Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 26, 2018

Mzee wa miaka 76 ajinyonga hadi kufa

Mzee anayenufaika na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Tasaf, Anthony Mikami (76) amejinyonga kwa kamba ya chandarua katika kijiji cha Nyabihanga kata ya Bukiriro wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa kile kinachodaiwa kuwa na msongo wa mawazo

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabihanga, Eradius Batakanwa amesema mzee huyo alijinyonga kwa kujitundika kamba kwenye mti mbali na makazi ya watu na aligundulika jana Jumatano Oktoba 24, 2018 saa 9:30 mchana kwa waliokwenda mabondeni kuvuna maharage.

Batakanwa amesema siku za hivi karibuni wakati wa uhai wake akiwa mnufaika wa Tasaf kijijini humo aliunguliwa na nyumba wakati akichoma viroboto na kuiteketeza nyumba hiyo.

"Baada ya kuunguliwa nyumba alichanganyikiwa maana alikuwa hana chakula cha usiku na mchana huku akiwa hana wasaidizi licha ya kujaliwa watoto watano wa ...kiume mmoja na wakike wanne," amesema Batakanwa na kuongeza kuwa hilo ni tukio la pili baada ya lile la kwanza lililotokea Februari.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )