Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, October 26, 2018

Polisi Kuwachia Huru Mmoja Anayeshikiliwa Kuhusiana Na Tukio La Kutekwa Mo Dewji

adv1
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema mtu mmoja aliyebaki kati ya saba waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi hilo kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji, ataachiliwa wakati wowote kwa sababu wameshamalizana naye.

Dewji maarufu ‘Mo Dewji (43)’, alitekwa wiki mbili zilizopita katika Hoteli ya Collesium, iliyopo Osterbay jijini Dar es Salaam na kupatikana baada ya siku tisa katika maeneo ya Gymkhana alikotelekezwa na wanaodaiwa kuwa watekaji huku pia wakitelekeza gari aina ya Toyota Surf likiwa na silaha kadhaa za moto.

Mtu anayeendelea kushikiliwa na Polisi ni miongoni mwa watu 26 waliokamatwa awali baada ya kuwaachia wengine 19 na kubakia saba na kisha sita wakaachiliwa na kubakia mmoja.

Miongoni mwa waliokamatwa na kuachiliwa ni pamoja na msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara aliyeshikiliwa na polisi kwa takribani wiki moja tangu alipokamatwa siku moja baada ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )