Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, October 24, 2018

Mh shonza Akanusha Tetesi za CCM Kuwatumia wasanii Kwenye Kampeni 2020

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Daniel Shonza,amefunguka kuhusiana na kile kilichokuwa kinasemekana kwamba chama hicho kimepanga kukutana na wasanii kwa lengo la kuwatumia kwenye kampeni za chama hicho mwaka 2020.

Naibu waziri ameongea hayo wakati anazungumza na waandishi wa habari jana katika kikao ambacho wasanii wa Bongo fleva na wasanii wa Bongo movie walialikwa na katibu mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole katika hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam.

Mhe.Shonza alijibu swali la mwandishi na kusema kuwa “Kikao hiki hakiko kisiasa na ndio mana tumealika wasanii wote na tunajua kuwa wasanii wetu wako vyama tofauti vya kisiasa,na kikao chetu hichi kimekutanisha wadau na wasanii wote bila kujali vyama wala itikadi zao za kisiasa na wala hakina malengo ya kampeni za 2020 japokuwa sisi tunafanya kazi karibu sana na wasanii”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )