Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 2, 2018

Rais Magufuli Katimiza Ahadi Yake Ya Milioni 20 Aliyoitoa Jana

adv1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 02 Oktoba, 2018 ametekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi Milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo jana alipokutana na wajasiriamali hao wakati akifanya mazoezi ya jioni pamoja na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli ambaye pia ametekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi Milioni 5 kwa akina Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.

Fedha hizo zimekabidhiwa na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kwa Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga, na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama.

Kabla ya kukabidhi fedha hizo Bw. Ngusa amesema pamoja na kutoa fedha hizo Mhe. Rais Magufuli ameagiza Manispaa ya Ilala impelekee taarifa ya mapato na matumizi ya soko la samaki la Feri haraka iwezekanavyo na amemuagiza Mkuu wa Wilaya na Manispaa ya Ilala kushughulikia kero za wavuvi na wajasiriamali wa eneo hilo ikiwemo ushuru wenye kero na tatizo la vyoo.

Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina mama wajasiriamali wa Feri Bi. Ashura Seif Nanjonga wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasaidia fedha hizo na kwa kuwajali wao pamoja na Watanzania wengine hasa wanyonge.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutembelea soko la Feri na kuwasaidia wajasiriamali wa soko hilo na amesema yeye na timu yake ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala wataanza mara moja kushughulikia kero za wajasiriamali hao.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Oktoba, 2018
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )