Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, October 21, 2018

Young Killer aondoka Wanene Entertainment

Msanii wa hip hop Bongo, Young Killer ameweka wazi kuwa mtataba na lebo yake ya Wanene Entertainement umemalizika.

Rapper huyo ameeleza kuwa mkataba wao ulikuwa wa miezi sita na sasa umeisha na hawezi kuendelea nao. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Young Killer ameandika;

"Napenda kuwashukuru Wanene Studios Kwa kuniamini na kupiga kazi pamoja na mimi kwa muda wa mkataba wa kipind cha miezi 6 ambacho tumepiga kazi. Ambapo mkataba wetu umeisha rasmi na sitoweza kuendelea

 "Nashukuru sana kwa kazi nzuri tulizoshirikiana kufanya kwa kipindi chote cha mkataba ambacho tulikuwa pamoja, tulifanya kazi pamoja na lengo letu lilikuwa nikuona mimi nafika mbali zaidi. Nimepitia vitu vingi sana changamoto nyingi sana. Yote kwa yote napenda kusema nimejifunza vingi ambavyo vitabaki kua kama alama ambayo itaniongoza kwenye safari yangu nyingine."

Utakumbuka kuwa Young Killer alisaini kuwa chini ya lebo ya Wanene April 13, 2018 na kutoa wimbo wake wa kwanza uitwao Shots ambao amemshirikisha Khaligraph Jones kutokea nchini Kenya.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )