Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 5, 2018

Wananchi Wafurika Tandale Kusherehekea Siku ya Kuzaliwa Msanii Diamond ikiwa ni Pamoja na Kupatiwa Mitaji, Bima

Mwanamuziki Naseeb Abdul, 'Diamond' amesimamisha shughuli zote za Tandale na kuwafanya mamia ya wakazi wa kitongoji hicho kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Magunia kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Mamia ya wanawake wamefurika kwa ajili ya kuandikisha majina ya kupatiwa mitaji na bima za afya za watoto.

Uandikishaji huo umeanza tangu asubuhi katika uwanja huo, ambao wanawake wameonekana kuwa katika foleni kwa watu watatu tofauti waliopewa kazi ya kuandika majina.

Shughuli nyingine atakazofanya Diamond ni pamoja na kugawa bodaboda kwa vijana, kukarabati shule zote za msingi za Tandale akianza na ile aliyosoma, kuchinja ng’ombe nyumbani alikozaliwa na kula na wanaTandale huku siku ya Jumapili anatarajiwa kufanya sherehe kubwa na marafiki zake katika boti ya kifahari.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )