Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, October 13, 2018

Masaa 48 Yamepita Mo Dewji Bado Hajapatikana.....Msako Mkali wa Kumtafuta Bado Unaendelea

Ni siku mbili zimepita tangu bilionea mashuhuri nchini, Mohammed Dewji ‘MO’  alipotekwa Alhamisi asubuhi katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi bado linafanya  jitihada za kumtafuta bilionea huyo wa Tanzania, ambaye  tangu alipotekwa amezua maswali miongoni mwa jamii wakitaka kujua sababu ambazo zimesababisha kutekwa.


Inaelezwa kuwa ulinzi umeimarishwa kila sehemu hasa  katika Pwani ya Bahari ya Hindi hususani katika hoteli zilizo ukanda huo ikiwamo Yacht Club.

Polisi  wamekuwa wakikagua kamera za video (CCTV) katika hoteli ya Yacht Club, lengo likiwa ni kumsaka mfanyabiashara huyo

Meneja Mkuu wa Yacht Club, Brian Fernandez jana alisema  kuwa tangu tukio la kupotea kwa Mo lilipotokea, polisi wameimarisha ulinzi na uchunguzi katika eneo hilo ambalo liko pwani ya Bahari ya Hindi.

Fernandez alisema Mo alikuwa mwanachama wa klabu hiyo na hakuonekana katika eneo hilo tangu juzi na hakuna boti ya mwanachama yeyote iliyoondoka tangu jana.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )