Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, October 1, 2018

Navy Kenzo Wazungumzia Kujiunga na Lebo ya WCB Ya Diamond

Kundi la Navy Kenzo ambalo kwa sasa linafanya vizuri na wimbo wao mpya 'Katika' ambao wamemshirikisha Diamond Platnumz limeeleza ilivyokuwa hadi kumshirikisha muimbaji huyo na ishu ya kusaini WCB.

Navy Kenzo wakizunguza na Waandishi kwenye red carpet ya Biko Jibebe Challenge, wamesema wimbo huo walimtumia Diamond wakijua fika angeupenda na kwa sasa wanafanya kazi na Meneja Sallam SK na sio lebo ya WCB.

"Huu wimbo ambao tunatakiwa tumuweke, tukamtumia nadhani alikuwa kwenye tour yake ya Marekani, yeye mwenyewe aliipokea kwa shangwe sana kwa sababu mimi mwenyewe nilijua ni wimbo ambao ataupenda, akarudi tukaifanya then we have Katika today," amesema Nahreel.

Kuhusu suala la kusaini kwenye lebo ya WCB, Nahreel amesema bado hilo ila kwa sasa wanafanya kazi na Sallam SK kutokea kwenye labo hiyo pia.

Tangu Navy Kenzo kuwa chini ya Meneja Sallam SK wametoa nyimbo mbili ambazo ni Fella na Katika.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )