Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, October 4, 2018

Mhadhiri UDOM Atiwa Mbaroni Kwa Rushwa ya Ngono

TAKUKURU Mkoa wa Dodoma jana usiku iliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Jacob Paul Nyangusi ambaye ni Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kosa la kumtaka mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kingono ili amsaidie katika mitihani ya marudio aliyofanya hivi karibuni.

Kosa hili ni kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Na. 11/2007.

Mhadhiri huyo alikamatwa saa tatu usiku katika eneo la nyumba mia tatu kata ya Nzuguni jijini Dodoma akiwa chumbani na mwanafunzi huyo. 

Awali TAKUKURU ilipokea taarifa za Mhadhiri huyo kutaka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake ambaye jina limehifadhiwa ili amwezeshe kufanya mitihani ya marudio baada ya kufeli na pia amsaidie wakati wa usahihishaji.

Baada ya kupokea taarifa hizo TAKUKURU ilifanya uchunguzi wa awali na kuandaa mtego uliofanikisha kukamatwa kwake. 

TAKUKURU inaendelea na uchunguzi na mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kikitolewa.

TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imekuwa inapokea taarifa za baadhi ya wahadhiri wasio waadilifu kuwataka wanachuo hasa wa kike kingono ili wawasaidie katika masomo yao.

 Aidha, baadhi wanawafelisha wanafunzi kwa makusudi na baadaye kuwataka rushwa ili warekebishe matokeo yao.

TAKUKURU inatoa wito kwa wanafunzi wa kike na wananchi wote kwa ujumla kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ya ngono wanapokutana navyo.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...