Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 11, 2018

RC Makonda Akanusha Taarifa za Mo Dewj Kupatikana, Atoa Onyo kwa Wanaosambaza uongo

adv1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekanusha taarifa za kupatikana kwa mfanyabishara Mohammed Dewji, na kwamba taarifa zilizosambaa kuwa amepatikana sio sahihi.

RC Makonda ametoa onyo kali kwa yeyote atakayeibuka na kuanza kusambaza taarifa za uongo kuhusiana na tukio hili au kuligeuza na kulifanya mtaji wa kisiasa.

Amesema msemaji wa tukio hili kwa upande wa polisi ni  Kamanda wa Kanda Maalum Dar Lazaro Mambosasa na kwa upande wa Serikali ni yeye.

Katika hatua nyingine,Makonda, amependekeza  kufungwa kwa kamera katika maeneo yote jijini Dar es salam, ili kupata msaada mkubwa yanapotokea matukio ya kiuhalifu kama hili.

Amesema iwapo Dar es salaam itafungwa kamera, itakuwa msaada mkubwa kwa vyombo vya usalama kufuatilia matukio ya kiuhalifu kama la kutekwa kwa Mo Dewji.

“Tuna mpango mkubwa zaidi nafikiri umefika wakati sasa wa mkoa wa Dar es salaam wote kufungwa camera, leo hii tungekuwa na camera, tungeongezea hata weledi wa jeshi letu la Polisi kufuatilia gari iko wapi, ifike hatua Dar es salaam iwe na camera tukamate wahalifu kwa haraka zaidi, kuliko kutumia nguvu kubwa kumfuatilia mtu ambaye hujui amepita wapi”, amesema Paul Makonda.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )