Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, October 22, 2018

TFF Imemthibitisha, Ammy Ninje Kuwa Mkurugenzi Wa Ufundi

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza kocha wa zamani wa Serengeti Boys, Ammy Ninje kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa Shirikisho hilo akichukua nafasi ya Salum Madadi.

Madadi aliondolewa katika nafasi hiyo mapema mwaka huu na kukaimiwa na Oscar Milambo ambaye baada ya uamuzi huu atarudi katika majukumu yake ya ukocha.

Ofisa habari wa TFF, Mario Ndimbo alisema kikao cha kamati tendaji ya TFF kilichokutana Jumamosi ya Oktoba 20 kilipitisha uamuzi wa kumteua Ninje.

"Ninje ndio atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi kwa sasa na anatakiwa kuanza kazi mara moja kwani TFF inatambua anaishi Uingereza, lakini kuanzia sasa atarudi hapa nchini katika kituo chake cha kazi, " alisema.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...