Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, October 16, 2018

Taifa Stars Yaichapa Cape Verde Bao 2-0 Uwanja wa Taifa Dar

Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 leo dhidi ya Cape Verde kwenye mechi yake ya 4 Kundi L kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019 nchini Cameroon.

Mabao hayo yaliyofungwa na  nahodha, Mbwana Samatta na Saimon Msuva sasa yamefufua upya  matumaini ya Taifa Stars kufuzu kwa fainali  hizo za Mataifa ya Afrika mwakani .

Mshambuliaji Difaa Jadidi, Msuva alifunga bao la kwanza kwa Stars akimalizia vizuri krosi ndogo ya Samatta aliyewatoka mabeki wanne wa Cape Verde na kupiga krosi iliyomkuta mfungaji.

Samatta alifanya kile walichosubiri mashabiki wa Tanzania katika kipindi cha pili kwa kufunga bao la pili kwa shuti kali akiwa ndani ya 18, baada ya kupokea pasi ya Mudhathir Yahya.

Ushindi huo unaifanya Taifa Stars kupanda hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 5, wakati Uganda wakiongoza Kundi L kwa pointi 7, wakati Cape Verde ya tatu na pointi 4 na Lethoso ya mwisho ikiwa na pointi 2.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )