Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, October 2, 2018

Rich Mavoko: Sina Ugomvi Wowote na Diamond

Msanii wa muziki Bongo, Rich Mavoko amesema hana tatizo lolote na Diamond Platnumz licha ya kuondoka kwenye lebo ya WCB.

Muimbaji huyo kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema kilichotokea kati yake na lebo hiyo sio ugomvi bali ulifika mwisho wa biashara yao, hivyo sasa wapo vizuri pamoja na uongozi mzima wa lebo hiyo.

Katika hatua hatua nyingine Rich Mavoko amesema kuwa maneno yanayosikika mwanzoni kwenye video ya wimbo Ndegele hayawahusu WCB kwani walikuwa wanataka tu kuvuta attention ya mashabiki ila kuhusu kuwa ni diss kwa lebo sio kusudio lao kabisa.

Mwaka 2016 Rich Mavoko ndo alijiunga na WCB, wimbo wake wa kwanza kutoa chini ya lebo hiyo unakwenda kwa jina la Ibaki Stori, kisha Kokoro na nyinginezo, pia ameweza kufanya kazi na wasanii wengine nje ya WCB kama Fid Q, Stereo, Nay wa Mitego, Lulu Diva na wengine.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...