Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 3, 2018

Mchungaji Msigwa Kumburuza Mahakamani Mkuu wa Mkoa Wa Iringa Ally Hapi

adv1
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema  atamfikisha mahakamani Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi  kufuatia uamuzi wake wa kumuweka ndani diwani wa Viti maalum CHADEMA, Silestina Jonso.

Msigwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa jana Octoba 2, alisema Hapi alimdhalilisha diwani huyo.

“Alidiriki kumdhalilisha diwani wetu, sheria iko wazi sana, vipengele vyote vile mkuu wa mkoa hakufuata, amekiuka, ametoa amri ya kumpeleka diwani wetu polisi kinyume cha sheria.

“Sasa kwa sababu amekiuka taratibu, mimi kama mwenyekiti wa kanda na mbunge ili kukomesha tabia hii ya RC Hapi  tumwambie hatukubaliani naye na hatujalala, anakuja na sheria zake za kutisha watu na kuwatia ndani.

"Tumejipanga vizuri tunamfungulia kesi mahakamani kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya. Tutakutana naye mahakamani kwa sababu anatumia madaraka vibaya.” Alisema Msigwa
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )