Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, October 6, 2018

Meya Boniface Jacob: Napenda Ukuu wa Mkoa, Lakini Siwezi Kuwasaliti Wananchi Wangu

Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Boniface Jacob amesema anapenda nafasi ya Ukuu wa Mkoa na Ukuu wa wilaya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini hawezi kuhamia chama hicho kwa kile alichokidai atakuwa amewasaliti wananchi wake, wanaoishi mazingira magumu hasa kwenye halmashauri yake.

Meya Boniface Jacob amesema katika vitu ambavyo hatamani kuvisikia kwa mtu yeyote ni kwamba yeye binafsi ana  mipango ya kuhamia CCM na kusema kauli hiyo ni inalenga kumdhalilisha.

“Kwa mfano mimi nina maisha magumu napenda Ukuu wa Mkoa, Ukuu wa Wilaya shida ni kwamba nitafata vitu vizuri lakini sitakuwa na amani ya roho sababu nitawasiliti watanzania wenye maisha magumu, hicho ndio kinanifanya nisiwe upande wa CCM,” Amesema Meya wa Ubungo Boniface Jacob.

Kuhusiana na mapigano ya hivi karibuni yaliyotokea kwenye Uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala amesema tukio hilo limemkumbusha uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji ambapo Meya huyo wa Ubungo alishikana mashati na Meya wa Temeke Abdallah Chaulembo.

“Unajua wananchi wanapaswa kujua kuwa vyama vya upinzani huwa vinapata tabu sana kwenye uchaguzi hapa nchini lakini niwaambie hatutakata tama, tutaendelea kutetea haki zetu.” Ameongeza Meya wa Ubungo Boniface Jacob.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )