Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 5, 2018

Mbwana Samatta Kujiunga na Taifa Stars Cape Verde Kuongeza Nguvu

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta, ameshindwa kujiunga na kambi ya timu ya Taifa Stars hapa nchini, badala yake atajiunga na timu moja kwa moja nchini Cape Verde.
 
Afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo ameweka wazi kuwa nahodha huyo atajumuika na timu huko Cape Verde, huku wachezaji wengine wa kimataifa wakitarajiwa kuwasili nchini kujiunga na timu muda wowote kuanzia leo.

''Tunatarajia wachezaji wetu wanaocheza soka nje ya nchi  watajiunga na timu muda wowote kuanzia leo lakini nahodha wetu Mbwana Samatta ataungana na timu huko Cape Verde'', amesema Ndimbo.

Mbali na hilo Ndimbo amemshukuru kocha wa Lipuli FC Selemani Matola kwa kuwaruhusu moja kwa moja wachezaji wake wawili Ally Sonso na Paul Ngalema kujiunga na kambi bila kutoka kwenda kuichezea timu hiyo ambayo leo inakipiga na Stand United.

Mbwana Samatta jana alikuwa uwanjani kuichezea klabu yake ya KRC Genk kwenye mchezo wa Europa League kundi I, ambapo ilikubali kichapo cha mabao 3-1 ugenini dhidi ya Sarpsborg 08 ya Norway.

Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo wake wa tatu katika kundi L kuwania ufuzu AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde mjini Praia, 12 Oktoba kabla ya mchezo wa marudio utakaopigwa Jumanne 16, Oktoba jijini Dar es Salaam. Tanzania inashika nafasi ya 2 ikiwa na alama 2 nyuma ya Uganda yenye alama 4.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...