Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, October 3, 2018

Tunayo Hapa Habari Njema Toka Hospitali ya Taifa Muhimbili Kama Una Mgonjwa Anayesumbuliwa na Haya Magonjwa

Napenda kuwataarifu kuwa hivi karibuni, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanzisha utoaji wa huduma za tiba radiolojia(interventional radiology)inayohusisha utaalam wa kutumia vifaa vya radiolojia kama MRI, CT-Scan, Ultra-Sound na X-RAY kutibu moja kwa moja au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.

Tayari tumeanza kuondoa uvimbe kwenye sehemu ya kinywa, uso na shingoni (sclerotherapy forhaemangioma and lymphangioma),kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya kutoa mkojo imeziba(nephrostomy tube placement), kuzibua mirija ya nyongo iliyoziba(percutaneous trans hepatic biliary drainage) na kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba(fallopian tube recanalization). Tiba nyingine ni kunyonya usaha ndani ya tumbo(abscesses drainage)

Kutokana na mafanikio hayo, napenda kuwataarifu kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na Chuo Kikuu cha Yale kilichopo nchini Marekani tumeandaa kambi maalumu ya kufanya uchunguzi na kutoa tiba radiologia kuanzia tarehe 22 Oktoba hadi 9 Novemba 2018, hivyo tunaomba mtume wagonjwa wenye matatizo yafuatayo:

Diagnosis/
Ugonjwa
Lung abscess/nodules/masses
Uvimbe / majipu kwenye mapafu
Liver abscesses/nodules/masses
Uvimbe / majipu kwenye ini
Kidney abscesses/nodules/masses
Uvimbe /majipu kwenye figo
Biliary system obstruction with dilatation
Mfumo wa nyongo ulioziba
Renal obstructive uropathy with severe hydronephrosis
Mfumo wa mkojo ulioziba
Abscesses/ collections anywhere (abdominal/pelvic/peritoneal)
Uvimbe /majipu ndani ya tumbo na nyonga
 
Gharama za Matibabu!
Wenye bima za afya waje nazo,wasiokuwa na uwezo tutawapa exemption.Kumbuka kuwapa barua za rufaa waje nazo.

Imetolewa na
Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja
Hospitali ya Taifa Muhimbili
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...