Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, October 7, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 02

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA

‘Ethan…..Ethan…….Ethan……’
Niliisikia sauti ya kiume ikiniita kwa mbali, nikajaribu kuangaza macho yangu ndani ya chumba hichi ili niweze kuona ni nani anaye niita ndani ya hichi chumba ila sikuweza kuona zaidi ya mapazia kuendelea kutingishika sana. Woga ukanijaa, mwili mzima ukazidi kunitetemeka.
“ETHAN……..”
Sauti hii nzito nikaisikia vizuri kwenye masikio yangu, taa zote ndani ya chumba hichi zikazima na nikaona kivuli cha mtu chenye mwanga hafifu sana kikiwa kimesimama kwenye moja ya ukuta wa humu chumbani huku kivuli hicho kikionesha mtu huyo akiwa amevaa joho kubwa sana, ila haonekani kichwa ni kipi wala miguu ni ipi jambo lilo nifanya niaguke chini mzima mzima huku nikitamani kupiga kelele ila sauti yangu haikuweza kutoka.
   
ENDELEA
“Usiogope, mimi sio mbaya kwako”
Sauti ya mwanaume huyu ikazidi kuniongelesha, jasho lililo tokana na joto kali likazidi kuniandama.
“Najua nini unacho kiwaza na kukifikiria. Nitakusaidia, kadri siku zitakavyo zidi kwenda ndivyo kadri nitakavyo zidi kuwa rafiki yako na msaada wako kwako. Usimuambie mtu wa aina yoyote habari hii umenielewa?”
Nikamjibu kwa kutingisha kichwa nikimaanisha kwamba nimelewa.
 
“Endapo utazungumza chochote kwa mtu yoyote basi mtu huyo nitamuua. Lala salama na usiku mwema”
Mara baada ya mwanaume huyo kuzungumza hivyo, taa zote zikawaka na kila kitu kikarudi kwenye hali yake, hapakuwa na pazia hata moja ambalo liliweza kutingishika. NIkasimama kwa haraka na kuanza kutembea hadi mlangoni ili nikawaeleze Bi Jane Klopp na mumewe habari hizi, ila nilipo kumbuka kwamba endapo nitamualeza yoyote atakufa, basi hamasa hiyo ya kuwaambia, ikaanza kutetea na mwishowe nikajikuta nikirudi kitandani mwangu na kuaa. Kusema kweli katika siku ambazo sikuwahi kulala ni hii ya leo, sauti ya mwanaume huyu ambaye sifahamu ni nani ikazendelea kujirudia kwenye masikio yangu. 
 
Nikastuka baada ya kengele iliyo fungwa mlangoni humu kuanza kuita, nikatazama saa ya ukutani nikaona ni majira ya saa kumi  na moja kasoro alfajiri. Nikakumbuaka kwamba jana usiku bibi Jane Klopp aliniahidi kwamba atakuja kuniamsha muda huu ili nianze kuajiandaa kwa ajili ya safari kwa maana ndege yetu inaondoka saa kumi na mbili asubuhi. Kengele ikaendelea kuminywa, taratibu nikashuka kiyandani na kuanza kutembea hadi mlangoni, nikaufunga mlango nakweli nikamkuta bibi Jane Klopp akiwa amejawa na tabasamu  pana sana usoni mwake.
“Umeamkaje Ethan?”
“Salama mama, wewe je?”
Niliitikia huku nikijifanya kama nina usingizi mwingi, ila kwa namna moja ama nyingine sina usingizi wa aina yoyote zaidi ya woga wa tukioa ambalo nilikutano nalo jana usiku.
 
“Tumeamka salama, jiandae tuianze safari”
“Sawa mama”
“Haya”
Bi Jane Klopp akaondoka mlangoni kwangu, nikafunga mlango na moja kwa moja nikalifwata sehemu begi langu la nguo lilipo, nikafungua zipo ya pembeni, nikatoa mswaki wangu pamoja na dawa yake, kisha nikaelekea bafuni. Nikasafisha kinywa changu, ndani ya muda mfupi nikiwa tayari nimesha maliza kukisafisha kinywa hichi. Nikaoga haraka haraka kisha nikarudi chumbani, nikavaa nguo nilizo kusudia kuzivaa katika safari hii, ambayo tayari hamu yake imerudi kwenye mstari hata tukio lililo tokea jana usiku likaanza kunipotea kwenye upeo wangu wa akili.
 
    Nilipo hakikisha kwamba nimemaliza kila kitu, nikamuomba Mungu kama nilivyo fundishwa na Bi Jane Klopp, ili awe kunitangulia katika safari hii, kisha nilipo maliza sala yangu, nikatoka chumbani humu huku nikilivuta begi langu. Kwa bahati nzuri nikakutana na Bi Jane Klopp  pamoja na mzee Klopp wakitoka kwenye chumba chao huku nao wakiwa tayari wamesha jianda. Nikamsalimia mzee Klopp kwa heshima zote, kisha tukaelekea nje ya hoteli hii na kumkuta yule dereva ambaye alituleta jana hapa hotelini akiwa tayari amesha fika kama vile alivyo elezwa na bi Jane Klopp aweze kuwahi asubuhi na mapesa kwenye hotel hii. 
Baada ya dereva kuingiza mabegi yetu nyuma ya taksi yake hii, mimi na bi Jane Klop tukaingia kwenye siti ya nyuma huku Mzee Klopp akipanda siti na kukaa siti ya mbele pamoja na dereva.
 
“Ethan mwanangu, unajisikiaje?”
Bi Jane Klopp aliniuliza huku akiwa amenishika mkono wangu wa kulia huku akiminya minya kiganja changu.
“Ndio mama, nina furaha sana”
“Unakwenda kuyaanza maisha mapya sasa Ethan”
“Kweli baba ninakwenda kuanza maisha mapya”
“Ila tutakuwa tunarudi Tanzania mara kadhaa, kuitembele hii nchi si unafahamu kwamba hii ndio nchi yako”
“Ndio mama”
“Hata ikatokea kwamba tumekufa, ila Tambua uhalisia wako wewe ni upi, wapi umetoka na tunaamini kwamba ipo siku utakuna na ndugu zako”
“Sawa mama”
 
Swala la ndugu zangu bado kwa upande wangu ni kitendawili, nina jaribu kuvuta kumbukumbu za kumkumbuka japo hata mama yangu wa kunizaa ila sipati hata taswira yake. Tukafika uwanja wa ndege, tukapitia hatua zote ambazo kama abiria anatakiwa kupitia, muda wa abiria kuelekea kwenye ndege tunayo paswa kusafiri nayo, ukawadia. Tukaingia kwenye ndege hiyo bibi Jane Klopp na mumewe wakaa katika siti za mbili huku mim nikikaa siti ya pembeni yao, ila na abiria mwengine ambaye ni mwana mama wa kiafrika. Nikamsalimia mwana mama huyu kwa heshima sana, hadi mwenyewe akanishangaa. Akaitikia salamu yangu huku akiwaametabasamu.
“Unaitwa nani mtoto?”
“Ethan Klopp”
“Anaa mimi naitwa mama Lukas”
“Nashukuru kukufahamu mama Lukas”
“Unasafiri peke yako?”
“Hapana, nipo na wazazi wangu, hao hapo”
Nikawaonyesha Bi Jane Klopp na mume, ambao nao kwa furaha wakasalimiana na mama huyu. 
 
“Kusema kweli nimetokea kumpenda sana huyu mtoto ana heshima na maadili mazuri sana”
“Hata sisi tunampenda Ethan wetu kwani ni kijana mtiifu na mwenye hekima sana”
“Aisee muendelee kumkuza kwenye maadili haya haya. Hapa ninawaambia muna tunda lilo bora”
“Tunashukuru”
“Munaelekea wapi?”
“Sisi tunarudi Ujerumani, tulikuwa Tanzania, kwa kazi ya mwaka mmoja, imeisha wiki hii basi tunarudi kwetu, japo Mungu ametubariki tunarudi tukiwa na mtoto wetu”
“Hahaha kweli Mungu amewabariki kwa kweli, yaani nina watoto kama huyu. Ila niwakorofi hakuna, ila nilipo muona huyu na jinsi alivyo nisalimia, hakika nikaona kwamba ndani ya huyu mtoto kuna tunda lililo jema”
 
“Shukrani sana”
Bibi Jane alijibu huku akiwa amejawa na furaha sana kwani nyota yangu ya kupendwa na watu inaanza kukua sasa.
“Wewe Ujerumani unakwenda matembezi au?”
“No, ninakwenda kikazi, raisi ameniteua kuwa balozi kule jana mchana, na leo nimegizwa nikawasili ubalozini haraka iwezekanavyo baada ya hapo, basi nitafanya hatua za kuwahamishia watoto wangu nchini humo”
“Ohoo hongera sana”
“Asante sana, nilikuwa ni mkurugenzi wa shirika la Afya, ila raisi alivyo ona anapendezwa na utendaji wangu wa kazi basi ameniteua katika nafasi hiyo”
“Kweli weli, vipi lakini una watoto wangapi?”
“Watu, wa kike wawili ni mapacha, Jane na Judy, hao wana miaka kumi na mbili sasa na Lukas cha ukorofi ana miaka sita”
 
“Waoo, naona hapo nina wajina wangu”
“Hee…unaitwa Judy na wewe?”
“No ninaitwa Jane Klopp”
“Okay safi sana, ninashukuru kwamba nimepata wenyeji wangu na hongera una fahamu Kiswahili vizuri sana”
“Yaa ni kweli, nilijifunza kwa juhudi mimi na mume wangu basi tumeweza kukifahamu. Na hata Ethan naye amesha kifahamu Kijerumani”
“Aisee Ethan inabidi unifundishe na mimi Kijerumani”
Nikamsalimia Mama Lukas kwa lugha ya kijerumani, akabaki akinitazama tu na kushindwa kunijibu.
“Ndio umesemaje?”
“Nimekusalimia habari yako mama”
Mama Lukas akacheka sana kwani nilimuacha njia panda.
“Haki ya Mungu nimefurahi sana. Ninawaomba siku nikihamishia familia yangu huku, ninawaomba basi mtoto wenu awe na urafiki na Lukas wangu”
 
“Usijali hilo hadi sasa hivi tumesha kuwa marafiki, Mungu atatutangulia kwenye maisha ya huko mbeleni”
“Kweli kweli”
Sauti ya muhudumu akituomba tuweze kufunga mikanda ya siti tulizo kalia, ikakatisha mazungumzo ya bi Jane Klopp na mama Lukas. Mama Lukas, alipo ona nina hangaika kuufunga mkanda wa siti yangu akanisaidia, na akaubana vizuri kiunoni mwangu.
Huku nikiwa ninachungulia dirishani, nikaanza kuona jinsi ndege inavyo tembea kwani baadhi ya ndege zilizo simama, tunaziacha zilipo simama.
 
“Huogopi kuangalia nje?”
Mama Lukas aliniambia huku akinitazama.
“Hahaa hapana siogopi”
“Kweli?”
“Ndio”
Ndege ikaanza kunyanyuka taratibu, matumaini ya kuishi maisha mapya yakazidi kujengeka. Machozi yakaanza kunilenga lenga, kwani ninaiacha nchi ambayo ndio niliyo zaliwa. Ila kutokana na maisha tu ina bidi niondoke nchini hapa, huku moyoni mwangu nikiendelea kujiapiza kwamba ni lazima siku moja nihakikishe kwamba nimeiutawala mji wa Dar es Salaam, japo sifahamu nitautawala vipi. Uchovu wa kuto kulala usiku kucha ukanitawala, taratibu nikaanza kusinzia na mwishowe usingizi mzito ukanipitia.. 
 
“Ethan….amka upate chakula”
Sauti ya Mama Lukas, ikasikika vizuri masikioni mwangu, nikayafumbua macho yangu na kumtazma, nikamuona muhudumu wa kike akiwa amesimama pembeni yetu akijawa na tabasamu.  Nikajiweka vizuri kwenye siti yangu huku nikijaribu kumtazama bibi Jane Klopp na mumewe sehemu walipo kaa wapo, bi Jane Klopp akanipungia mkono huku akiw ameshika sambusha mkononi mwake. Nikatabasamu kidogo kisha nikamtazama muhudumu.
 
“Unahitaji nini mtoto”
“Sambuza na juisi?”
“Ngapi?”
Nikamjibu kwa kumuonyeshea vidole vyangu vya mkono wa kulia, nikimaanisha kwamba ninahitaji sambusa tatu.
Muhudumu akaondoka na kutiacha na mama Lukas, ambaye naye anapata chakula aina ya tambi taratibu.
“Tumetembea sana enee?”
“Hahaa ndio hasi sasa tuna masaa manne angani”
“Sawa”
Muhudumu akaniletea nilicho muagiza, akanisaidia kunikunjulia kijimeza changu kilichopo pembeni ya siti yangu. Akaniweka chakula changu, akanikaribisha na kuondoka. Taratibu nikaanza kula sambusa moja huku nikiwa na furaha moyoni mwangu.
“Ethan”
“Naam”
“Unapenda kuwa nani mkubwani?”
Nikamtazama Mama Lukas kwa muda huku nikifikiria cha kumjibu, kwani maisha yangu ninahitaji kuwa mtu mwenye nguvu ila sifahamu ni nguvu ya namna gani ambayo ninatakiwa kuwa nayo.
 
“Aha…nahitaji kuwa mtu mzuri nitakaye pendwa na watu”
“Mbona hata sasa hivi ni mtu mzuri na unapendwa na watu. Maana ya swali langu ni kwamba unapenda kuwa nani, labda rubani kama hawa wanao endesha hii ndege, au mwalimu….”
“Ahaaa….ninataka kuwa mwana michezo”
“Mchezo gani unapenda?”
“Mpira”
“Kweli?”
“Ndio”
“Basi inabidi ujitahidi na kuwa kama kina Mbwana Samatta, je una mfahamu?”
Nikatingisha kichwa nikimaanisha kwamba simfahamu, mama Lukas akafungua pochi yake na kutoa simu. Akaanza kunionyesha picha za mchezaji huyo aliye nitajia jina.
“Huyu ni kijana Mtanzania, kwa sasa anacheza huko nchi za nje. Sasa na wewe kama unataka kuwa mchezaji wa mpira basi unatakiwa kujitahidi kuwa zaidi ya huyu”
“Ila yeye ni mkubwa tayari?”
“Yaa na wewe si utakuwa mkubwa, ukiwa tu mkubwa hakikisha kwamba unacheza mpira vizuri na uwe mahiri sawa”
“Sawa nitakua”
“Tupige”
 
Mama Lukas alizungumza huku akinionyesha kidole chake cha mwisho cha mkono wake wa kulia, tukakutanisha vidole vyetu na kumfanya bibi Jane Klopp na mume wake kutabasamu kwa kitendo hichi ambacho ni cha furaha sana.
“Yeah usipo kuwa tu mchezaji mzuri basi siku tukionana nitakuuliza kwa nini hujawa”
“Sawa”
Safari hii kusema kweli ni nzuri sana, sikujisikia unyonge hata kidogo kwenye ndege. Safari ya kutoka nchini Tanzania hadi Ujerumani, ikachukua msaa mia moja ha hamsini ambayo ni sawa na siku mbili na masaa saba. Tukafika nchini Ujerumani, ikiwa ni majira ya usiku. Baridi kali ya nchi hii, ni tofauti kabisa na baridi ya nchini Tanzania tena kule Arusha nilipo kuwa nikiishi. Tukaagana na mama Lukas, akaingia kwenye gari alilo kuja kuchukuliwa watu wa Ubalozini kisha nasi tukapanda gari nzuri sana ya milango sita ambayo mzee Klopp na mkewa wamekuja kuchukuliwa.
 
“Hapa ni Berlin ukiwa unasoma kwenye masomo ya historia, utaweza kusoma mji hu wa Berlin. Hapa ndipo ulipo fanyika mkutano wa kusuluhisha vita kuu ya dunia”
Mzee Klopp aliniambia huku akinionyesha majengo makubwa na mazuri kuliko hata yale niliyo yaona jijini Dar es Salaam.
“Ni pazuri?”
“Yaaa hapa ni pazuri sana, ila kesho mama yako akipata muda basi unaweza kukutembeza na ukazidi kufahamu uzuri wa eneo hilo”
“Usihofu Ethan, tutatembea karibia nchi nzima ili mradi tu uweze kuifahamu vizuri sana, kwa maana muda wa kuanza shule bado”
“Yaa utaanza mwezi ujao”
“Sawa sawa wazazi wangu”
 
“Sisi hapa Berlin tuna makampuni yetu mawili, moja inahusika na maswala ya kutengeneza magari  na nyengine ni hospitali inayo husika na magonjwa ya moyo”
“Ahaaa”
“Katika hiyo hospitali, dada yako ndipo anapo fanyia kazi, yeye ndio msimamizi mkuu wa hospitali hiyo”
Bibi Jane Klopp alinipa maelezo hayo niliyo yaelewa vizuri sana. Tukafika katika jumba moja kubwa sana lililo zungukwa na miti mingi na mirefu sana kwenda juu.
“Hapa ndipo tunapo ishi, kidogo tupo nje ya mji. Tumesha kuwa wazee sasa na hatuwezi kukaa mjini”
“Ahaa”
Taratibu geti likafunguka na gari likaanza kuingia taratibu hadi kwenye eneo la kusimamia. Nikamuona binti mmoja mrefu akiwa amesimama nje huku akionekana kujawa na shahuku kubwa sana ya kuweza kuwaona watu walipo ndani ya gari. Taratibu dereva akatufungulia mlango, akaanza kushuka mzee Klopp, binti huyo akamkumbatia baba yake kwa furaha sana, akashuka bibi Jane Klopp kisha nikafwatia mimia. Binti huyu akamkumbatia bibi Klopp.
 
“Mery kutana na Ethan”
“Mambo Ethan”
Binti huyu alizungumza kwa furaha kidogo.
“Safi tu dada”
Ethan huyu ni Mery ndio yule binti yetu tuliye kuambia.
“Nashukuru kukutana na wewe dada Mery”
Nilizungumza huku nikimpa Mery mkono, akautazama kwa muda mkono wangu kisha akaupotezea na kujifanya ana kwenda kusaidia kushusha mabegi kwenye gari. Kitend hichi kusema kweli kikanifanya nijisikie vibaya hadi Mzee Klopp na mkewa walakifahamu hilo.
“Mzoe si unajua madaktari wana mambo mengi”
Bi Jane Klopp alijitahidi kunifariji, ila hata wao hawakupendezewa na jambo hili. Tukangia ndani ya jumba hili kubwa, kusema kweli ni jumba ambalo limejengeka vizuri sana. Bibi Jane akanionyesha chumba changu cha kulala, nikaweka begi langu kisha tukarudi sebleni na kupata chakula kilicho andaliwa vizuri sana. Ila muda wote nikajikuta nikimtazama Mery na kujiuliza ni kwa nini amenidharau.
 
“Mery unatakiwa kumuomba msamaha Ethan kwa kuto kuupokea mkono wake.”
Mzee Klopp alizungumza huku akinimtazama Mery.
“Baba na mama pasipo kuwavunjia heshima siwezi kumuomba huyo sokwe msahama, na inakuwaje munaleta Masokwe nyumbani kwetu na wala hamjanishirikisha eheee?”
Kauli hii, ikaulipua moyo wangu, hasira ikapanda na kunifanya mwili mzima kunitetemeka, glasi ya juisi niliyo ishika mkoni mwangu, nikajikuta ikiniponyoka na kuanguka chini jambo lililo wafanya watu wote kunishangaa.

ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )