shule za serikali,” amesema Manara huku akishangiliwa.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )