Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, October 7, 2018

Vijana Nchini Waaswa Kuanzisha Miradi Ya Kimkakati itakayowawezesha kiuchumi.

Vijana nchini wametakiwa kubadili mtazamo kwa kuanzisha miradi ya kimkakati itakayowawezesha kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipofanya ziara hiyo Mkoa wa Iringa kwa lengo la Kuhamasisha na kukagua maeneo ya ujenzi wa Vitalu Nyumba (Green House) na uwepo wa miundombinu itakayotumika kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Mhagama amesema sekta ya kilimo inaajiri na kuchangia katika pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 60%, hivyo vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wakatumie rasilimali ardhi kama mtaji wa kujiajiri na kuweza kuajiri wenzao.

“Lengo letu ni vijana kutumia sekta hii ya umahiri kwa ajili ya kuwaondoa kwenye mitazamo finyu na kuwa na mitazamo chanya ili waweze kunufaika na miradi itakayo buniwa na kutumika kama mfano kwa vijana nchi nzima.” Alisema Waziri Mhagama

Aliongeza kuwa vijana watafundishwa kilimo cha Kitalu nyumba ambavyo vitawawezesha kuongeza thamani kwenye mazao watakayozalisha na mradi huo ukawe sehemu ya ajira zao.

Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa taifa kwa kushirikiana kwa pamoja bila kujali itikadi zao ili kutimiza adhima ya vijana wote.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela alisema mradi huo utawawezesha vijana wa mkoa wa Iringa kuweza kuondokana na changamoto ya ajira kwa kuwa Serikali imewaletea teknolojia hiyo itakayo wawezesha vijana kujiajiri.

Naye mmoja wa vijana aliweza kuishukuru Serikali kwa kuanzisha mradi huo wenye tija ya kuwanufaisha vijana wote katika kuwaletea mabadiliko na ukombozi wa kiuchumi.

“Mradi huu utatuwezesha sisi vijana kunufaika na teknolojia hii ya kilimo cha kisasa kwa kutumia sehemu ndogo ya mashamba kuzalisha mazao mengi yatakayotusaidia kujipatia mtaji ili tuondokane na umaskini.” Alisema Peter Seni

Katika Ziara hiyo Waziri Mhagama alitembelea Chuo cha Ihemi kwa ajili ya kukagua majengo yatakayokuwa yanatumia kufundishia vijana elimu ya ujasiriamali na kilimo cha kitalu nyumba (Green House). 
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )