Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, October 24, 2018

Serikali Yawapatia Huduma Ya Usafiri Wajane Wa Aliyekuwa Makamu Wa Rais Wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe

Serikali imewapatia huduma ya usafiri wa gari wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Viongozi wa Kisiasa Na. 3 ya mwaka 1999 na Marekebisho yake ya mwaka 2005 inayoelekeza utoaji wa stahili kwa wajane wa viongozi wa Kitaifa Wastaafu.

Akikabidhi gari hilo kwa wajane hao jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) amesema licha ya kuwa ni utekelezaji wa sheria lakini pia ni sehemu ya kuuenzi mchango wa wastaafu katika ujenzi wa taifa letu.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo, stahili za wajane kwa viongozi wa Kitaifa Wastaafu ni pamoja na malipo ya pensheni, malipo ya posho ya matunzo ya kila mwezi, gharama za matibabu katika hospitali zilizomo nchini na kupatiwa huduma ya usafiri.

Akizungumzia mchango wa Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Mhe. Mkuchika amesema, alikuwa ni kiongozi mahiri, jasiri na mchapakazi aliyeweza kutuliza machafuko yaliyowahi kutokea Zanzibar na amefanya kazi ya kuwaunganisha watanzania.

Kwa upande wake, mmoja wa mke wa Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi. Zeyana Rashid ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuihudumia familia hiyo kwa kuipatia mahitaji yote muhimu.

Ziara za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) ni mwendelezo wa kuwajulia hali viongozi wa Kitaifa Wastaafu kwa lengo la kuboresha huduma wanazopatiwa na Serikali.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...