Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, October 23, 2018

Mwanafunzi Afariki Dunia Baada ya Kugongwa na Gari Akielekea Shuleni

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Igokelo wilayani Misungwi wamelazimika kusitisha masoma baada ya mwenzao kugongwa na gari na kufariki dunia.

Mwanafunzi huyo Mariamu Bupilipili ambaye alikuwa kidato cha tatu amekutana na mkasa huo uliochukua maisha yake leo asubuhi wakati akienda shuleni.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Hamisa Hassan  alisema walipokea taarifa za kugongwa kwa mwanafunzi huyo asubuhi na kuthibitisha kwamba ni mwanafunzi wao.

"Tumesikitika sana kwa kumpoteza Mariamu, alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi tuliowategemea sana. Siwezi kuzungumzia sana hii habari maana polisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hili," alisema Hamisa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema taarifa za kugongwa kwa mwanafunzi huyo zilikuwa hazijafika ofisini kwake.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )