Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, October 6, 2018

Serikali Yatangaza ajira mpya 171

Watumishi wapya 513 wa kada mbalimbali za afya wameajiriwa na Serikali ili kujaza nafasi zilizoachwa na wenzao waliochaguliwa awali na kushindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi walivyopangiwa.

Watumishi hao 513 ni kati ya watumishi 6,180 walioajiriwa na kupangiwa vituo vya kufanyia kazi ikiwa ni zahanati na vituo vya afya katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Nchi, Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema Oktoba 5, 2018 kuwa licha Serikali kutoa ajira hizo bado kuna kada ambazo zimekosa watu wenye sifa wa kuajiriwa na Serikali.

Amezitaja kada ambazo hazijapata watu wenye sifa wakati wa shughuli ya kuajiri ni pamoja na ile ya ofisa uuguzi msaidizi daraja la pili, ofisa muuguzi daraja la pili, daktari daraja la pili, tabibu daraja la pili, na tabibu msaidizi.

Waziri Jafo amezitaja kada nyingine zilizokosa watu wenye sifa ni pamoja na nafasi ya mteknolojia mionzi, mfamasia daraja la pili na mtoa tiba kwa vitendo.

Aidha, Serikali  imetangaza ajira mpya 171 za kada mbalimbali za sekta ya afya ambapo nafasi hizo zinapaswa kuombwa kuanzia Oktoba 5 2018 hadi  Oktoba 12 2018.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )