Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, October 21, 2018

Mtoto amuua baba kwa Shoka kisa kunyimwa mahari

Jeshi la Polisi mashariki mwa mji wa Eldoret, kaunti ya Uasin-Gishu magharibi mwa Kenya imemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 28, Andrew Kimutai, akituhumiwa kumuua baba yake, Joseph Marindany .

Akithibitisha tukio hilo OCPD wa Eldoret Mashariki Bw Richard Omanga, amesema kuwa Andrew anatuhumiwa kumuua baba yake kwa kumkata kichwa kwa kutumia shoka, baada ya kukataa kumpa kondoo wa familia ili alipe mahari kukomboa mtoto wake wa kiume aliyempata nje ya ndoa.

“Marehemu alikataa kumpa mwanawe kondoo kwa sababu hakujua alikuwa amezaa mtoto nje ya ndoa kama alivyodai. Mshukiwa alikasirishwa na msimamo wa baba yake ndipo alimvamia baba yake akiwa chumbani mwendo wa saa moja, akamkatakata kwa shoka,” alisema OCPD Omanga.

Mtuhumiwa huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Naiberi akisubiri kufunguliwa mashtaka baada ya uchunguzi kukamilika.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...